Elections 2010 [NOT CONFIRMED]: Prof. Mlambiti (wa Uchumi SUA) naye ashinda Ulanga

prof. Mlambiti wa chadema ndie mshindi na kinachosubiriwa ni nec ulanga kumtangaza, tarafa za malinyi na ngoheranga historically ndio ngome thabiti za ccm lakini 2010 wameamua kuchagua mtu na siyo chama, msingi wa taarifa yangu jamvini unategemea fact hizi.

tarafa za ngoheranga na malinyi zina kata tano katika hizo tano ccm wameshinda 4 na chadema 1 hiyo ni udiwani, kwenye ubunge kura 75 % zote zimeenda chadema, maana prof ameshinda almost 99 polling station za tarafa hizi isipokuwa vijiji vya ihowanja na mbalinyi. Hapa ameshinda sana kwa sababu ya majeraha ya kura za maoni hususani vijana waliojitokeza kumuangusha dkt.ngasongwa baada ya wao nao kuchakachuliwa na tabibu mponda kwa nguvu ya celina kombani na ccm wilaya wakaiasi ccm na kumpigia debe prof. Mlambiti, kosa lingine ni kitendo cha mgombea wa ccm tabibu hadji mponda ni kuitenga na kuidharirisha kambi ya ngasongwa ktk kampeni zake kwa imani kuwa yassin njayagha na simon ngonyani watamsaidia hali ikawa ni tofauti sana maana hao aliowategemea ndio waliotuma majeshi ya kummaliza. Alisituka kuitafuta shuka alfajiri kuwa jamaa wanammaliza tena baada ya ujio wa kingunge jimboni aliyeagiza wagombea wote ktk kura za maoni warudi jimboni na kumtaka dkt ngasongwa akaokoe jahazi, bahati mbaya dkt ngasongwa akiwa ktk safari ya kuitikia wito akapata ajali njiani na kumfanya kukosa sehemu kubwa ya kampeni za lala salama ingawaje ndio aliwaokoa madiwani wa ngoheranga, biro na ihowanja. Dakika za lala salama ccm waliliona tatizo na kuwataka njaygha na ngonyani wakasafishe sumu walioipanda jimboni kama wasemavyo waswahili siku ya kufa nyani vijana hao wakiwa ktk gari moja walipata ajali sehemu ileile ambayo dkt ngasongwa alipatwa na ajali na kujikuta wanarudi mjini ifakara kwa matibabu na kumuacha tabibi hadji mponda akipata sapoti toka kwa alhaj ngasongwa ili kuirejesha malinyi ccm.

tarafa ya mtimbira takwimu zaonyesha kuna kata 6 katika hizo chadema ameshinda mbili lakini kura za ubunge zimegawanyika 55% ccm na 45 chadema, hii imetokana na uzawa wa wagombea wote wawili, wote wanatoka tarafa hiyo na ni wapogoro vidabagha tabibu hadji mponda kwa mtimbira yeye ni mhamiaji lakini prof ni mzawa halisi wa mtimbira, kinachosumbua hapa ni wanamtimbira kuwekwa njia panda ila advantage imekwenda kwa prof.mlambiti na chadema, tarafa ya lupiro kuna kata tano chadema wamezinyakua 2, katika ubunge kura zimegawanyika kwa 55 chadema na ccm 45, hii imetokana na majeruhi wa kura za maoni ccm ndg njayagha ambaye ni mzaliwa wa lupiro kumuunga mkono prof.mlambiti .

mtaji mkubwa hapa ni kura za maoni ndani ya ccm, uongozi wa ccm mkoa na wilaya ulielekeza nguvu ya kumng'oa hasimu wao mkuu dkt ngasongwa wakiamini kuwa tatizo lao ulanga magh ni ngasongwa wakasahau kura jimboni humo ni za mtu si chama. Katibu wa ccm alikula 5m toka mgombea wa ccm anayeshindwa uchaguzi sasa na kijana ngonyani na mkiti alikula mzigo kwa wagombea wa udiwani karibu wote ++yassin njayagha.
kwa msingi huo prof.mlambiti ndio chaguo la ulanga magharibi 201-15.

ktk hali hii ccm ulanga 2012 inatakiwa ifanyiwe overhaul halisi kuelekea 2015,ccm tujipange upya 2015.

Nimekuogopa wewe unadata mno!
 
ASANTE FDR, JR. KWA TAARIFA ZA KINA SANA.
Tunaomba utujuze zaidi jinsi mambo yatakavyoenda kwa ujumla wake
 
Duh FDR.Jr nimekukubali kwa data za ulanga... Tafadhali endelea kutujuza zaidi.
 
Bravooooo my prof.... You deserve it.. Kaza buti kanyaga twende tukalete ukombozi.
 
Habari za punde ulanga magharibi kuna mchezo unataka kufanywa kumpoka ushindi prof mlambiti, tarafa ya mtimbira ambako wagombea wote wawili wanaopambana wanatokea matokea hayajawekwa hadharani mpaka daki 5 zilizopita, kuna kada mmoja wa chama cha mapinduzi ameatawanya habari kuwa ccm imeshinda kwa kura 12 dhidi ya elfu nane za prof mlambiti. Takwimu hizi si za ukweli ila wanaangalia prof mlambiti amempiku kwa difference ya kura ngapi mponda ili wamchakachue, kada huyu anaitwa kanduru. Hizi ni taarifa za ndani ya kambi ya ccm

tume yenyewe ahaijasema lolote mpaka sasa licha ya kuwa jana iliahidiwa kuwa leo saa sita usiku matokeo yangelikuwa hadharani.

Chadema makao makuu wanapaswa kuilifuatilia jambo hili kwa speed ya umeme vinginveyo ccm watampora kura prof.mlambiti
 
12 elfu wadau kwa 8elfu. Kimsingi hapa naliona tatizo, chadema taifa watoe macho makavu vinginevyo celina kombani anampitisha mtu wake kwa kura za maruhani.
 
habari njema hizi! nguvu ya umma !!!!!!!!!!!! mwenyezi mungu ni mkuu!
 
Taarifa nilizo nazo ni mchezo uleule waliomfanyia dkt. Ngasongwa pale mtimbira, kura zinazoingizwa sasa toka mtimbira ni zile za kupikwa ili kumpa margin mgombea wa ccm. Kuna taarifa wazi kuwa mawakala wa chadema pale mtimbira wamenunuliwa kwa fedha ili kuruhusu mchezo huo ufanywe na kuzibariki kura hizo, sasa sijajua upande wa chadema wao wanasemaje juu ya hili. Maana takwimu hazituonyeshi kuwa kuna wapiga kura wa kiasi hicho mtimbira.

Chadema makao makuu kama wamo humu wawashe helicopter waende huko kumnusuru prof mlambiti.
 
Duuuuu, Prof namkubali. Nakumbuka siku aliyomuuliza maswali magumu Mh. Mkapa pale freedom square Mazimbu Campus - Morogoro, sasa akiingia mjengoni itakuwaje!!!!!!!!!? Upumbavu na ubabaishaji mjengoni utaisha.
 
Upinzani umechukua kata ya sOFI baada ya mpambano wa vijana wenzangu wazawa wa kiswago kudra kikohi ccm na machawa wa tlp, tlp udiwani wameshinda kwa tofauti ya kura 21, hivyo ulanga magharibi upindanzani umebeba madiwani malinyi mjini, sofi, kata 2za itete, lupiro na kivukoni na zilizosalia ni ccm-kilosa kwa mpepo,ngoheranga,biro,igawa, usangule na mtimbira. Naomba kurekebisha kuwa kata ni 12 na si 16 hivyo. Narudia tena kuwa chadema wanapaswa wakamsaidie prof. Mlambiti kula mahenge asidhulumiwe.
 
jumla ya kata ni 15,CCM imepata-10
upinzani-5
inasemekana wachakachuaji watashinda,
Ulanga mashariki ccm wameshinda {celina kombani}
 
jumla ya kata ni 15,ccm imepata-10
upinzani-5
inasemekana wachakachuaji watashinda,
ulanga mashariki ccm wameshinda {celina kombani}

kata za ulanga magharibi ni hizi hapa
  1. kivukoni-chadema
  2. mavimba/minepa-ccm
  3. lupiro-chadema
  4. kichangani-ccm
  5. iragua-ccm
  6. itete-chadema
  7. njiwa-chadema
  8. mtimbira/madira-ccm
  9. mtimbira-usangule-ccm
  10. sofi-tlp
  11. malinyi-chadema
  12. igawa-ccm
  13. biro-ccm
  14. ngoheranga-ccm
  15. kilosa kwa mpepo-ccm
ukweli ndio huo na ni mtindo uliomuondoa dkt ngasongwa ktk kura za maoni chini ya uratibu wa celina kombani,ccm wilaya na mkoa ndio umetumika kumtoa roho profesa mlambiti.

amini usiamini mtimbira hawana vote za kumshindisha mgombea katika hali ya namna hiyo. Tafakarini wana ulanga na tupatieni majibu
 
kata za ulanga magharibi ni hizi hapa
1. kivukoni-chadema
2. mavimba/minepa-ccm
3. lupiro-chadema
4. kichangani-ccm
5. iragua-ccm
6. itete-chadema
7. njiwa-chadema
8. mtimbira/madira-ccm
9. mtimbira-usangule-ccm
10. sofi-tlp
11. malinyi-chadema
12. igawa-ccm
13. biro-ccm
14. ngoheranga-ccm
15. kilosa kwa mpepo-ccm
ukweli ndio huo na ni mtindo uliomuondoa dkt ngasongwa ktk kura za maoni chini ya uratibu wa celina kombani,ccm wilaya na mkoa ndio umetumika kumtoa roho profesa mlambiti.

amini usiamini mtimbira hawana vote za kumshindisha mgombea katika hali ya namna hiyo. Tafakarini wana ulanga na tupatieni majibu 2015
 
Msongoru kama una presha we usiangalia mtandao jikalie tu nyumbani ule vitoga, ukiangalia mtandao huu uwe na kifua, si umesikia watu wanakimbizwa hospitali ?
 
ukweli ndio huo na ni mtindo uliomuondoa dkt ngasongwa ktk kura za maoni chini ya uratibu wa celina kombani,ccm wilaya na mkoa ndio umetumika kumtoa roho profesa mlambiti.

ndo kusema mlambiti hajashinda?
 
Back
Top Bottom