North Mara: Kashfa ya maji ya sumu toka mgodini!


Hivi Kikwete anasoma au anapata habari kama hizi? na kama hapati au whatever kisingizio atakachotoa kuhusiana na hili, je anaendelea kujiita kuwa ni Raisi wa Tanzania na kamanda mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa watanzania wote (ikiwemo hawa wa North Mara) ?
 
Mods unganisheni hizi zote...thread na ile ya mwanakijiji tuwe tunachaningia pamoja...
Nmara,Nmara,Nmara,ohhhhhhhh

Sidhani kama kuna tatizo lolote hii ikiwa hapa peke yake watu wakachangia pia. Wanaochafua mazingira huko North Mara lazima waanikwe vya kutosha hapa jamvini.
 

Ukisikia spinning ya hali ya juu ambayo bado imeangukia pua basi hapa kwa maelezo haya (utetezi wa wachafuzi wa mazingira) ni makao makuu.
 
Serikali kiziwi, yenye upofu na ububu katika masuala yanayohusu wananchi wake! Nifahamuvyo mimi, mkataba wa wananchi na watawala wao ni kwamba serikali na dola yake iwalinde wananchi in return of the priveldge wanazopata. Tanzania yetu ulafi umeongoza. Serikali haina cha kusaidia. Kila mtu afe kivyake. Maajabu ni kwamba kuna mtu bado anakwenda kwenye chumba cha kupiga na kura na kusema next time ccm, Lord have mercy!
 

nimeipenda sana hiyo in red, inawezekana huyu Buswelu ndiye Dr Burian mwenyewe au mtu wa karibu naye au ndiye aliyeaandaa report iliyosomwa na bi burian mjengoni...inauma sana kama mtanzania anaweza akasema kodi za serikali ni muhimu kuliko maisha ya watanzania!!we need people to think differently in a positive way siyo hata matope unayanadi ni different thinking while what he is saying/writing does not involve thinking at all...in short Buswelu did not think,he/she just wrote.
 
MKUU wa Wilaya ya Tarime, Frank Uhahula amesema kwamba uongozi wa Kampuni ya Barrick inayochimba mgodi wa dhahadu wa North Mara haukudanganya kuwaonyesha maeneo yanayotiririsha maji yanayodaiwa kuwa na ‘sumu’ kwenye Mto Tigithe.

Kauli hiyo ya Uhahula inaelekea kupingana na aliyotoa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamisi Kagasheki alipofanya ziara kwenye mgodi huo kupata uthibitisho wa maafa makubwa yanayodaiwa kusababishwa na sumu inayotiririka hadi kwenye maji ya mto huo.

Mto huo unategemewa na maelfu ya wakazi wa eneo la Nyamongo lenye kata tatu za Kibasuka, Kemambo na Matongo. Maji ya mto huo hupitia kijiji cha Kewanja ambako ndiko tindikali asilia (siyo sumu) aina ya paf (potential acid forming material) huingilia kutoka kwenye rundo la mawe machafu yaliyowekwa na Barrick eneo la Gokona.

Lakini Uhahula, ambaye alikuwa anajibu maswali ya wataalamu, wabunge na mawaziri katika msafara wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ya Bunge chini ya Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, Jumatatu iliyopita, alisema Barrick hawakuwaficha chochote.

“Naapa haki ya Mungu, hapa tulifika,” alisema Uhahula huku akiashiria kukata shingo kwa kidole alichogusisha kwenye mchanga msafara huo ulipofika kushuhudia dimbwi dogo la maji mekundu mithili ya damu yaliyojikusanya kutoka kwenye mawe yenye tindikali ya paf katika eneo la Gokona.

“Naona imeingia siasa katika suala hili, maana hapa tulifika na pale tulifika pia,” alisisitiza Uhaula huku akionyesha maeneo hayo.

Hata alipoulizwa na Ndugai kwamba Kagasheki alidanganywa wapi, Uhahula alijibu hakuna.

“Tulipokuja na Barrick tulipandia pale, hatukusimama hapa tulipo,” alifafanua Uhahula akionyesha tofauti ya kama mita tano hivi.

Kamati hiyo ilitembelea maeneo yote yanayolalamikiwa ya Nyabirama, hasa Gakona ambako ni chimbuko la mkasa huo.

Eneo lote chini ya tuta kubwa kuelekea kwenye shamba la migomba ya ndizi limejaa maji yanayovuja kutoka kwenye mabwawa ya kuhifadhia maji yenye tindikali hiyo ya paf katika eneo hilo. Majani yote yanaonekana yamenyauka kutokana na tindikali hiyo ambayo kwa asili iko kwenye miamba inayochimbwa madini.

Tindikali hiyo ndiyo inadaiwa na wakazi wa Nyamongo kwamba, imesababisha vifo vya watu na mifugo kadhaa katika vijiji vya Nyakunguru, Nyarwana, Weigita na Nyangoto.

Wiki iliyopita wakazi hao walidai tindikali hiyo ilisababisha vifo vya watu 21, lakini kamati ya Ndugai iliambiwa vifo vimefikia watu 43, ng’ombe 401, mbuzi 523, kondoo 185, punda 63 na mbwa 227. Taarifa hiyo haina uthibitisho wa wataalamu.

Aidha, Kamati ya Ndugai iliambiwa pia kwamba kuna wagonjwa kadhaa walioathiriwa na tindikali hiyo pamoja na vumbi linalotokana na umwagiliaji wa maji hayo na linalotimuka kutokana na upasuaji miamba.

Vilevile, wanadai kwamba nyumba nyingi zimepata nyufa kutokana na mtikisiko wa shughuli za upasuaji na nyingine kupigwa na mawe. Pia wanadai kuwa vyanzo vyote vya maji vimepata tindikali.

Hata hivyo, wataalamu mbalimbali kutoka Baraza la Mazingira (Nemc), Bonde la Ziwa Victoria (Lake Victoria Initiative), ofisi ya Mkemia Mkuu na Barrick walisema kiasi cha tindikali hiyo ya paf (ph) haina uwezo wa kusababisha madhara hayo.

Kuthibitisha kwamba sumu hiyo pamoja na cyanide inayotumiwa kusafishia madini eneo la Nyabirama hazina madhara, Mtaalamu wa mazingira wa Barrick, Samwel Hailu na Ofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Tewell Tewell walikunywa maji hayo. Kamati ya wataalamu wa mazingira, afya, Mkemia Mkuu imepewa siku 14 kukamilisha kazi ya kubaini tatizo hilo.

Wiki iliyopita Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamisi Kagasheki alisema kuwa alitembelea mgodi huo kwa maagizo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili kujionea hali halisi na kujua ukweli wa mambo.

Akisimulia aliyokutana nayo katika mgodi huo, Balozi Kagasheki alisema alipokwenda alipokelewa vizuri na uongozi wa mgodi huo na kumtembeza katika maeneo waliyoeleza kuwa ndiyo yanayodaiwa kuwa chanzo cha kuvuja kwa sumu hiyo.

"Nilikwenda kutembelea mgodi wa North Mara, nikifuata maagizo aliyoyatoa Waziri Mkuu alipokuwa akitoa majumuisho ya hotuba yake ya bajeti. Nilipofika huko uongozi ulinipokea vizuri na kunitembeza katika maeneo waliyoeleza kuwa chanzo cha kuvuja sumu hiyo," alisema Balozi Kagasheki na kuongeza kuwa baadaye msamaria mmoja alimwambia kuwa wanamdanganya kuna eneo ambalo hali hiyo inaonyesha wazi athari za sumu hiyo.

"Baada ya kumfuata msamaria huyo nilijionea hali halisi, nikasikitika sana kwa sababu uongozi wa mgodi ulinidanganya. Niliyoyaona nitapeleka kwa Waziri Mkuu, kwa kweli si nzuri, itabidi nifikishe ripoti kwa Waziri Mkuu," alisema naibu waziri huyo akionyesha kukasirika na kusikitika kwa tukio hilo.
 
hawa nao yaani kunywa maji ndo kipimo kuwa maji hayana sumu??mbona kazi ipo hapa ..haya ngoja tusubiri
 
Ebu anagalia hii hapa fact,

13th July 2009..... Source NIPASHE







Itawasilishwa bungeni na kujadiliwa




Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Job Ndugai.



Taarifa ya uchunguzi wa mgodi wa North Mara ulioko wilayani Tarime mkoa wa Mara, imekamilika na itakabidhiwa kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, leo na wabunge kupata nafasi ya kuijadili wiki hii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Job Ndugai, ambayo ilifanya uchunguzi wa sakata zima, aliliambia gazeti hili katika viwanja vya Bunge mwishoni mwa wiki, kuwa kamati yake imekwisha kukamilisha kazi ya kuandika ripoti.
Kamati hiyo ilikwenda North Mara kufanya uchunguzi huo, wiki mbili zilizopita, kufuatia madai ya
wananchi wa eneo hilo kuwa maji ya mto Tigithe ambayo wanayatumia kwa matumizi yao na mifugo, yamechafuliwa na sumu inayotiririka kutoka kwenye mabwawa ya mgodi huo na kuingia mtoni.
Bila kuzungumzia kwa undani mambo ambayo Kamati yake imebaini, Ndugai alisema: “Sisi tupo na wananchi, hatuwezi kuwakumbatia wawekezaji.”
Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa (CCM), alisema Kamati yake imefanya kazi yake kwa usahihi na umakini mkubwa.
Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alisema kutokana na unyeti wa ripoti hiyo, atairuhusu Kamati ya Ndugai kuiwasilisha bungeni ili umma uweze kujua ukweli wa sakata zima. "Nitampa nafasi Mwenyekiti kuiwasilisha taarifa yake baadaye, kwa sababu ina 'public interest', tusubiri niipate," alisema Spika Sitta katika majibu yake ya maandishi kwa Nipashe.
Serikali ilifikia uamuzi wa kuchunguza madhara ya maji ya mto Tigithe kutokana na malalamiko ya wananchi wanaotumia maji hayo kuwa yamechafuliwa na sumu inayotoka katika mabwawa ya mgodi wa North Mara, unaomilikiwa na kampuni ya Barrick Gold Tanzania.
Kumekuwa na madai ya vifo vya watu zaidi ya 40 huku mamia ya mifugo ikidaiwa kufa; watu wengine wanadaiwa kuwa ni wagonjwa kutokana na madhara ya maji hayo.
Mimea pia imekauka kandokando ya mto huo.
Katika hatua nyingine, habari kutoka Mara zinasema licha ya Serikali kutamka kuwa maji ya mto huo kuwa hayafai kwa matumizi ya viumbe hai kutokana na kubainika kuwa na sumu, bado mgodi huo wa North Mara unaendelea kutiririsha maji yanayoingia kwenye mto huo, ambao maji yake yanatumiwa na binadamu na mifugo.
Mapema mwezi huu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamisi Kagasheki, alitangaza kuwa maji ya mto huo hayafai kwa matumizi ya binadamu, baada ya kujionea mwenyewe jinsi maji ya sumu yanavyotiririka kutoka kwenye mabwawa hayo hadi mtoni.
Siku chache tu baada ya kauli hiyo Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ikishirikiana na ile ya Nishati na Madini, zilifanya ziara na kujionea hali halisi sambamba na kukutana na wananchi na uongozi wa mgodi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian, akitoa taarifa ya serikali mara baada ya kikao cha majumuisho ya kamati hiyo kwa waandishi wa habari alisema maji hayo hayafai kwa matumzi ya binadamu.
Alisema kutokana na maji ya sumu kuendelea kuvuja na kuingia mtoni, itabidi wananchi watafutiwe vyanzo vingine vya maji, na kwamba kazi hiyo ifanyike haraka iwezekanavyo ili kunusuru maisha ya watu na viumbe wengine.
 
Haya, naona hii issue imelala mpaka uchaguzi...ripoti ya wataalum ilidai kuna haja ya upelelzi zaidi. Waliodaiwa waathirikia wamepimwa na la...hakuna uhusiano wa kisayansi. Kama ni hivyo basi watnzania tunastahili tuzo ya siasa.

Kama haitoshi sasa naona NGO zilizorusha madai bila ushahidi wa kisayansi zinaanza kubanwa....

Barrick Gold Corporation and African Barrick Gold would like to take this opportunity to respond to false allegations made by Foundation HELP, a non-governmental organization located in the Tarime District of Tanzania.
We are deeply concerned that Foundation HELP continues to circulate alarming material which attributes serious health ailments to the operations of the North Mara mine. The material in question features photographs of two persons, a young male and an elderly female, with severe skin conditions. Devoid of medical evidence of any kind, these images are the basis for a "call to action" against the mine and have been distributed widely via the internet by activist groups.
African Barrick Gold has taken a series of actions consistent with our commitment as a responsible corporate citizen. To be clear, any credible claim of a health issue associated with the company's operations (whether involving an employee or community member) would be assessed and any necessary medical assistance provided.

We have attempted to identify and locate these two individuals. Although we enlisted the assistance of government and village leaders, we have been unable to do so. No one has come forward or indicated they know these persons or could assist us.

We then consulted with a team of medical experts, namely Dr. Robert Weiss, President, Dermatology Society of South Africa, Dr. Rob Barbour, Chief Medical Officer for Barrick Gold Corporation, Dr. Mark Divall, an occupational health physician based in South Africa, and Mr. Yahya Kishahu, an occupational health specialist and academic with Muhimbili University College for Health Sciences of Tanzania.
They each examined the photographs and provided their assessment of the possible causes of the medical conditions afflicting the two individuals. Their analysis is limited to the images circulated and, to arrive at a comprehensive conclusion, a full medical examination and case history would be required.
Based on their assessment, however, the image of the elderly woman (identified as Mama Otaigo, allegedly from Weigita village) shows a condition that is entirely consistent with vitiligo, a chronic disorder that causes depigmentation of patches of skin. The causes or origins of this disease is largely unknown but is widely considered to have an immunological basis.
The image of a young boy (identified as Paul, allegedly from Nkerege village) is consistent with a form of ichthyoids (Lamellar), an inherited skin disorder which causes plate-like scaling of the entire body surface and is present at birth.
These medical disorders are chronic, long-term diseases caused by genetics, immunological or other conditions. They were not caused by impacts associated with the North Mara operation over the past year, as claimed by Foundation HELP.
As Dr. Weiss stated, "there is no doubt that neither of these conditions are the result of contaminated water." Furthermore, the two villages cited by Foundation HELP are located some 30 to 35 kilometers away from North Mara and both are upstream from the mine.


To our knowledge, Foundation HELP has made no effort to have these cases brought to the attention of authorities or a qualified medical professional. No effort has been made to contact the company or the mine.
Thus, we have concluded that Foundation HELP's claims are neither credible nor motivated out of concern for these two individuals. This organization is not raising awareness of a public health concern or seeking assistance for these alleged victims. Rather, this material exploits the ill-health of others to mobilize anti-mining sentiment and harm the reputation of our companies.
ABG has requested that Foundation HELP cease from repeating and circulating these defamatory allegations. Regrettably, their response has been to ignore this appeal, to circulate this material more widely, and avoid taking any responsibility for the truthfulness of their claims. For this reason, ABG directed legal counsel to contact this organization to seek a retraction of this material from circulation. We continue to strongly urge all those involved with Foundation HELP to be accountable and refrain from repeating these false allegations.
We are also concerned about the health and well-being of this young boy and elderly woman. On humanitarian grounds, ABG's medical professionals would welcome the opportunity to provide assistance by directing them to the appropriate medical experts.
As leaders in corporate social responsibility, Barrick and ABG are committed to making a positive contribution to local communities. To date, we have invested US$40 million in community programs and initiatives in Tanzania, including vital health programs which have benefited tens of thousands of people.
We will continue to ensure that our stakeholders have accurate information about the impact and benefits of our operations in Tanzania, today and in the future.
 
Hawa ndio Barrick, kazi kubadili tuu majina, wakawa ABG, sasa ni Acacia!. Why?.

P.
 
Hawa ndio Barrick, kazi kubadili tuu majina, wakawa ABG, sasa ni Acacia!. Why?.

P.

Wanazingatia ushauri mnaowapa wenyewe. Wanasheria wenu serikalini na waliowaajiri ndio kazi yao kuwapa mbinu za kuwaibia na kutakasa taswira mbele ya jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…