North mara gold mine Nyamongo

Wababa

Senior Member
Jul 21, 2011
158
14
Hbr zenu wana jamii, jamani mwenzunu nimewahi kufanya kazi katika migodi mbali mbali hapa nchini, ila cjawahi pata ona sehemu yenye wageni toka nje za nchi yani ma expart wengi wao wakitokea south africa, ghana, na uingereza, hawa jamaa kinachoumiza zaidi hawajui kazi ya aina yoyote, zaidi ya watu weusi wao ndiyo wafanyakazi wakubwa, ma expert hao kazi yao kubwa ni kuvuta sigara na kunywa kahawa, jamani serikali yetu ikwapi ije iwakague hawa watu, nahisi hata kuingia hapa tz itakua ni kwa ujanja ujanja.
 
huo ni uzaifu wa idara ya uhamiaji maanake wao ndo wanahusika zaidi
 
Yani ni noma m2 wangu, ukiwa unaingia kazini asubuhi utafikiri upo soth kila corner una meet na makaburu, tena wanakera xana alafu hawajui ki2 at the same wanapewa hela nyingi sana kila ijumaa huwa wanapewa cigaratte money ambayo ndiyo mshahara wa mwezi moja wa juniour emplyoee, tena ujue ni jinsi gani hawa watu bado wana discrimination kuna mess ya white people ambao ni seniours mess na juniour employees mess, 4really bado serikali haipo serious na hawa wageni wanaotoka njee wkt wabongo wanazimudu shughuli tena kwa ufanisi mkubwa, embu imagine mshahara wa expert mmoja ni sawa mara 30 ya mtanzania anayelipwa laki nane per mounth???
 
kuna mmoja yuko buzwagi eti katoka uk kaja kuwa meneja mahusiano kati mgodi wa buzwagi nawanakijiji.....kazi ipo tanzania
 
Ha ha ha nimecheka sana...Kuhusu ili Manager Mahusiano buzwagi alikuwa kama country manager wakati flan au consultant kati ya nmara na migodi mingine anajua mpaka kikurya yule.....Wewe wa nmara....pale panaitwa special zone....tatizo pamoja na mishahara midogo mnayo pewa bado hamko committed na kazi zenu...tuongee ukweli kuzuga kwingi...ukiambiwa..unasema nifanye kazi kwa bidii kwa mshahara gani.

Tumeshaona..malalamiko mengi ufanisi mdogo kwa kuangalia ulivyo andika tu unaonekana kilaza.....its all commitment njoo na argument nzuri hapa twende pamoja kikazi zaidi uone kwanini hawa jamaa wapo hapo sina maana nawatetea lakini nataka tuangalie na upande wetu.
 
Well-done yote kwa yote wa TZ pia tuna matatizo na tunasababisha haya yote maana hatuji-Commit vilivyo kwenye kazi zetu hii ni kuanzia ngazi za juu serikalini ndiyo maana utaona mikataba mibovu ya madini hakuna anayehoji watu wanasema hakuna taabu.
Hao wazungu wako commuted na kazi zao sana usishangae kuona hao jamaa hawajui kazi lakini wewe unawafundisha ili wakusimamie vyema na usipate mwanya wa kutegea ukiwa kazini.
Swala hapa ni kwa Wa-Tanzania tuwajibike katika kazi zetu za kila siku tuache umagimeze.
 
Huo mgodi upigwe stop mambo ya ajira yaangaliwe upya hapo, huku ni kutuibia na wapigwe fini ya maana kama dola milioni mia kazaa hivi next time wawe na somo la kukariri.
 
we uliwahi ulifanya mimi bado nafanya,wapo madereva wa magari ya mafuta,walinzi wa kupima watu pombe,wote hawa ni experts ambao kazi wamejifunzia hapa lakini wana mishahar ya zaidi ya usd 4000 wakati wazawa wa kazi hiyo wana chini ya usd 400
 
Me sipati picha na hao experts walioajiriwa kwaajili ya kuendesha hayo ma fuel truck, na hao wa wafilipino ******* flani kazi yao kuwapima watu pombe, mikataba mibovu ya madini ndiyo inaruhusu hivyo,
 
Ukweli ni kwamba Buzwagi kufikia hatua ya kuweka fuel attendant wa kigeni wamepitia mengi kama unakumbuka habari ya wizi na kufukuza wafanyakazi especialy dump track operator,supervisor ilikuwa ni kwa ajiri ya mafuta. Fine ni wanaiba kwa ajiri ya mishahara midogo..je is that a solution?

Yaani kama mshahara ni mdoogo basi uibe? Ndio watanzania tunatakiwa kuwa hivyo?. All in all kama mwekezaji ana una vidhibitisho kuwa locals wanaajiliwa na wanakuwa wezi wanamtia hasara anaweza kabisa kupeleka hivyo na kuruhusiwa kupata parmit ya kuleta expert..

Tunaiba na production inakuwa chini kwa kuwa usiku kucha wa shift tunashughulika na wizi...ukizingatia wakati buzwagi inafunguliwa serikali waliahidi kuwapa grid ya taifa 24 hr as special lini lakini haikuchukua muda kabla ahadi yako ku fail kabisa..na kulazimisha mwekezaji kuingia extra cost za kuagiza magereta ya kuzalisha umeme kwa ajiri ya mashine zake na hayo yanatumia mafuta...so is both tanzania goverment na sisi watanzania wenyewe...
 
Bora huko, hapa kwetu hata mmwagilia maua na bustani ni expat. Pia kuna expat anaefanya kazi ya kufukuza ndege pori kwenye kiwanja cha ndege lakin analipwa ma milioni
 
Back
Top Bottom