pole sana mdada, ni kwa nini ulienda kujenga nyumbani kwenu? kama ulikuwa na uwezo wa kujenga nyumba dadaangu kwa nini hukununua kiwanja chako ujenge? naandika huku naumia sana utafikiri ni mm ndo nafanyiwa hivyo. kwa upeo wangu unaweza kujenga kwenye kiwanja cha nyumbani iwapo umepewa urithi au ukaamua kujengea wazazi as a gift. sijui mapatano yako na wazazi hadi kuanza kujenga nyumba ni kuita ya kwako kwenye kiwanja cha familia labda utwambie tujue pa kuanzia kutoa ushauri.
A.K.A jini mikosi, nuksi......wabongo huwa tunakimbilia huku mapema sana...kwa staili itabidi umtafute ustaadh Michael ......mtaalamu wa Diamond akupatie jini mvuto.......utani tu!Pole dada yangu hapo kwa jinsi nilivyoona utalaumu mama,mume na hautapata majibu katika ali ya kibanadamu,mm nnacho ona kuna supirit of rejection inakutesa tafuta makanisa ya kiroho kwa jina la yesu itatoka coz umekataliwa na mume na wazazi pia
mweh mweh mweh!!!!!
Nilizani familia yangu tu matatizo. Kumbe tupo wengi jamani.
Ugombanishaji wa kifamilia ndio unaanzaga hivo, dada we.
Ulikuja kuambiwa na mtoto wa baba ako mkubwa.
Nawe ukaenda kuuliza kama ni kweli.
Na mama akajibu ni kweli.
Jiulize mazungumzo yao yalianzia na nini?
Na kwanini mama hakuja kukuambia wewe mwenyewe?
Mie nafikiri hao watoto wa baba ako mkubwa wanaona umependelewa, wewe kukaa hapo ikiwa wao walifukuzwa. Na wanataka na wewe pia ufukuzwe kama wao.
Nafikiri walienda kumlaumu au kulalamika ama kumuliza mama mbona wewe hakufukuzi? Ikiwa wengine aliwafukuza!!!
Ndio hapo mama ako akajibu, "nitamtoa na yeye pia nipangishe", maana kakaa muda mrefu sasa.
Umeona picha?
Ushauri wangu, fanya kama my brother.
Mwambie mama yako "hapa sitoki", nitakaa hapa hapa.
Ukitaka nitoke njoo niue mimi na wanangu.
Na waambie jamaa zako wote utakaa hapo hapo, mali za baba ako na mama ako alie kuzaa.
Utaona mama ako wala hatokufukuza, atawaambia nyie si mumemsikia alivo jibu? Hatoki, mimi nikamue mwanangu ili iweje? Akae tu.
Mie naona hao ndugu zako, jamaa zako wanakuonea wivu umependwa kupewa kiwanja ujenge. Hizo mali za baba ako na mama ako mzazi, wao wanataka kujingiza kwa vile wamekulea au mama ako aliwalea? Kha...
Sema hautoki, fanya lolote lile mama
NI mama yangu kabisaaaaaa, na ni msomi mzuri na ana nyumba Tano hapa Dar, na kapangisha zote, Lakini sijui ni nn kwa kweli, niombeeni, maana nimeanza kufunga na kusali ili Mungu anionyeshe ni nn kipo ndani yake.
mweh mweh mweh!!!!!
Nilizani familia yangu tu matatizo. Kumbe tupo wengi jamani.
Ugombanishaji wa kifamilia ndio unaanzaga hivo, dada we.
Ulikuja kuambiwa na mtoto wa baba ako mkubwa.
Nawe ukaenda kuuliza kama ni kweli.
Na mama akajibu ni kweli.
Jiulize mazungumzo yao yalianzia na nini?
Na kwanini mama hakuja kukuambia wewe mwenyewe?
Mie nafikiri hao watoto wa baba ako mkubwa wanaona umependelewa, wewe kukaa hapo ikiwa wao walifukuzwa. Na wanataka na wewe pia ufukuzwe kama wao.
Nafikiri walienda kumlaumu au kulalamika ama kumuliza mama mbona wewe hakufukuzi? ikiwa wengine aliwafukuza!!!
Ndio hapo mama ako akajibu, "nitamtoa na yeye pia nipangishe", maana kakaa muda mrefu sasa.
Umeona picha?
Ushauri wangu, fanya kama my brother.
Mwambie mama yako "hapa sitoki", nitakaa hapa hapa.
Ukitaka nitoke njoo niue mimi na wanangu.
Na waambie jamaa zako wote utakaa hapo hapo, mali za baba ako na mama ako alie kuzaa.
Utaona mama ako wala hatokufukuza, atawaambia nyie si mumemsikia alivo jibu? hatoki, mimi nikamue mwanangu ili iweje? akae tu.
Mie naona hao ndugu zako, jamaa zako wanakuonea wivu umependwa kupewa kiwanja ujenge. Hizo mali za baba ako na mama ako mzazi, wao wanataka kujingiza kwa vile wamekulea au mama ako aliwalea? kha...
sema hautoki, fanya lolote lile mama
hata mimi naona ni bora aachane na huyo mama yake akaanze upya ni maisha tubidii uliyokua nayo hadi kufika hapo ulipofikia naomba uiendeleze na ujipange upya utafute kiwanja kingine ujenge,maana huwezi kung'ang'ania kwenye kiwanja cha familia hususan mama kashakupa makavu live,cha msingi muombe akupe muda(ikiwezekana mkae kikao cha familia)ili utafute mwelekeo.Dah hata siamini kama huyo ni mama yako mzazi pole sana na jipe moyo kwani Mungu wetu ni mwema utafanikiwa tu.
Mimi nilienda kuomba kujenga kwenye kiwanja hicho , ni baada ya kushindwa maisha na vituko vya mume wangu, nikaenda kuomba kujenga vyumba viwili ili nitafute kwangu, baba akaja kunisalimia , akaniambia nijenge nyumba kubwa nikae maana hamna mtu atakayekuja kukusumbua,basi nikaona kama mwenye kiwanja katoa go ahed kwa nn nisijenge nkajenga . Baadae nikapata pesa nikaamua kuweka kitega uchumi ili niweze kuishi vizuri nisije nikamanga manga na wanaume tena nikapata magonjwa nikawaacha wanangu. Sasa nilianza kusikia kwa ndugu watoto wa mama mkubwa kuwa mama anasema hayo nikawa siamini, juzi nimeyasikia kwa kaka mtoto wa baba mkubwa, kuwa anasema haoni faida ya mm kuendelea kukaa pale, ikabidi nimfuate ndiyo akanipa live kuwa kama ni nyumba basi nitoe tofari zangu. kwa kweli nimechoka hoiii, nashindwa la kufanya , sipati usingizi, naona dunia imenisonga, pa kushika sina nifanyeje?
Natafuta mke.
Hayo makanisa yenyewe laana tupu hata wachungaji wenyewe laana mshauri lingine.
usipende ku-generalize eti makanisa na wachungaji ni laana tupu otherwise unatafuta HASIRA YA MUNGU! maana naona unafika mbali ktk comment yako! Take care my dear!!!
Habari wana JF, nimejiunga na hii Forums siku si nyingi, ila nimependa sana comment zenu , na ushauri mnaotoa kwa watu mbali mbali pale wanapoomba msaada wa mawazo, nami nikavutiwa nikaona bora nijiunge nanyi labda nitapata mawazo mazuri ambayo yatanifanya niendelee kuishi.
Mimi ni mtoto wa pili katika familia yetu, tulizaliwa wasichana wote 4, tulilelewa vizuri na kusomeshwa pia, bahati nzuri tulipata kazi na Mungu akabariki tuliolewa wote, ila katika maisha Mungu huwa na mipango yake, ndugu zangu wawili wakafariki dunia na kutuachia watoto ambao tunawalea mm na mdogo wangu.Katika kuishi huko mm ndoa ikanishinda ikabidi niachike, nikaenda kujenga kwenye kiwanja cha wazazi wangu, nashukuru Mungu maisha yakaanza kuwa mazuri, nikawa naweza kulea watoto wangu wawili pamoja na wandugu yangu wawili umla nilikuwa na watoto 4.
Katika kuishi huko nikaweza kuongeza nyumba ya pili ambayo nimepangisha napata pesa za kusomeshea watoto. Lakini linalonitatiza ni Mama yangu Mazazi simuelewi kabisa, kwamba anataka mm nitafute sehemu nihame pale kwa sababu anahitaji hizo nyumba kupangisha , anasema nimeshakaa sana inatosha, sasa nikamuuliza kuwa mm si ndiyo nimejibana nikajenga, ananiambia nitoe tofari zangu.
Imefikia steg ya kubagua hata wanangu, kwa kweli inaniuma sana, kwa sababu yeye ni mama yangu, anatakiwa aniunge mkono aslimia 100, lakini yeye ndiyo anakuwa kikwazo kwangu , sifahamu ni kwa nn, na kama nimemkosea kwa nn asiniambie?, najiuliza nimemchukiza nn, sipati jibu.Kama matumizi nampa, au anaona hazitoshi?
Sipendi kuandika hapa , ila imenibidi, naona sina faida ya kuendelea kuishi, maana mume kanishinda
na ninayemtegemea kunisupport kanigeuka, naona bora nife mm na wanangu nimuachie hizo nyumba.
naombeni ushauri nifanyeje?
Inawezekana kuna laana juu yako au kwa Mama yako. Utafute kanisa wanalotoa huduma za maombezi ukaombewe.
Wewe ni nani mbele ya MUNGU kwani hujui siku hizi hayo makanisa yenu yanawachukulia sh 500 za walalahoi kwa kutumia jina la Yesu?
kuna wachungaji ni zaidi ya mafisadi kwa vitendo vyao hao ndo ninaowazungumzia.
Sijamanisha nimejenerize ila nawafocus hao wakiana kakobe types na utapeli wao kwa kutumia jina la Yesu.So kamanda tuliza munkali hatupo kwenye vita hapa.