Nokia 3310 kurejea tena.

Nokia 3310 kurejea tena.

Kukaa na Chaji muda mrefu hii ni kwasababu ilikuwa ni ya kutumia kwa kupiga/kupokea na kutuma sms.

Baada ya hapo hakuna chochote ulichoweza kuchezea na kikamaliza chaji.

Hata radio ilikua haina.

Tuliita Jeneza.
Ina redio. Na inacheza game piaa. Ina games nzuri sana za miaka ilee
 
IMG-20170129-WA0010.jpg

hii ndio copy copy iliyouza kuliko aina zote za sm ambazo zishawahi kutolewa na Nokia, ndio ukweli halisi..
 
Hii simu imebeba historia kubwa sana kwangu.. Ilikua miaka ya 2006 kama sijasahau natoka mkoa kuja dar. atakae nipokea ubungo simjui, basi nimechaji simu usiku kucha nisije nikakosa mawasiliano safarini.. Asubuhi nimeamka freshi nimepanda gari yani sijatoka hata kilometa 6 simu ikapiga bips za battery low ikazima. Haha duh.. kufungua battery limevimba hilo balaa na simu ikazima mazima, kilichotokea ubungo mungu anajua.
 
Mimi mpaka leo nilikuwa naitafuta hii simu ,naona ni bora wangeirudisha sokoni kama ilivyokuwa mwanzo bila kuongeza features zozote
 
Hiyo simu nilinunua mwaka 1999. Nilidumu nayo kwa miaka 7. Walipoitungia Nina JENEZA nikaiweka ndani,ninayo.
1999 hii simu ilikuwa imeshatoka ? Nakumbuka Nokia Ringo au Siemens c25 na baadae c35 ndio zilitoka miaka ya 2000 mwanzoni
 
Thanks

Lakini nilisikia kuwa kiwanda chao kiliuzwa kwa Microsoft kama sijakosea sana

Kwanini soko liwe katika nchi hizo tu kwa kuanzia "According to reports, the phone will initially be available only to European and North American consumers and will cost €59, significantly less than its original price in 2000 of £129"
kiwanda cha smartphone pekee ndio kiliuzwa
 
View attachment 470752 Hii ni miongoni mwa simu iliyouzwa kwa wingi duniani kuliko simu nyinginezo.
Simu ya Nokia 3310 iliingia sokoni miaka 17 iliyopita na ikaachwa kutengenezwa tena. Inakadiriwa kuwa simu 126 million ziliuzwa mpaka simu hizo zilipokoma kutengenezwa.
Sifa kuu za simu hizi ilikuwa ni uimara, kukaa na chaji muda mrefu na nyinginezo.
Simu hii inarudi tena sokoni ikiwa imeongezewa vionjo vya soko la kisasa na unafuu wa bei.
Je, unaweza kuitumia tena simu hii au ni vyema kuisahau kabisa?
Inakukumbusha nini?
Naikubali sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom