Simu ya Nokia 3310 iliingia sokoni miaka 17 iliyopita na ikaachwa kutengenezwa tena. Inakadiriwa kuwa simu 126 million ziliuzwa mpaka simu hizo zilipokoma kutengenezwa.
Sifa kuu za simu hizi ilikuwa ni uimara, kukaa na chaji muda mrefu na nyinginezo.
Simu hii inarudi tena sokoni ikiwa imeongezewa vionjo vya soko la kisasa na unafuu wa bei.
Je, unaweza kuitumia tena simu hii au ni vyema kuisahau kabisa?
Inakukumbusha nini?