Nocking him hard: Taarifa ya Cyprian Musiba dhidi ya Tundu Lissu

Sesimba

Senior Member
Dec 20, 2016
189
382
_______________________________________
Taarifa ziwafikie pia vijana wote wa Lumumba.

Hakuna umasikini mbaya kama umasikini wa akili.

Kuna mtu mmoja ameamua kujilipua ili watanzania waendelee kujua kuwa uwezo wa vijana wengi wa CCM na wana CCM wengi ni mdogo sana ama wanajitoa ufahamu kabisa ili kujipendekeza.

Kwamba Cyprian Musiba ametangaza kumfungulia mashitaka Tundu Lissu huko ICC nchini Uholanzi.

Kwamba huyu Cyprian Musiba ana jopo la wanasheria watakaopeleka na kusimamia mashitaka yake ICC.

Ndugu zangu mahakama ya ICC haishughuliki na aina ya kesi za ajabu ajabu kama hii ya Musiba inayoongozwa na wanasheria uchwara na wasiojua hata majukumu ya ICC.

Kesi zinazoshughulikiwa na ICC ni za aina tatu tu kama ifuatavyo.

1.Kesi za mauaji ya Kimbari(Genocide).

Haya huwa ni mauaji yanayolenga kuangamiza kabisa ki(kundi) cha(la) watu fulani katika nchi.

Inaweza kuwa kabila fulani, inaweza kuwa wanachama wa chama fulani ama wa imani fulani nk. Mfano ni mauaji ya Kimbari Rwanda.

Hawa wanasheria uchwara wa Cyprian Musiba watuambie ni lini na wapi Tanzania yamefanyika mauaji ya Kimbari?

Watuambie pia ni lini na ni wapi Tundu Lissu alifanya mauaji ya Kimbari hapa Tanzania?

2.Kesi za uhalifu wa kibinadamu(crimes against humanity).

Haya ni makosa ya kushambulia mtu/watu, kunyanyasa watu kwa manyanyaso mbalimbali ikiwemo ubakaji, utesaji nk.

Makosa ya uhalifu wa kibinadamu ili yakidhi kigezo cha kuitwa makosa ya uhalifu wa kibinadamu ni sharti yawe yametekelezwa na serikali ama utawala ama mfumo wa utawala.

Tundu Lissu siyo serikali wala siyo mtawala maana makosa haya yanapaswa kuwa yametekelezwa na serikali.

Sasa waulizeni hawa wanasheria uchwara wa Cyprian Musiba kama Lissu ni serikali iliyofanya makosa ya uhalifu wa kibinadamu.

Muwaulize na vijana wa Lumumba waliosambaza hilo andiko uchwara kama wanajua ICC ni kitu gani.

3.Kesi za makosa ya kivita( war crimes).

Hii ni aina ya tatu na ya mwisho inayoweza kupelekwa ICC.

Haya ni makosa yanayoweza kutekelezwa wakati wa vita ama vurugu kwa pande zinazo-zozana.

Makosa ya ubakaji, mauji, utekekaji, utesaji yakifanyika katika wakati wa vita ama mzozo basi yanakidhi vigezo vya kupelekwa ICC.

Lakini pia ili kesi yoyote ipelekwe ICC ni mpaka serikali ya nchi husika ama isiwe na uwezo kusikiliza mashauri hayo, ama haina nia ya kuyasikiliza mashauri hayo nk.

Nchi hii inawanasheria wa ajabu kama hawa wanaoandaa mashitaka ya Lissu kuyapeleka Uholanzi na vijana wa Lumumba wanashangilia kwa kuwa hakuna wanalojua kuhusu ICC.

Hapa mashitaka ya musiba yakifika ICC hayatapata hata heshima tu ya kujadiliwa na jopo la mahakama hii.

This is a total trash and will be immediately dumped into the trashcan .

Mashitaka haya yatatupiliwa mbali Mara tu baada ya kufika ICC.

Huwezi kupeleka ugoro huu wa Cyprian Musiba na jopo lake la wanasheria uchwara eti ukajadiliwe ICC. Kama Musiba anatafuta kick basi ni aibu yake.

Na: Mshinga JN

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Nitamwambia waziri mkuu wa Canada ashughulike swala la mapanga shaaa unasema mbele za watu

Aisee ile sio shithole country

You are missing something here hahahahaa
 
Nilipoona tu thread title kwamba eti kuna mtu anataka kumfungulia Tundu Lissu kesi ICC, wala sikujisumbua hata kupoteza bundle ya kufungua hiyo thread manake niliona ni ujinga ule ule wa akina Jerry Muro na sasa kaamua nae kudhihirisha ujinga wake.

Trust me, sikumbuki kuwahi kusoma threads zinazohusu Jerry Murro na kama nimewahi then sio zaidi ya moja kuangalia ni nini hasa huwa anaongea.
 
Vyama vya siasa viache kuendeshwa kijanja janja, ajirini jamani siyo mtu akishinda tu kibarazani anajua kuongea uongo bila aibu basi unampa kadi.

Matokeo ndiyo ya Musiba na Sepetu
 
Huyo Msiba ni Kilaza sijawahi ona. Anaongea vitu rundo visivyo na mpangilio wala mantiki. Ovyo sana.
 
Nakumbuka tu ile kesi ambayo Ukawa waliwadanganya wafuasi wao kuwa wataipeleka ICC.
 
UNATEGEMEA NN KWA MTU ALIYEGUSHI CHETI?KWELI UVCCM NIKIOTA CHA WAJINGA.hyo namba ndyo itawabana wao wenyewe
 
Huyu musiba ni mjita lakini napata mashaka na uelewa mfinyu alionao wajita hawako hivyo!
 
Sesimba
Boss Sesimba. Kuna vitu watu hawavifahamu?
Swali lahisi la kuuliza nikuwa, ni wakati gani defamation accusation inapokuwa defamation?

Ukweli sio uzushi, ukweli ni ukweli daima.
Nafikiri Musiba, ni genius gau ambaye sio rahisi kila mtu kumfahamu.
Anataku kupiga ile ya mfalme j.u.h.a.

Wenye akili wanamsubiri. Na hapo ndipo atakapojua kuwa ukweli siku zote huwa ukweli.


Sent from Itel g5 ya Tochi using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom