NOAH yaua abiria wote!

NOAH yaua abiria wote!

Aiseee n hatari..ht kusini ni hivyo hivyo...nilsema sitorudi tena kule...ndani ya noah mpk kwa buti abiria...mizigo...kibaoo...na zinakimbia balaa
Kinachokera dreva anaweka buku 2 za trafiki na hakuna issue ya level sit. Yaani mkijaa hadi kwenye tank la mafuta trafiki akishapewa buku 2 yake wakat mwingine jero atawaacha mkafie mbali na dreva wenu! We maiti zinatolewa then watu wanashangaa, hivi wote walikuwa in this Noah only?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Daah! too sad, ilikuwa inatokea dumila au morogoro, maana nshawahi kupanda hizo noah,zinakuwa kiatu sana! RIP marehemu wote.
Mkuu hiyo kitu Dom to Moro! Mi pia nimewahi kutumia usafiri huu. Sumu sasa ukemee hii tabia ya kujaza watu kama gunia la mkaa, abiria watatamani kukutafuna!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
poleni sana wahanga wote wa ajali hiyo mbaya
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu pahala pema peponi AMINA

NOAH NI JANGA LA KITAIFA HAIFAI KUFANYA BIASHARA YA KUPAKIA ABIRIA
 
Mkuu ilikuwa inatokea Dodoma to Morogoro jamaa akaivaa gari ya mizigo. Hizi Noah majanga bandugu, hakuna level sit. Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Yaani imetoka Dodoma? Aiyaaa...Pole natoa. Lakini ngoja kwanza mkuu hivi ingekuwa level seat pengine wangenusurika au chanzo ni uzembe wa dereva wa Noah???????????
 
Mungu awape raha ya milele,na faraja kwa wafiwa wote...
Lakini pamoja na kwamba zinajaza sana of which si sahih pia madereva wengi hawako makini barabarani na ajali nying zinatokana na overtake pamoja na mwendo mkali.
 
RIP marehemu wote. Mungu azijalie faraja familia zote zilizokumbwa na msiba
 
Ndiyo matokeo ya kuruhusu mambo kisiasa! Wataalamu walishasema haya si magari mahsusi kusafirisha abiria, lakini "Serikali Sikivu" ikawaona wapuuzi! Ikaenda bungeni na kubariki hatari hii. Wananchi nasi tunashangilia tukipangwa kama maboga. Ajali ikishatokea ndipo utasikia vilio na kusaga meno, lakini wakati haijapinduka ukithubutu kumtaka dereva apunguze kasi, utashambuliwa mithili ya mwizi. Vifo vya aina hii si mapenzi ya Mungu, bali ni mapenzi ya wanasiasa wetu waliowapiku wataalamu!
 
Mkuu ilikuwa inatokea Dodoma to Morogoro jamaa akaivaa gari ya mizigo. Hizi Noah majanga bandugu, hakuna level sit.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Mkuu ndo nimepita mda huu naelekea Mwanza,dah yani haifai hata kuwa chuma chakavu imekuwa nyang'anyang'a! Hamu ya safari imekufaa kabisa yani, nashindwa kudrive. Dah mbaya sana ngoja nipumzike kidogo nitafune mahindi ya uchemsha kwanza.
 
Yaani imetoka Dodoma? Aiyaaa...Pole natoa. Lakini ngoja kwanza mkuu hivi ingekuwa level seat pengine wangenusurika au chanzo ni uzembe wa dereva wa Noah???????????
Mkuu naongelea namna Noah zinavyojaza. Ajali huwa mbaya zaidi inapoua watu wengi. Mungu atusaidie!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mbona mabasi ya dom-moro-dar yapo kibao? Wanashawishika nn kupanda Noah? Tena kwa taaaaabu hivyo?

Mabasi yapo, lakini wasafiri nao wapo wengi na most of people wanapenda cheap nauli.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ndiyo matokeo ya kuruhusu mambo kisiasa! Wataalamu walishasema haya si magari mahsusi kusafirisha abiria, lakini "Serikali Sikivu" ikawaona wapuuzi! Ikaenda bungeni na kubariki hatari hii. Wananchi nasi tunashangilia tukipangwa kama maboga. Ajali ikishatokea ndipo utasikia vilio na kusaga meno, lakini wakati haijapinduka ukithubutu kumtaka dereva apunguze kasi, utashambuliwa mithili ya mwizi. Vifo vya aina hii si mapenzi ya Mungu, bali ni mapenzi ya wanasiasa wetu waliowapiku wataalamu!
Mkuu magari mengi ni ya wakubwa hao hao ndo maana wanayatetea! Si unaona hata wabunge wanajenga nyumba zao na kukodishia halmashauri kama ofisi?lazima watetee!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom