Mantissa
JF-Expert Member
- Jul 24, 2010
- 876
- 166
Kwa mara ya kwanza niliuangalia Mdahalo wa Mh Slaa kupitia Michuzi blog. Alipoulizwa maswali na mwendesha kipindi, hakika nawaeleza hakuna point aliyojibu. Kitu alichhofanya ni kama alivyofanya bungeni- alikuwa critical na wala hakutoa utatuzi wa tatizo.
Nitatoa mfano wa maswali haya mawili:
1. Mh Slaa, K AMPENI ZA MWAKA HUU ZIMELAUMIWA KUINGILIWA NA UDINI, NA CHADEMA KIMEKUWA KIKINYOSHEWA KIDOLE, NA PENGINE TUHUMA HIZO ZINAKULENGA WEWE Mh, wasemaje juu ya swala hilo?
Jibu: Nani asiyejua kuwa mimi ni mkatoliki au nani asiyejua kuiwa mimi nilikuwa Padre.......
Basi alibwabwaja hapo bila hata kujibu swali la msingi. Hatujakataa kuwa watanzania hawana dini zao wala hatujakataa kuwa watanzania na viongozi hawahudhurii misikitini na makanisani. Sasa ni nini anachotuambia hapo. Baada ya hapo akaja kwenye profesional yake ya kutoa critics kwa wengine. Huyu ni rais kweli au kichwa maji.
2. Elimu bure, utawezaje hilo.
Jibu: Mh Kikwete ameorder mabango ya picha yake ya kampeni toka Kanada. Na yamesafirishwa kwa ndege. Na yamesambazwa nchi nzima. Hata kule mtwara kuna nyumba inataka kuanguka lakini nje imebandikwa picha ya Kikwete. Gharama ya shughuli yote imeghalimu dola 1 mil.
Sasa hizo zingetumika kusomeshea wanafunzi zingetosha.
Kweli huyu mtu ni kichwa maji, wewe unaamini kweli kuwa dola 1 mil zinatosha kusomeshea wanafunzi tanzania nzima?
Majibu ya swali hilo yanahitajika yawe katika mtiririko ufuatao:
Idadi ya wanafunzi mwaka huu ni...........
Kila mwanafunzi anagharimu sh..........
Jumla ni sh..........
Pesa hiyo tutaitoa hapa sh.......pale sh.......na.....na...
Hivyo ndivyo wizara yake kivuli ya uchumi ilibidi ifanye mahesabu kabla ya kupayuka kwenye majukwaa elimu bure.
Huyu kwenye uchumi ni Mbumbumbu kabisaaaa
NO WAY, NO HOW, NO SLAA.
Wewe umejiandaa kutoelewa make hata wanafunzi darasani wako wa type yako, hivo mi sikushangai. Sasa JK anajua huo uchumi? Mpaka sasa hivi unajua katoa ahadi hewa ngapi? Kwa vile ubongo wako umeuandaa kutoelewa, itakuwa hivyo.
Subiri kesho JK atakachoongea ndo ulinganishe na alichokisema Dr Slaa. Jk tunamjua ni mbumbumbu mzungu wa leli, hata degree yake alipata gentle, mvivu kusoma huyo.
Kesho utapata majibu, ila watu kama wewe huwa wanashabikia upuuzi.