NO way, No how, No Slaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NO way, No how, No Slaa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zawadi Ngoda, Oct 28, 2010.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kwa mara ya kwanza niliuangalia Mdahalo wa Mh Slaa kupitia Michuzi blog. Alipoulizwa maswali na mwendesha kipindi, hakika nawaeleza hakuna point aliyojibu. Kitu alichhofanya ni kama alivyofanya bungeni- alikuwa critical na wala hakutoa utatuzi wa tatizo.

  Nitatoa mfano wa maswali haya mawili:

  1. Mh Slaa, K AMPENI ZA MWAKA HUU ZIMELAUMIWA KUINGILIWA NA UDINI, NA CHADEMA KIMEKUWA KIKINYOSHEWA KIDOLE, NA PENGINE TUHUMA HIZO ZINAKULENGA WEWE Mh, wasemaje juu ya swala hilo?

  Jibu: Nani asiyejua kuwa mimi ni mkatoliki au nani asiyejua kuiwa mimi nilikuwa Padre.......

  Basi alibwabwaja hapo bila hata kujibu swali la msingi. Hatujakataa kuwa watanzania hawana dini zao wala hatujakataa kuwa watanzania na viongozi hawahudhurii misikitini na makanisani. Sasa ni nini anachotuambia hapo. Baada ya hapo akaja kwenye profesional yake ya kutoa critics kwa wengine. Huyu ni rais kweli au kichwa maji.

  2. Elimu bure, utawezaje hilo.

  Jibu: Mh Kikwete ameorder mabango ya picha yake ya kampeni toka Kanada. Na yamesafirishwa kwa ndege. Na yamesambazwa nchi nzima. Hata kule mtwara kuna nyumba inataka kuanguka lakini nje imebandikwa picha ya Kikwete. Gharama ya shughuli yote imeghalimu dola 1 mil.

  Sasa hizo zingetumika kusomeshea wanafunzi zingetosha.

  Kweli huyu mtu ni kichwa maji, wewe unaamini kweli kuwa dola 1 mil zinatosha kusomeshea wanafunzi tanzania nzima?

  Majibu ya swali hilo yanahitajika yawe katika mtiririko ufuatao:

  Idadi ya wanafunzi mwaka huu ni...........

  Kila mwanafunzi anagharimu sh..........

  Jumla ni sh..........

  Pesa hiyo tutaitoa hapa sh.......pale sh.......na.....na...

  Hivyo ndivyo wizara yake kivuli ya uchumi ilibidi ifanye mahesabu kabla ya kupayuka kwenye majukwaa elimu bure.

  Huyu kwenye uchumi ni Mbumbumbu kabisaaaa

  NO WAY, NO HOW, NO SLAA.
   
 2. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hata mtandao wa NEC ambao ni nec.go.tz kama unavyoonekana hapo chini una leta wasiwasi kama kweli NEC ni chombo kitakachotuhakikishia uchaguzi huru na wa haki. Hivyo ndivyo mtandao wao unavyo-share IP na mmoja wa wagombea uraisi! Kwa namna hii maswali ni mengi sana... kwanini? Na kama ni IP ni ya serikali kwa nini campaign team ya mgombea itumea IP hiyo? je huku si kukiuka sheria za uchaguzi? Wasiwasi wangu ni hapo ndipo kura zinaweza kuchakachuliwa! Lazima tuchunge kura zetu katika kila stage
  [​IMG]
   
 3. v

  vickitah Senior Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 18, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  \


  Zawadi nahisi huna jipya huyu mtu unayemuona mbumbu anajua kitu anachokisema na ana watu wazuri tu wa kumshauri, ni kwamba we umejiaandaa kuto kumuelewa. mi naamin hata darasani sio kila mtu anaelewa somo, na mara nyingi wasioelewa wanasema mwalimu mbovu.

  na hili swala la elimu bure kwani Slaa kasema mara ngapi linawezekana kwa kupunguza matumizi ya serikali ( mashangingi, posho za chai na vitu km hivyo) nahisi umedandia treni kwa mbele ndo mana hujamuelewa ule mfano aliotoa ni moja tu ya mifano ya hela ambazo zinatumika vibaya badala ya kwenda kumsaidia mtanzania. kama rais umefanya mambo mazuri kwa nin utumie hela yote hiyo kwenye kampeni wakati wananchi wako ni maskin wa kutupa.

  Ufafanuzi kuhusu elimu bure unaotaka tayari ushanyambulishwa humu ndani zawadi kwa faida yako tu gonga link hii https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/78602-kwa-nini-elimu-bure-inawezekana.html

  Pigia kura Chadema, Elimu bure inawezekana.. Chadema kwa maendeleo ya Tanzania!! Chagua Dr. Slaa (PhD)
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Zawadi, hii makala yako naona umechelewa saana kuileta.

  Au ndiyo Maji ya Shingo?

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. S

  Singo JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  doubt is part and parcel of the power of darkness, while optimism that one feels belong to the kingdom of light and life . learn to be the master of your destiny, think positive. SLAA ANAWEZA , NITAMPIGIA KURA, SIDANGANYIKI
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tatizo la Zawadi Ngoda ni kwamba anaandika asichokijua.
  Ni mtu ambaye badala ya kujibu au kuibua hoja analeta vioja
   
 7. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 3,173
  Trophy Points: 280
  Ushauri wa bure kwako Zawadi "Try to keep your words soft and tender because tomorrow you may have to eat them." Huyu unayemwona wewe ni mbumbuu sisi kwetu anatufaa.
   
 8. M

  MULANGIRA Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makame ni mnufaika wa mabadiliko ya Katiba

  Hadi Februari 2005 sifa za Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilitajwa na Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa zifuatazo:

  Tume ya Uchaguzi
  74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-
  (a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
  (b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;

  (c)wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

  Lakini ili kumlinda Jaji Makame aendelee kushika nafasi hiyo sifa hizo zilibadilishwa katika Mabadiliko ya Kumi na Nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanywa tarehe 7 Februari 2005 na kukubaliwa na Raisi Mkapa mnamo tarehe 6 Aprili 2005.

  Ibara ya 74 (1)(a) na (b) hivi sasa inasomeka:

  74 (1) (a) Mwenyekiti ambaye atakuwa ni Jaji wa Mahakama au Mahakama ya Rufani au ni mtu mwenye sifa ya kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na mitano (Nimeongeza msisitizo)

  (b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa ni Jaji wa Mahakama au Mahakama ya Rufani au ni mtu mwenye sifa ya kuwa wakili na amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungau miaka kumi na mitano (Nimeongeza msisitizo)

  Kwa minajili hiyo ni wazi kuwa Jaji Lewis Makame amenufaika na mabadiliko hayo na kwa hiyo ndiyo maana anaendelea kuibeba CCM katika utendaji wake. Ni lazima kuyasema hayo na kumtaka yeye na Tume kuthibitisha uadilifu na kuaminika kwao.
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hata wewe ni mbumbumbu wa uchumi heshma ya Jamii forums ndo inatufanya tukuvumilie.
  Wachumi asilia wanajua kwamba Bandu bandu humaliza gogo, pia wanajua kwamba Haba na Haba hujaza kibaba.

  Kuna Dola Milioni moja ilotolewa penny 1 ikabakia dola milioni moja??
  Au kwa mfano wa fedha za Madafu.

  Kuna Shillingi milioni moja ambazo hubakia milioni moja ikitolewa shilingi moja tu???!!?
   
 10. Nkoboiboi

  Nkoboiboi JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli Zawadi we ni zawadi kwa Kikwete!!

  Hivi huko kijijini kwenu (hata Dar kuna vijiji) hujaona nyumba za tembe 49 yrs after the said uhuru!! We need total UHURU hasa wa fikra
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Zawadi Ngoda, unaweza kuwa unasema kitu toka moyoni mwakko, lakini the thing is JK hatumtaki maana ana ahadi zisizotimilika, na ni msanii no1!...hiyo tu inatufanya tusibadilike hata ukinena kwa lugha za MALAIKA!...POLE!
   
 12. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Zawadi unaongea pumba tupu.

  CCM wote ndiyo MAMBUMBUMBU wa uchumi. Ndiyo maana Kikwete alipoulizwa kwanini Tanzania ina RASLIMALI NYINGI LAKINI wananchi wake maskini akajibu kuwa HAJUI!

  Ndiyo maana hata majizi ya FEDHA ZA EPA ameshindwa kuyabana kwaababu hajui maana ya ufisadi wala umaskini.
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu mie ndo MSANII hapa. sema kikwete ni NDUMILAKUWILI namba moja.
  Huyu ngoda anachoongea hakitoko moyoni mwake bali msukumo toka nje maana yeye ni mwaongo kama bwana ake alivyo mwongo
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  zawadi pole sana nakumbuka ile Methali isemayo aliyelala usimwamshe
  Umejiandikisha kupiga kura?
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  DataVision CEO :: Mwaijonga, G MacLeans :: UDSM Undergraduate Admission 2009/2010 ::
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu... sisi tu wapita njia na tusemayo yanapita na muda pia... in January tutakua tunasoma post zetu zenyewe na kutoamini tuliyosema

  Tumuombee Zawadi atambue kwamba ni bora utukaniwe mama yako kuliko kusingiziwa udini

  Ruvuma wanamuelewa sana zawadi
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tunamhitaji Zawadi, shemeji yetu, amefuzu vigezo vyote vya kuwa mpinzani wa serikali ya dr Slaa baada ya Uchaguzi. Ajifunze sasa kuwa critical kwani kuwa mpinzani ni kuwa critical
   
 18. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Dah!....
  it's very very LATE mhishimiwa ''zawadi ngoda''

  WHY DON'T YOU :tape::tape::tape::tape:?

  ......:rip: zawadi ngoda
   
 19. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  Kura zinahesabiwa kwenye vituo, website ya nini tena?
   
 20. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wewe Zawadi kama utakuwa umejiandikisha kuwa mpiga kura nakushauri kwa heshima na taadhima tarehe 31.10.2010 nenda kapigi kura yako ya urais kwa Doctor wa kweli wa kusomea Dr Slaa.Tafadhali badilika na ipende nchi yako Tanzania na wakati muafaka ni huu
   
Loading...