Hospitali ya KCMC yakumbwa na tuhuma nzito za ufisadi wa mabilioni ya fedha

FACTUAL

New Member
Feb 26, 2017
4
5
Hosipitali ya Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC), imekumbwa na tuhuma nzito za ufisadi wa mabilioni ya fedha, yanayo ongozwa na Mkurugenzi mtendaji Dr. Gileard Massenga na Mkurugenzi wa Fedha Mrs Mungure. Kupitia urafiki wa karibu na Askofu mkuu wa KKKT Dr Alex Malasusa aliyepita na Askofu Shoo wa sasa, wamekuwa wakitumia mbinu haramu kutafuna fedha za Watanzania kwa ajili ya kujilimbikizia. Kwa namna yakufanya ukarabati wa majengo, kutoajiri wafanyakazi wao an kutumia wanafunzi wa chuo kutibu bila kuwalipa na ununuzi wa Magari ya kifahari na ujenzi wa Hosteli mpya Flats 20 Chini ya Pesa za Hospitali .

Ikumbukwe huyu bwana alipoingia madarakani haraka haraka alianzisha ujenzi ikiwa ndo sehemu nzuri ya kupiga hela ambapo amejenga Restaurants na maduka na saloon ndani ya hospitali. Wakati huohuo wagonjwa wakikosa hata sehemu ya Kulala na wegine kulala chini koridoni na wamama wanaojifungua hulazwa chini au kulala wawiliwawili kitandani. Hii ni Aibu.

Chanzo cha kuaminika cha habari kimedai kuwa ufisadi huo unasimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji bwana Dr Gileard Massenga kwa kukingiwa kifua na swahiba wa karibu Askofuu Mkuu wa KKKT Askofu Shoo, kuwa anatumia madaraka yake ya ukurugenzi kupitia bahasha ya aliyompatia Askofu pindi alipoingia madarakani yenye thamani ya milioni 10 kuwa utamaduni wa shirika kila mara.

Nikizungumza na chanzo cheat cha ndani, kimesema kuwa kwa msukumo wa Dr Gileard Massenga, Hosipitali ya KCMC mali ya GSF, imeendelea kufujwa fedha. Chanzo kimesema kuwa kwa mujibu wa nyaraka ambazo kimezinasa,

  1. Deni la Hospitali lina zidi kukua kutoka Sh Milioni 5 mwaka 2010 hadi Biloni 2.9 Mwaka 2013 na Bil 5.2 mwaka 2016.
  2. Hela zilizokuwa za CT Scan kwenye akaunti ya Fix kiasi cha 1.7 Bilioni hazijulikani zilipo. (CT scan ni mwaka wa kwanza imefungwa na imekuwa ikiharibika mara kwa mara japokuwa inadaiwa ni mpya na imenunuliwa na Kanisa ELCT kwa BIL.2.4.
  3. Hela zilizopatikana kwa kuchangia Fundraising 2010 - 2011 kiasi cha Milioni 700 na 2014-2017, 1.4Bilioni hazijulikani zilipo na hakuna maelezo na mara kwa mara wamekuwa wakihonga na kukataa auditors kutoka nje. Tunaomba mkaguzi wa Serikali aje alione hili.
Pia mtoa Vibali – chini ya Wizara ya Afya na Katibu Mkuu akague Hospital ndogo na Clinics mjini Moshi na rejea Kanuni za maadili kwa utumishi wa umma isiyoruhusu umiliki aina ya huduma itolewayo na nafasi aliyepio na kwa muda wa kazi. Hili ni kubwa sana na pia swala la Mke wake Kutumia Jina la Dr. kufanya kazi nje ilihali si Daktari. Nytaraka zipo.

"Ndugu, mchezo anaofanya Dr. Gileard Masenga, hasa kupitia majungu ya watafuta umaarufu, ni ule kutumia vikao na kujaza manesi na ambao baadhi ana uhusiano nao. Amekuwa akiwaburuta vikaoni bila kupata criticism ya wakuu idara na kutafuta fedha haramu kwa kuwaibia Watanzania kupitia Clinic zake za nje. Moja ikiwepo hapo Mjini Moshi opposite na Benki ya Stanbinc Hope-Clinic ambayo wamejiweka hapo na Wakuu wa idara nyingine waliopo KCMC na mkurugenzi wa Huduma Dr.Sara Urasa ambao walitakiwa kutoa huduma hizo hapo Hospitali huku huduma za hospital zikizorota. Huku baadhi ya vipimo muhimu kama FB azifanyiki cha ajabu huduma hizo zipo kwenye hizo clinic zao na kuwatuma wagonjwa waende huko. Hi ni Aibu na fedheha kwa Daktari ajiitaye mwalimu.

Ikumbukwe ndani ya Miaka Kumi KCMC ilifukuza madaktari Bingwa Juu ya Utovu wa Maadili kama huu, wakiwemo maprofeso nyezo waliokuwa na tija kwa Hispitali na sambamba na Chuo cha TIBA KCMU-college.

Ikumbukwe mwaka 2008/2009 Mfuko wa Jamii walioomba kuwajengea hosteli hizo bila ya Kutumia Senti za shirika. Huo mradi ulizimwa kwa nguvu zote kupitia Mkurugenzi na Askofu Martin na Mkurugenzi wa Hospitali.

Ikumbukwe KCMC ilikuwa na Uwezo na Vifaa nyenzo kutoka Marekani vya upasuaji wa moyo na Daktari bingwa aliyebobea Prof. Chugulu ambaye alifukuzwa na Mkurugenzi kushirikiana na mkuu wa Idara upasuaji kwa figisu za kuzidiwa usanifu na ujuzi na Daktari huyo kuhamia Soweto Designated Hospital na kuliongeza Taifa Gharama ya Kutuma watoto kufanyia upasuaji…

Si hapo tu, lakini pia Dr. Massenga ni mtu wa chuki na visasi kwani ameweza kumfukuza pia Daktari bingwa wa akina mama Prof. Olola Oneko na kumkataza asiwepo hospitali hata kwa kujitolea baadsa ya bingwa huyo kumzidi ufanisi katika kupambanana. Tafiti na tiba kwa cancer ya Kizazi kwa akina mama huduma iliyotukuka na hutolewa bure.

Tukiendelea hapo kwa idara ya Cancer chini ya Taasisi mpya inatumiwa nguvu kubwa kwa kila mtuishi kukatwa sehemu ya mshahara wao kusaidia ikumbuke Serikali inachangia Bil.2 kila mwaka na wagonjwa wanatakiwa kulipishwa mpaka Milioni -7 kwa huduma hiyo ya Dawa za kupabana na Cancer na hivyo kuwafanya wagonjwa wengi kukimbilia Ocean Road.

"Sasa ni kipindi cha miezi 5 sasa operation zinazofanyika hutozwa gharama kubwa mpaka hasa pale zinapohusisha mfuko wa watanzaia wa Bima NHIF na ulaji huo huwa una mgawo pande zote. Kitu ambacho si halali na uhalisia na ukichunguza operesheni nyingi hufanywa na wanafunzi ambao hawalipwi kwa kufanya na kutishiwa hasa sisi manesi.

Mbaya zaidi muda mwigi madaktari hao huwa kwenye clinic zao Arusha na Moshi. Hali hii ni kuibia Serikali ilipayo takribani 800M kwa mwa mwezi Mishahara kwa watumishi na huduma hawatoi. Wahusika wakubwa katika haya ni Dr. Massenga Mwenyewe, Dr. Kondo – Upasuaji, Dr. Mavura - Ngozi, Dr. Mandari - Ortho na Dr. Mbagga Mkurugenzi - KCRI

Haina mvuto kama ilivyokuaga ada yake ambayo hata mgonjwa unaweza kupelekwa na kutokana na uzuri wa mazingira na hata majengo hakika unapona. Nyakati hii ya uongozi Dr Gileard Massenga yani choka mbaya kabisa! Kiasi ambacho hata Wazungu wamekuwa wakikimbia hospitali hiyo wakichajiwa pesa nyingi Mfano $150 sawa na 320,000 kufungua File kwa kumwona daktari kitu kinachoiharibia sifa nchi kwa kuonekana ni gharama kubwa kwa huduma mbovu na vipimo vibofu. Mimi kama nesi naumia sana nikimwoa mgonjwa anaondoka sababu gharama. Ni nje ya maadili na miiko, ila huyu baba Massenga hana huruma

Mwaka huu Mkuu wa mkoa aliyetimuliwa na Mh. Raisi Meck Sadick aliiombea hospitai hiyo kwani inashangaza, haina madaktari walioajiriwa na kwa mwaka wa 2 zaidi ya madktari 20 - 30 wamekuwa wakijitolea na hospitali ikishindwa kuwalipa hata hela ya nauli. Napenda kumpongeza Rais na namshauri afanye uchunguzi wa kimapato kwa hospitali ni ya wezi na wanaibia watanzania na Serikali yao. Ikumbukwe mwaka jana kuingia mwaka huu taarifa ya ndani ilisema hospitali yajiendesha kihasara na faida kiduchu ya Mil.4 kwa Mwezi ukilingaisha na BIl. 2 - 4 za Muhimbili. Hospital hii ni picha tosha ya upigaji kwa wafanyakazi hulipwa na Serikali zaidi ya Mil.800/mwezi na vitanda na vifaa vigi ni misaada ya bure toka nje wao wakinunua labda ni mafyekeo na mafagio ya ndani kazi amabazo nyingi hufanywa na wafungwa_magereza.

Inaelezwa pia amekuwa akikumbatia fursa na kuwanyima wa chiusi yake hasa pale anapofanya mafunzo Ulaya kupitia mfuko wa wanafunzi ambao BSU Grants kuwaacha wanafunzi wanateseka na kukosa fursa lengwa. Natamani kulia kama muuguzi kwa fani yetu ina huruma sana na mambo yanavyoendelea hapa.

Viwanda vidogo na Idara tanzuka kama za usafi, ushionaji na ufuaji bila kusahau estate zimekodishiwa kampuni binafsi na mpaka canteen nyingine wamegawaa wao na Maaskofu akina Shoo na tender nyingi zikitangazwa ni geresha tu, usiooteze hela yako ya Bid.

Kili wonders hoteli pia hapa Moshi wana muona huyu bwana huwa hapa na visichana na kutumbua alizofuja akiwa nchini. PCCB tusaidieni

Tuamuomba Rais Magufuli atupie jicho KCMC atubadilishie hawa watu na tupate chachu ya maendeleo na huduma iboresheze.

Swali la msingi kwa nini Muhumbili wanaweza? Ni aibu na fedheha kwa Taifa.
 
Hii kitu inaonekana umeandika kwa hasira sana mkuu, pengine na mikono ilikuwa inatetemeka
 
Uandishi mzima una kasoro nyingi sana. Lakini sio haba, ujumbe umefika.
Nitajaribu kuchambua baadhi ya hoja kwa uchache.

1/Ni makosa makubwa sana kuilinganisha KCMC na Muhimbili kwa sababu...
-Muhimbili ni shirika kuu la serikali(umma) lina fungu kubwa rasmi la bajeti yake kutoka serikalini kila mwaka kwa ajili ya kuendesha kila kitu. Idadi ya watumishi wa Afya walioajiriwa Muhimbili ni wengi kuliko taasisi yoyote ya Afya hapa tanzania(interms of Patient to medical personnel ratio), na wote wanalipwa na serikali, tena mishahara mikubwa zaidi kuliko watumishi wengine wote wa Afya hapa Tanzania wa serikali.(Hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi ya watumishi wa Sekta ya Afya serikalini)

-KCMC ni taasisi ya kanisa, inaendeshwa kwa pesa za kanisa, misaada ya marafiki, malipo ya wagonjwa wanapotibiwa na ruzuku ya serikali. Wanajiendesha kwa wakati mgumu sana. Kuajiri watumishi wao itakuwa ni mbinde kweli kweli.

2/Japokuwa sijafanikiwa kufika KCMC kwa miaka mingi sana, lakini mara kadhaa siku za hivi karibuni nimeona kupitia kwenye vyombo vya habari kuwa ndani ya miaka mitatu wameweza kuanzisha vitengo vipya maalum vya Dharula(Emergency), Moto(Burn), Figo bandia, Kansa, Ulemavu wa mifupa, kitengo cha kihasibu cha malipo kutumia mtandao/benki nk.
Sasa sijui kama hao wakuu wao wapya waliyakuta hayo tayari au wao ndio waliwezesha hayo?

3/Ukweli ni kwamba mpaka sasa KCMC ndio hospitali tegemeo sana kwa ukanda mzima wa Kaskazini, ikihudumia mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga, lakini pia mikoa ya Singida, Dodoma na baadhi ya maeneo ya Kenya nk. Kuna vitengo viko pale(kama macho, ngozi nk) ambavyo ni tegemeo kubwa kwa Afrika na dunia. Lakini KCMC imekuwa ikipewa ruzuku kidogo mno kutoka serikalini. Katika mazingira hayo usitegemee mambo makubwa sana zaidi ya watu kutibiwa na kwenda zao. To sustain that thing sio jambo la mchezo mchezo.

4/Tuhuma nyingi zimelenga watu fulani badala ya kulenga hoja. Na nyingi ni hisia zenye aina fulani ya chuki au wivu. Kwa mfano, mleta mada anahoji kwanini viongozi wa hospitali hiyo ambao ni madaktari wanafanikisha huduma bora katika hospitali zao binafsi lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa KCMC? Jibu ni moja tu, kule kunakomlipa mtu vizuri kutakuwa bora tu.

5/Nadhani KCMC ni mali ya kanisa la Lutherani Tanzania kwa 100%. Serikali ni mdau tu mwenye dhamana ya kuhakikisha malengo makuu ya KCMC ya kutoa huduma za Afya yanatekezwa. Sasa malalamiko yake dhidi ya Kanisa hilo katika ufujaji wa fedha zake zenyewe yanakosa nguvu ya kufanyiwa kazi hata kama ni malalamiko yana ukweli kabisa. Ni nani wa kufuatilia hayo kwa kina? Ni nani wakuchukua hatua dhidi ya Kanisa hilo?
 
Napenda kuona mabadiliko makubwa yakifanywa hapo KCMC la sivyo wahusika watakuwa kwenye matatizo mara moja!
 
Hebu nipeni maelezo kwa ufupi Serikali na KKKT wanamiliki hiyo hosp kwa makubaliano yapi. Na wananufaika vipi. Maana mkisema kuna ufisadi mara sijui raisi aende, mara oooh wazir wa afya wakati ni hospital ya asasi ya kidini nashindwa elewa
Gonga like. Nipe maelezo. Sitaki povu

Kumkoma nyani geladi
 
Yaliyosemwa yafanyiwe uchunguzi, sipendi kudharau hoja maana mbeleni huwa inamadhara mkubwa.
 
Back
Top Bottom