This is known as delay tactic!
Not only a delaying tactics, but CCM trying to play peoples mind away!.
Karume na Seif hili waliliona ndio maana walifanya siri. Kwa kutumia hoja ya referendum, CCM inataka kuwafanya Wanzanzibari wote ni mataahira. Hivi kweli hoja ya umoja ndio mkawaulize wananchi!. Mbona hoja kubwa za kuua mamlaka ya nchi na kujisubmit kwenye muungano, hamkuwauliza? leo ndio muwaulize kujiunga na CUF?!.
Hoja ya kuuwa ASP kuiunganisha na TANU ya bara kuunda CCM hakuwauliza ila kuunganisha CCM ZnZ na CUF ZnZ zote za huko ndio waulizwe wananchi?!.
Rais wa Zanzibar alikuwa Makamo, kapokwa, he is nothing kwenye muungano, hamkuwauliza, lakini leo kumfanya Seif/Duni/ au Hamad Rashid kuwa Waziri Kiongozi ndio mkaulize?.
Articles za Union zilikuwa na items 11, sasa zimeongezwa ziko zaidi ya 20, hamkuuliza leo kuongeza item 1 tuu ya serikali ya umoja wa kitaifa ndio mkaulize wananchi?.
Hawa CCM wana lao jambo, tena hawaitakii mema Zanzibar.
Alhamisi baraza linaijadili hoja, Mungu awabariki muamue uamuzi wa busara kwa kuweka maslahi ya Zanzibar mbele na sio kuendekeza siasa za vyama.
Huu ni mustakabali wa nchi, sio vyama!.