No half Revolutions: Resignation or dissolution is not enough; The parliament should go too

Pande za shilingi ziko mbili. zimeshageuzwa zaidi ya hapo, hakuna mabadiliko. 2015 mbali sana.

Hivi mnafikiri mnaweza kuchukuwa madaraka ya hii nchi? si 2015 hata 2030 hamchukui, si kwa nguvu si kwa kura.
 
Mapinduzi yanakuja naturally.
Hakuna chama kitacholeta mapinduzi Tanzania. Kwa sababu watu hawajali ni chama gani unatokea kwani vyote vina wezi na wabadhirifu wa fedha.
You can write books, conduct seminars and travel all over Tanzania. But change comes from the hearts of people, not from Politicians. Once politicians (especially career politicans) get involved, the revolt will loose its meaning.
I still don't believe CDM is the right Party, and I will keep telling my people that.

Yes mapinduzi (Revolution) rhetoric is outdated and lately in modern history never worked very well, mfano mzuri milolongo yake africa with no better results infact they just made things worse.

Cha msingi hapa ni upeo na ufunuo wa mawazo ya wananchi wetu. Hapa kwetu tumeona katika hichi kipindi cha miaka kama ishirini nguvu ya CCM ikipungua taratibu. Haitoshi sisi hapa JF kusema CCM haifai ilhali majority ya waTz wakiendelea kuipigia kura CCM na kuirudisha madarakani, hivyo cha msingi ni kuitoa CCM madarakani kwa njia za demokrasia ambayo katiba yetu hata hii mbovu ya sasa inawezekana, na hilo ndio la msingi. Siku wananchi watakapochoka (not far from now hopefully) kuipigia kura CCM basi tutakua na chama kipya madarakani sio Mapinduzi ya bunduki bali mapinduzi ya fikra ndio yanahitajika bongo yetu.

Imefika muda chama kingine kiingie madarakani tuone upeo wao na utendaji wao ukumbuke hakuna guarantee kuwa CDM wakichukua nchi basi watakuwa bora kuliko CCM ila ni vyema tuona nao utendaji wao ukoje...

MMM,

Unapoadvocate mapinduzi bila kusema nani waingie madaraka is not enough haitoshi kusema ooh CCM waondoke bila kusema mbadala iwe vipi.

Hili sakata la sasa la kina Zitto ni kwa mujibu wa sera na siasa zetu za sasa na katiba iliyoko, Zitto can only work na sheria na taratibu za bunge alokuwemo. Na mimi nakata dhana kuwa utaratibu wote ni mbovu nafikiri swala kubwa ni watendaji na kujiuzulu ni kawaida hata kwa wenzetu ambao wamepea kidemokrasia ndio kawaida hawakimbilii kubadili utaratibu au katiba kila mara mambo yakiharibika ila huwashurutisha watu wawajibike au basi hicho chama hupoteza imani na wananchi na kupoteza madaraka kwa kupitia KURA...
 
Wadudu wa maradhi wanapokuwa sugu(resistance) huwa hawabadiliki, kinachotokea ni mbinu za kubadilisha vijiasili(code) ili viweze kukwepa 'target' ya dawa husika. Na hufanya hivyo kila inapoletwa dawa mpya.

Hivi ndivyo serikali ya CCM inavyochezea akili za Watanzania. Kulikuwa na wakati wa kuunda tume ambazo hatujui matokeo yake. Tume za kupooza munkari wa Watanzania. Hili likashtukiwa na Wananchi,limeonekana kutofanya kazi upande wa serikali, resistance ikaonekana haifanyi kazi.

Umezuka utamaduni wa kuiacha serikali ifanye kazi kama tulivyoona tuhuma za Kagoda. Hapa wanaotumiwa ni Polisi, idara ya mkurugenzi wa mashitaka na mkuu wa makosa ya jinai. Tumeona jinsi watu walivyouawa na mabomu, tunachojua ni kuwa Rais alitoa rambi rambi. Hatujui matokeo ya uchunguzi kama yale ya Kagoda na kashfa nyingine. Waziri aliyehusika yupo kazini na hakuna aliyeajibika. Utadhani mabomu yaliamua kulipuka tu baada ya kuchoka na wale waliokufa ni kazi ya mola. Ile resistance inafanya kazi

Imetokea kashfa ya rada, serikali ikakimbilia kushughulikia jambo hilo, kama zilivyo kashfa nyingine hii nayo imeisha kiutalaam hakuna anayewajibika. Pesa zilitoka zenyewe Hazina zikachukua British airways hadi London. Alitumwa waziri kwenda kuzichukua.

Suala la ripoti ya CAG siyo geni. Hapa JF tumelipigia kelele sana miaka mingi tu. Hakuna anayejali.
Kinachoshangaza anayepokea taarifa ni Rais na huonekana akiwa na taarifa iliyofungwa kama birthday gift.
Baada ya hapo inawekwa katika masanduku salama pale magogoni.

Hoja ya Zitto si ngeni ingawa ni ngeni kutinga bungeni kwa aina hii. Akili za kawaida zinatushawishi kuwa Rais ndiye mtu wa kwanza kupewa hiyo ripoti ya CAG. Mtendaji wake mkuu ni waziri mkuu. Rais na Waziri mkuu hushirikiana kuunda baraza la mawaziri. Wanashirikiana pia katika kuteua watendaji kama wakurugenzi wa miji, maafisa tawala n.k.

Ni Rais na msaidizi wake peke yao wanaoweza kuteua au kutengua uteuzi wa watendaji waliowateua.
Inapofikia mahali Rais na Waziri mkuu hawajui kwanini tuna tatizo basi wao ndio tatizo kabla ya tatizo.

Kwa vile wanajua wao ni tatizo inabidi waje na usugu(resistance). Usugu sasa ni kuita wazee na kuelezea tatizo na si ufumbuzi wa tatizo.

Kwa mwendo huo sioni kwanini tuamini kuwa dawa infanya kazi wakati tukijua fika wadudu wanabadili code na dawa zetu hazifanyi kazi. Miaka 50 ni mingi sana na sijui kama ipo nafasi ya miaka hata mitano ya kusubiri.

Endapo tutaruhusu hali hii kwa dhana ya heri nusu ya shari kuliko shari kamili,wataendelea kutuchezea kama wendawazimu. Nadhani ni wakati sasa tuache kuangalia dalili za ugonjwa bali tutafute ugonjwa uko wapi.

Na hapa nasema wazi tatizo si mawaziri wala waziri mkuu, tatizo ni Rais aliyeshindwa kutimiza kazi tulizompa watanzania.
Tangu alipoingia Ikulu tumempa nafasi za kutosha na tumejaribu mara nyingi. Sidhani kama tunahitaji nafasi zaidi huku watu wakitupora. Hata kanuni za asili zinatueleza kuwa tuna nafasi ya kujitetea.Ni wakati wa kumwambia Rais, tafadhali sana mpishe mwenye nia na mapenzi mema na nchi yetu.
Tuanze na Rais ili ajae awadhibiti wateule wake na hapo tutakuwa na standard.

Sisi ndiyo wenye nchi tuliomwajiri Rais. Hatukumwajiri Waziri mkuu, mawaziri, makatibu wakuu au wakurugenzi. Tuna haki ya kumwambia sasa basi tumechoka tunaomba atupishe.

Rais hawezi kukusanya kodi zetu, akawaachia wajanja wasiozidi 100 watubebeshe mzigo wa madeni na inflation iliyofikia 20% halafu tumtafute kibarua wake na kumsulubu.

Kwanini tusianze na Rais tliyemwajiri! Tutakubali kuchezewa hivi hadi lini?
Tunarithisha watoto wetu madeni na umasikini badala ya siku njema za usoni kwasababu tunamuonea haya.

Muda wa kufikiri umekwisha! Ni wakati sasa Kikwete apumzishwe na aambiwe wazi tumemchoka sana na uvumilivu sasa basi.
 
Nguruvi huwezi kuajiri hata hausigeli utaweza kumuajiri Rais.

Rais hakuajiriwa na wewe. Rais kaajiriwa kwa uwezo wake.

Nawashangaa mnaolalama kuhusu Rais. Huyohuyo aliyewaletea mwanzo wa demokrasia ya ukweli leo amekuwa mbaya? huyohuyo anaeweka mawaziri vinara ndani, leo mnamuona hafai? huyohuyo anejenga zahanati nchi nzima ambazo hazikuwepo kabla yake mnamuona hafai?

Nna uhakika upinzani hautokani na mapungufu ya Kiongozi upinzani unatokana na shinikizo la tabaka fulani kwa maslahi yao binafsi kwa kuwa tu, wanahofia miaka ijayo na si leo. Wanaona na wanaelewa kuwa kwa mwenendo huu wa Kikwete kuzifunguwa sehemu zilizofungwa kuanzia na mkoloni, kwao itakuwa shida.

Hakuna cha zaidi ila hilo. Na hilo Kikwete na wengine wengi wenye fikra ndefu wanaliona waziwazi.

Kifo cha 83 / 17 kimewadia na hakiwafurahishi wengi.

Nashanga pale watu wanapolalamika wawekezaji kupewa Ardhi kubwa waziendeleze lakini hakuna anaeuliza kwanini tabaka fulani linahodhi Ardhi kubwa baada ya Serikali. Na wao si wawekezaji ni wafuasi tu wa imani fulani, na Ardhi hiyo wanayohodhi hawajaiendeleza hata kwa asilimia tano. Kulikoni?
 
Heri ulivyokuwa unatumia jina lileee angalau ulikuwa unaeleweka kidooogo. Hivi Mohamed Said naye kafia wapi??

Uwezo wa muajiriwa haimaanishi kwamba anaweza kujiajiri mwenyewe bila ya kuajiriwa na mwajiri na kwenye ajira wewe unajua labda Mkuranga kuwe hakuna kanuni za ajira, kwamba muajiriwa ili aajiriwe ni lazima yeye akubaliane na masharti (terms) ya muajiri. Masharti ya ajira ya Rais yamo kwenye katiba na si hiyari kwa Rais kuyafuata bali ni lazima!!
 
Hivi kwanini sheria kama ya CAG haiweki triggers za kuilazimisha serikali?
 
Have we been there?? Time and time again,
MMJ, ooh dear, have we been there?
Your account of history left me with the bad feelings we had those days when things were cooling down to the same normal which was before the great expectations.
I remember though young, then, 'ripoti ya jaji warioba'
what next?
Lakini, mapinduzi ya damu, kwangu ni hapana.
Ccm kuondoka, lazima, katiba ya watu ndio. Lazima.
Tunajiweka mikononi mwa mtu gani? tusikubali kujikabidhi kwa mtu au chama kingine tena, wananchi tuchukue madaraka kupitia katiba.
Je tunaweza kujikabidhi future yetu kwa tume ya katiba?
 
Mwanakijiji sisi hatuhangaiki kubadili sheria badala yake tuko bize kubadili watu. Leo hii tangu Jaji Nyalali aseme kwamba kuna sheria Kandamizi 40 zinatakiwa zifutwe ni ngapi mpaka sasa zimerekebishwa na tume ya kurekebisha sheria au ni ngapi zimefikishwa bungeni kwa ajili ya kuondolewa?

Kuna makala uliandika kuhusu nguvu za mwendesha mashtaka wa serikali, ni wapenda mapinduzi wangapi wamewahi hata kujishughulisha na kupeleka muswada bungeni aongezewe nguvu na kinga kama wanaona sheria iliyopo haitoshelezi kudili na wahalifu walipo. Ni mara ngapi tumewaambia watumie sheria ya uhujumu Uchumi kuwashitaki hawa wanaotufilisi lakini HAWATAKI?

Tatizo hata wale tunaowaona wako tofauti na CCM na wao pia wamedurufu (copy) mfumo wa kutenda mambo toka CCM. Moto hauzimwi kwa moto!!
 
Quote of the day!!!!!
 
Nguruvi huwezi kuajiri hata hausigeli utaweza kumuajiri Rais.

Rais hakuajiriwa na wewe. Rais kaajiriwa kwa uwezo wake.

Nawashangaa mnaolalama kuhusu Rais. Huyohuyo aliyewaletea mwanzo wa demokrasia ya ukweli leo amekuwa mbaya? huyohuyo anaeweka mawaziri vinara ndani, leo mnamuona hafai? huyohuyo anejenga zahanati nchi nzima ambazo hazikuwepo kabla yake mnamuona hafai?

Nna uhakika upinzani hautokani na mapungufu ya Kiongozi upinzani unatokana na shinikizo la tabaka fulani kwa maslahi yao binafsi kwa kuwa tu, wanahofia miaka ijayo na si leo. Wanaona na wanaelewa kuwa kwa mwenendo huu wa Kikwete kuzifunguwa sehemu zilizofungwa kuanzia na mkoloni, kwao itakuwa shida.

Hakuna cha zaidi ila hilo. Na hilo Kikwete na wengine wengi wenye fikra ndefu wanaliona waziwazi.

Kifo cha 83 / 17 kimewadia na hakiwafurahishi wengi.

Nashanga pale watu wanapolalamika wawekezaji kupewa Ardhi kubwa waziendeleze lakini hakuna anaeuliza kwanini tabaka fulani linahodhi Ardhi kubwa baada ya Serikali. Na wao si wawekezaji ni wafuasi tu wa imani fulani, na Ardhi hiyo wanayohodhi hawajaiendeleza hata kwa asilimia tano. Kulikoni?
Sisi Watanzania (sio mimi Nguruvi) ndiyo tumwemwajiri Rais. Tatizo ni kuwa hujui kuwa Rais ndiye mtumishi namba moja wa umma. Hujitambui kuwa alipokuja kukuomba kura alikuwa anaomba ajira! Ni dhana ngumu sana inahitaji kufikiri na kuona mbali zaidi ya pua.

Pili, nashindwa kuelewa kama unafahmu kuwa demokrasia ni haki yako ya kuzaliwa. Hupaswi kuletewa na mtu. Demokrasia siyo jiwe unaloweza kulibeba na kulitua mahali! Nayo pia ni dhana pana! Anyway tuyaache hayo

Na mwisho, hebu jibu hoja kwa hoja tena zenye mashiko! kuna wakati kukaa kimya nako ni busara
 
Wadudu wa maradhi wanapokuwa sugu(resistance) huwa hawabadiliki, kinachotokea ni mbinu za kubadilisha vijiasili(code) ili viweze kukwepa 'target' ya dawa husika. Na hufanya hivyo kila inapoletwa dawa mpya.

Hivi ndivyo serikali ya CCM inavyochezea akili za Watanzania. Kulikuwa na wakati wa kuunda tume ambazo hatujui matokeo yake. Tume za kupooza munkari wa Watanzania. Hili likashtukiwa na Wananchi,limeonekana kutofanya kazi upande wa serikali, resistance ikaonekana haifanyi kazi.

Umezuka utamaduni wa kuiacha serikali ifanye kazi kama tulivyoona tuhuma za Kagoda. Hapa wanaotumiwa ni Polisi, idara ya mkurugenzi wa mashitaka na mkuu wa makosa ya jinai. Tumeona jinsi watu walivyouawa na mabomu, tunachojua ni kuwa Rais alitoa rambi rambi. Hatujui matokeo ya uchunguzi kama yale ya Kagoda na kashfa nyingine. Waziri aliyehusika yupo kazini na hakuna aliyeajibika. Utadhani mabomu yaliamua kulipuka tu baada ya kuchoka na wale waliokufa ni kazi ya mola. Ile resistance inafanya kazi

Imetokea kashfa ya rada, serikali ikakimbilia kushughulikia jambo hilo, kama zilivyo kashfa nyingine hii nayo imeisha kiutalaam hakuna anayewajibika. Pesa zilitoka zenyewe Hazina zikachukua British airways hadi London. Alitumwa waziri kwenda kuzichukua.

Suala la ripoti ya CAG siyo geni. Hapa JF tumelipigia kelele sana miaka mingi tu. Hakuna anayejali.
Kinachoshangaza anayepokea taarifa ni Rais na huonekana akiwa na taarifa iliyofungwa kama birthday gift.
Baada ya hapo inawekwa katika masanduku salama pale magogoni.

Hoja ya Zitto si ngeni ingawa ni ngeni kutinga bungeni kwa aina hii. Akili za kawaida zinatushawishi kuwa Rais ndiye mtu wa kwanza kupewa hiyo ripoti ya CAG. Mtendaji wake mkuu ni waziri mkuu. Rais na Waziri mkuu hushirikiana kuunda baraza la mawaziri. Wanashirikiana pia katika kuteua watendaji kama wakurugenzi wa miji, maafisa tawala n.k.

Ni Rais na msaidizi wake peke yao wanaoweza kuteua au kutengua uteuzi wa watendaji waliowateua.
Inapofikia mahali Rais na Waziri mkuu hawajui kwanini tuna tatizo basi wao ndio tatizo kabla ya tatizo.

Kwa vile wanajua wao ni tatizo inabidi waje na usugu(resistance). Usugu sasa ni kuita wazee na kuelezea tatizo na si ufumbuzi wa tatizo.

Kwa mwendo huo sioni kwanini tuamini kuwa dawa infanya kazi wakati tukijua fika wadudu wanabadili code na dawa zetu hazifanyi kazi. Miaka 50 ni mingi sana na sijui kama ipo nafasi ya miaka hata mitano ya kusubiri.

Endapo tutaruhusu hali hii kwa dhana ya heri nusu ya shari kuliko shari kamili,wataendelea kutuchezea kama wendawazimu. Nadhani ni wakati sasa tuache kuangalia dalili za ugonjwa bali tutafute ugonjwa uko wapi.

Na hapa nasema wazi tatizo si mawaziri wala waziri mkuu, tatizo ni Rais aliyeshindwa kutimiza kazi tulizompa watanzania.
Tangu alipoingia Ikulu tumempa nafasi za kutosha na tumejaribu mara nyingi. Sidhani kama tunahitaji nafasi zaidi huku watu wakitupora. Hata kanuni za asili zinatueleza kuwa tuna nafasi ya kujitetea.Ni wakati wa kumwambia Rais, tafadhali sana mpishe mwenye nia na mapenzi mema na nchi yetu.
Tuanze na Rais ili ajae awadhibiti wateule wake na hapo tutakuwa na standard.

Sisi ndiyo wenye nchi tuliomwajiri Rais. Hatukumwajiri Waziri mkuu, mawaziri, makatibu wakuu au wakurugenzi. Tuna haki ya kumwambia sasa basi tumechoka tunaomba atupishe.

Rais hawezi kukusanya kodi zetu, akawaachia wajanja wasiozidi 100 watubebeshe mzigo wa madeni na inflation iliyofikia 20% halafu tumtafute kibarua wake na kumsulubu.

Kwanini tusianze na Rais tliyemwajiri! Tutakubali kuchezewa hivi hadi lini?
Tunarithisha watoto wetu madeni na umasikini badala ya siku njema za usoni kwasababu tunamuonea haya.

Muda wa kufikiri umekwisha! Ni wakati sasa Kikwete apumzishwe na aambiwe wazi tumemchoka sana na uvumilivu sasa basi.

Mkuu umenena maneno murua na ukiangalia na jinsi anavyochukulia mambo ni kweli ameshindwa au anajiona hana cha kupoteza kwani 2015 yeye hasimami tena kuomba kura zetu. Hivi katika mazonge zonge yote haya unaweza kuwa nje ya nchi kwa safari ambazo hazina tija kwa nchi yako kweli?
 
Mwanakijiji sisi hatuhangaiki kubadili sheria badala yake tuko bize kubadili watu. Leo hii tangu Jaji Nyalali aseme kwamba kuna sheria Kandamizi 40 zinatakiwa zifutwe ni ngapi mpaka sasa zimerekebishwa na tume ya kurekebisha sheria au ni ngapi zimefikishwa bungeni kwa ajili ya kuondolewa?

Kuna makala uliandika kuhusu nguvu za mwendesha mashtaka wa serikali, ni wapenda mapinduzi wangapi wamewahi hata kujishughulisha na kupeleka muswada bungeni aongezewe nguvu na kinga kama wanaona sheria iliyopo haitoshelezi kudili na wahalifu walipo. Ni mara ngapi tumewaambia watumie sheria ya uhujumu Uchumi kuwashitaki hawa wanaotufilisi lakini HAWATAKI?

Tatizo hata wale tunaowaona wako tofauti na CCM na wao pia wamedurufu (copy) mfumo wa kutenda mambo toka CCM. Moto hauzimwi kwa moto!!

Tatizo kuu ni watu au tuseme wanasiasa wetu sababu hata bila kubadili katiba kwa katiba na sheria zilizoko sasa zinaruhusu kabisa watu kushtakiwa kwa uhujumu uchumi au matumizi mabovu ya ofisi zao. Swala ni wangapi wameshitakiwa au mbona hata CDM hawapeleki mahakamani kesi kuwashtaki mawaziri kwa ubadhirifu maana haikatazwi mtu yeyote mwenye ushahidi kufanya hivyo.

Hivyo hata kama tukiwa na katiba mpya na tunashindwa kuwawajibisha viongozi wetu haitasaidia, suala ni kuanza kufanya hivyo vitu sasa. Zitto kumlazimisha WM kujiuzulu ni mwanzo maana hio kama ikifanikiwa itatrigger Rais abadili baraza lote. Kumuimpeach Rais kwa katiba ya sasa ni ngumu maana ni lazima 75% ya wabunge waafiki ambayo ni ndoto. Ila kujadili waziri mkuu kujiuzulu inawezekana ndio maana wanakusanya signature hizo.

Kuhusu hizo tume kuanzia za Nyalali mpaka Warioba ni kweli vitu vingi hafijafanyiwa kazi ingawa baadhi vimefanyiwa ni wakati wetu huu sasa kwenye huu mjadala wa katiba mpya tuhakikishe kuwa mapendekezo yote mazuri yanashirikishwa na ni matumaini yangu kuwa itakuwa hivyo ukichukulia kuwa Warioba ndio mwenyekiti wa hiyo tume...so fingers cross tuone na kuhimiza ni wajibu wetu sote kuona tunapata katiba nzuri lakini vilevile ni wajibu wetu kuwazonga na kuwahimiza wabunge wetu bila kujali chama wawakalie kooni mawaziri wote wabovu na kuwavalia njuga ama wajiuzulu ama washtakiwe sio longolongo tu kila siku.
 
Mzee Mwanakijiji, you have said more than a nutshell can hold; What you have said cannot be overemphasized. We, the People, should not settle for resignations or desolation. We need to make the parliament go! the question is how do we do it. Should we take to the street? (the police does not have enough bullets for us all any way). How are we to return the government to the The People?
 
Sisi Watanzania (sio mimi Nguruvi) ndiyo tumwemwajiri Rais. Tatizo ni kuwa hujui kuwa Rais ndiye mtumishi namba moja wa umma. Hujitambui kuwa alipokuja kukuomba kura alikuwa anaomba ajira! Ni dhana ngumu sana inahitaji kufikiri na kuona mbali zaidi ya pua.

Pili, nashindwa kuelewa kama unafahmu kuwa demokrasia ni haki yako ya kuzaliwa. Hupaswi kuletewa na mtu. Demokrasia siyo jiwe unaloweza kulibeba na kulitua mahali! Nayo pia ni dhana pana! Anyway tuyaache hayo

Na mwisho, hebu jibu hoja kwa hoja tena zenye mashiko! kuna wakati kukaa kimya nako ni busara
Back to square one.
Hatujamwajiri rais wetu. Katiba yetu haituwezeshi sisi kumwajiri rais.Hatuwezi hata kumwondoa, the same system ipo kwenye vyama mbadala, kuna watawala na wengineo ni watwana. Hata ukiamua kugombea nafasi fulani huruhusiwi kwa sababu wewe ni mtwana. Sasa hiyo ndiyo tuiondoe.
Tunapenda kujiaminisha kuwa tumewaajiri hawa wanasiasa ilhali hao ndio wametuajiri tuwafanyie kazi na kuwatajirisha. Dah!! aliyegundua pilau ana akili kuliko Einstein.
 
Pilau tena!? sisi ndiyo waajiri lakini hatujijui kama ni waajiri. Kutokujijua kwetu kama sisi ndiyo waajiri hakuondoi ukweli kwamba sisi ni waajiri na mwajiriwa wetu namba moja ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania ambaye kwa sasa ni Jakaya Mrisho Kikwete.

Mara zote watu wanapenda kushika vivuli na kuachana na vitu halisi. Mwanzoni niliuliza kwenye hoja ya Zitto na Sahihi zake 70 kwamba Zitto alikuwa hajui kama zilikuwa zinatakiwa siku 14 kabla ya hoja yake kufikishwa Bungeni kwa ajili ya majadiliano? Hapa nilikusudia kwamba Zitto kwa hali yoyote ile alikuwa hana uwezo wa kumlazimisha Spika ambaye ana maslahi na walioko madarakani kuitisha kikao cha Dharura cha Bunge ili kumjadili Waziri Mkuu. Lakini eti watu walikuwa wanakaa "mkao wa kula"

Tukubali kwamba mapambano yaliyopo mbele yetu ni zaidi ya kuleta "maneno Maneno"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom