Wanadai posho iongezwe wakati wengi wao huko wanakwenda kuuchapa usingizi tuu!!! Jamani ni mahospitali mangapi hayana dawa!!! Kule mkoani Kilimanjaro hospitali kubwa ya rufaa tena yenye jina kubwa KCMC haina mashine ya CT-SCAN huu ni mwaka wa nne, serikali angalieni hali za wananchi wenu wa chini, ni wagonjwa wengi sana wanakufa kwa kukosa vipimo lakini wapo watu wachache wenye kupenda matumbo yao wanasema posho ya Tsh 300,000 kwa siku ni ndogo, vipi walimu wanaolipwa Tshs 250,000 kwa mwezi!!! Mbona wao hamuwaonei huruma au kutetea maslahi yao!!! Hivi hii serikali yetu ina nini!!! Au ndo kasi mpya, ari mpya ya kuchukua chako mapema!!!