NMB yaipa Serikali Gawio la Tsh. Bilioni 45.5

NMB yaipa Serikali Gawio la Tsh. Bilioni 45.5

Wananyonya sana wafanyakazi faida wanagawia serikali. Kumbe kwa mafweza hayo mengi walikuaa wanaweza kabisa kupunguza Riba kwenye mikopo yao
Mtwa Mkulu : hapo kuna vitu vya msingi kumbe:

1. Huenda wana riba kubwa kwenye mikopo yao na ndio maana kila siku tunasikia nyumba za wateja zinauzwa na madalali wa benki kwa wateja wengi kushindwa kulipa mikopo!

2. Hii benki ina kesi nyingi mno katika mabaraza ya ardhi na mahakamani kwa kushindwa kuwakabidhi wanunuzi wa nyumba baada ya kununua kwenye minada!

3. Huenda hawa ni wanyonyaji kwa wafanyakazi kazi... hii ni hoja kubwa mno! Inahitaji majibu na ufafanuzi wa kina kama walivyojitutumua na faida na pia Gawio kubwa kwa Serikali??

4. Hii benki ndio inaongoza kwa kuwa na kesi nyingi dhidi ya wafanyakazi katika Mahakama za Kazi Tanzania.
Wananyonya sana wafanyakazi faida wanagawia serikali. Kumbe kwa mafweza hayo mengi walikuaa wanaweza kabisa kupunguza Riba kwenye mikopo yao

Basi kama hayo yote ni sahihi hata hilo gawio waliotoa pamoja na mbwembwe zote hizo ni kiduchu mno. Huenda hata walitakiwa kutoa gawio mara kumi kuliko kama walivyofanya!

Ni mawazo fikirishi.

Cc FaizaFoxy, Evelyn Salt, Pascal, Mpwayungu Village, RaraaaReree, Involved et al
 
Serikali imepokea gawio la Shilingi bilioni 45.5 kutoka benki ya NMB PLC ikiwa ni sehemu ya faida waliyopata katika mwaka 2022 ili kuboresha huduma za jamii nchini ikiwemo elimu na afya nchini kwa maendeleo endelevu.

Akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi hicho wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 25 ya mafanikio ya benki hiyo iliyofanyika Juni 17, 2023 jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imepokea gawio kubwa ambalo limetolewa na taasisi ya fedha nchini.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bi Ruth Zaipuna amesema gawio las benki ya NMB kwa Serikali limeendelea kuongezeka kwa kiasi kikubwa na endelevu kutoka Shilingi Bilioni 4.5 mwaka 2009 hadi kufikia Shilingi Bilioni 45.5 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 911 katika kipindi hicho cha mrejesho.

Katika kusherehesha hafla hiyo, burudani kutoka vikundi mbalimbali zilipata wasaa wa kuburudisha hadhira iliyofurika katika ukumbi wa Mlimani City akiwemo Msanii wa Music wa dance Christian Bella pamoja na vikundi vya ngoma.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, Mawaziri, Makatibu Wakuu akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania Nyakaho Mahemba.View attachment 2661020View attachment 2661023View attachment 2661021View attachment 2661024View attachment 2661022View attachment 2661025
IMG-20230618-WA0030.jpg
View attachment 2661027View attachment 2661026
IMG-20230618-WA0024.jpg
IMG-20230618-WA0028.jpg
IMG-20230618-WA0029.jpg
IMG-20230618-WA0027.jpg
 
Huyu afisa Mtendaji wa NMB anafaa sana kuwa Gavana wa BOT

Ana mikakati inayotekelezeka na anasimamia utekelezaji.

BOT wwmekuwa hawana tija kubwa zaidi ya kutoa taarifa tu. Hata mzunguko wa fedha wamekuwa kama hawana dhamana nao

Mavi ya kuku labda awe gavana ya spidi ya mabasi!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki hafla ya NMB kukabidhi Gawio kwa Serikali na kusherekea Miaka 25 ya Safari ya Mafanikio ya Benki ya NMB katika Ukumbi wa Mlimani City leo 17 Juni, 2023.

Akizungumza kwenye halfa hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amemshukuru Rais kwa kuhuduria na kupokea gawio kwa Serikali kutoka Benki hiyo.

Katika kipindi cha miaka 25 ya Benki hii, ilianza kama Benki ndogo ikiwa na mtandao wa matawi 97 nchini bila kuwa na ATM wala mawakala.

View attachment 2660342
Ruth Zaipuna, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB
Mwaka 2005, Serikali ya Tanzania ilibinafsisha kwa kuuza hisa ya 49% na mwaka 2008 ilipunguza kisa zake zingine na kufanya iorodheshe kwenye soko la hisa la Dae es Salaam ikiwa na hisa 31.8%

Sasa ina matawi 227 Nchini, ATM 781, Mawakala 23679 na Akaunti Milioni 6.3 Nchi nzima. Hii inafanya kuwa benki yenye akaunti nyingi zaidi kuliko benki zingine Tanzania na Mwaka 2022 pekee, benki hii ilisajili akaunti mpya milioni 1.2.

Benki hii itatoa gawio la Bilioni 45.5 kwa Serikali na tayari imeshawekwa kwenye Akaunti ya hazina na kwa ujumla, bilioni 143.1 zimetolewa kwa wanahisa wote mwaka huu.

Aidha, kwa mwaka 2022, NMB imelipa kodi ya tsh bilioni 453 Serikali.

Katika kusherekea miaka 25 ya Benki hii, Zaipuna amesema tayari Bilioni 2.5 kujenga shule ya mfano kwenye mkoa na eneo atakalopendekeza Rais Samia.

Rais Samia ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa NMB kwa kazi kubwa waliyofanya kwa kuwa Benki kiongozi nchini kwa kuzalisha faida, na akiwa ya 3 Kwenye Ukanda wa Afrika Mashafiki kwa Kutengeneza faida kubwa.

Aidha, Serikali imeanza kufanya tathimini ya Mashirika yote ya Umma na yale ambayo Serikali ina hisa kubwa ili kubaini mashirika yasiyo na faida na yaliyoshindwa kujiendesha yakiitia hasara Serikali yafutwe, yapewe miongozo jinsi ya kujiendesha au yasaidiwe ili kwa pamoja wote wazalishe faida.

Amesema lengo la Serikali kuanzisha mashirika hayo ni kuisaidia kuzalisha fedha na si mashirika kula serikalini bila kurejesha faida na mengi yakiwa ya aina hii.

Rais Samia amewataka wananchi wanaopatiwa mikopo na benki hiyo bila dhamana warudishe imani hiyo ili kutoiua au kuiangusha.
Hiyo ni comedy kma magu alivyokua anapewa gawio...maza nae anapita mulemule mana hana hata uwezo wa kutawala
 
Mtwa Mkulu : hapo kuna vitu vya msingi kumbe:

1. Huenda wana riba kubwa kwenye mikopo yao na ndio maana kila siku tunasikia nyumba za wateja zinauzwa na madalali wa benki kwa wateja wengi kushindwa kulipa mikopo!

2. Hii benki ina kesi nyingi mno katika mabaraza ya ardhi na mahakamani kwa kushindwa kuwakabidhi wanunuzi wa nyumba baada ya kununua kwenye minada!

3. Huenda hawa ni wanyonyaji kwa wafanyakazi kazi... hii ni hoja kubwa mno! Inahitaji majibu na ufafanuzi wa kina kama walivyojitutumua na faida na pia Gawio kubwa kwa Serikali??

4. Hii benki ndio inaongoza kwa kuwa na kesi nyingi dhidi ya wafanyakazi katika Mahakama za Kazi Tanzania.

Basi kama hayo yote ni sahihi hata hilo gawio waliotoa pamoja na mbwembwe zote hizo ni kiduchu mno. Huenda hata walitakiwa kutoa gawio mara kumi kuliko kama walivyofanya!

Ni mawazo fikirishi.

Cc FaizaFoxy, Evelyn Salt, Pascal, Mpwayungu Village, RaraaaReree, Involved et al
Hakika mkuu umenena
 
Kwa upande wng bado gawio naliona dogo, wabaneni wanauwezo wa kutoa zaidi ya hapo hao. Wanatufanyia unyama sna kwenye kaunti zetu huku
 
H
Hiyo shule ya bilioni 2.5 ijengwe katikati ya nchi 'Dodoma' ili ifikike kirahisi na wananchi kutoka kila pembe...wanasiasa wasije jipendelea maeneo waliyozaliwa
naunga mkono hoja
bi tozo hachelewi kuchagua ikajengwe kisiwa ndui 😄 zenj huko
 
Back
Top Bottom