NMB - Ujinga wenu wa 'network inasumbua' unaharibu biashara zetu

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Tunakusanya pesa zetu kupitia NMB kwa sababu ndiyo inapatikana sehemu nyingi walipo wateja wetu; lakini mara utasikia network inasumbua na hivyo wateja wa biashara yangu wanashindwa kutuma pesa kwa wakati. Na wengine hata kama hawana nia ya kutuma pesa basi husingizia tu, network inasumbua na kutokomea na pesa. Hili tatizo lina karibu mwaka mzima sasa, kipindi ambacho tatizo la msingi lingeweza kutatuliwa. Cha ajabu lakini katika kulipa mikopo yao hata siku moja network haisumbui. Huku nu kurudishana nyuma kwa hiyo yoyote anayehusika na mambo ya IT huko NMB ahakikishe kuwa wanarekebisha na kama wanadhani wataendelea kuwa peke yao kwenye soko la vijijini wachunge sana kwani CRDB na Barclays wameanza kusogea.
 
Back
Top Bottom