NMB:Hii si sawa

NMB:Hii si sawa

Malikauli

Senior Member
Joined
Mar 3, 2012
Posts
150
Reaction score
114
Za saa hizi mabibi na mabwana..
Kwa umri nilioishi hapa duniani nimeshuhudia unyanyasaji wa kila namna unaofanya na hii serikali dhalimu na taasisi nyingine nyingi zinazopaswa kuwajibishwa na serikali hii ila hili la leo nashindwa kulivumilia..
Nimekuwa mteja wa NMB kwa miaka mitatu sasa na nilijisajili mkoani Morogoro,juzi walinitumia msg kwamba kadi yangu ime-expire nikachukue kadi yangu mpya Morogoro au tawi lolote la NMB lililopo karibu,nimeenda tawi la karibu hapa Mlimani City naambiwa napaswa nilipe Sh. 15000 ya kusafirisha kadi hii....serious? kwa kadi ambayo kwa uamuzi wenu mmeamua kuiita expired na wala si uamuzi wangu?hii kadi inakodiwa Abood kuisafirisha peke yake?Mmefanya tathmin hii 15k ina thamani gani kwa wengi wa wateja wenu ambao ni makabwela?mbona hamkunidai hata senti kunifikishia kadi yangu ya mwanzo ambayo naamin mliitoa dar mkaniletea Moro? Naamin hapa jamvini kuna watu kutoka menejimenti ya NMB wanaperuse...go and rethink.I am not gonna pay a single coin for this,tupeni hiyo card na account fungeni siku nikiwahitaji nitafungua nyingine si kwa sababu hiyo 15k sina ila nauona ni wizi wa mchana kweupe hasa ninapogundua watu waliofungiwa kadi ni wengi sana (nimekutana na watu 6 mlimani city with same problem) na this is going to give you lots of money msiyostahili.Natambua kosa si la kwenu ila ni kiburi chenu na majivuno kinachosababishwa na ukweli kwamba mmewekeza kwenye linchi lisilokuwa na utawala wa sheria,lisiloweza kusimamia wawekezaji wanafanya nini wala wanaumiza vipi wazawa.Asanteni kwa muda mliokuwa nami, ngoja nijaribu hawa wawekezaji wenzenu
 
Ndugu umeongea kwa uchungu mkubwa sana sasa tunaibiwa wazi wazi na mamlaka zinazohusika zimelala,Naamin imefikia kipindi watanzania kufanya maamuzi magumu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kwel huu ni zaidi ya uchizi kwan haiwezekan wakuchaj pesa nying kama hizo. Na kiukwel ni kuwa hizo kadi hutolewa bure
 
Kwenye mabenk kuw na kipinda cha card ku-expire ni utaratibu wa usalama kimataifa hata BOT wanahitaji hivo, hilo la 15k tuwaachie wenyewe
 
Kwanza hiyo Card wanaisafirishaje? kwa Fast-Jet au?
 
Hao watu wa nmb ni xuma kuliko unavyoweza kudhani--wanaboa sana, tena sana. Ni wezi wa kutupwa na hawana pessure na wateja kwani wanajua kwamba serikali dhalimu ya CCM imewalazimisha wafanyakazi wote wa umma kufungua akaunti zao kwenye benki hii ya kichoko--vinginevyo ingelikwisha kufa kitambo sana. Hawa wajinga wana matatizo makubwa sana na ukiwatumia tatizo kwenye emaili huwa hawajibu. Libenki lao lina matatizo lukuki--kumeza atm cards za wateja, atm kukosa fedha, matatizo ya kiufundi ya atm--na ni kila siku!!!! wapuuzi kwakubwa!

mkuu, kama wewe sio mtumishi wa serikali, nakushauri ufungue akaunti CRDB kwa kamanda Kimei--CRDB ni JEMBE!
 
Za saa hizi mabibi na mabwana..
Kwa umri nilioishi hapa duniani nimeshuhudia unyanyasaji wa kila namna unaofanya na hii serikali dhalimu na taasisi nyingine nyingi zinazopaswa kuwajibishwa na serikali hii ila hili la leo nashindwa kulivumilia..
Nimekuwa mteja wa NMB kwa miaka mitatu sasa na nilijisajili mkoani Morogoro,juzi walinitumia msg kwamba kadi yangu ime-expire nikachukue kadi yangu mpya Morogoro au tawi lolote la NMB lililopo karibu,nimeenda tawi la karibu hapa Mlimani City naambiwa napaswa nilipe Sh. 15000 ya kusafirisha kadi hii....serious? kwa kadi ambayo kwa uamuzi wenu mmeamua kuiita expired na wala si uamuzi wangu?hii kadi inakodiwa Abood kuisafirisha peke yake?Mmefanya tathmin hii 15k ina thamani gani kwa wengi wa wateja wenu ambao ni makabwela?mbona hamkunidai hata senti kunifikishia kadi yangu ya mwanzo ambayo naamin mliitoa dar mkaniletea Moro? Naamin hapa jamvini kuna watu kutoka menejimenti ya NMB wanaperuse...go and rethink.I am not gonna pay a single coin for this,tupeni hiyo card na account fungeni siku nikiwahitaji nitafungua nyingine si kwa sababu hiyo 15k sina ila nauona ni wizi wa mchana kweupe hasa ninapogundua watu waliofungiwa kadi ni wengi sana (nimekutana na watu 6 mlimani city with same problem) na this is going to give you lots of money msiyostahili.Natambua kosa si la kwenu ila ni kiburi chenu na majivuno kinachosababishwa na ukweli kwamba mmewekeza kwenye linchi lisilokuwa na utawala wa sheria,lisiloweza kusimamia wawekezaji wanafanya nini wala wanaumiza vipi wazawa.Asanteni kwa muda mliokuwa nami, ngoja nijaribu hawa wawekezaji wenzenu
unalalamika nini sasa au ndio ubahili tu kama unaona sio halali funga account tu na siyo kuanza kulalamika tafuta kopo uwe unaweka ili usiwe na makato kabisa mbona ndivyo wanavyofanya nakumbuka hata mimi niliwahi kulipia mwaka 2005 kipindi niko huko hii ni kawaida sana
 
Ninauhakia kama sio serikali hii kufanya kitendo cha udhalimu na unyanyasaji wa kulazimisha watumishi kufungua Acount NMB . wasinge kuwa na mteja hata mmoja huduma zao mbaya kauli mbaya kwa wateja tellers kuondoka na kuacha wateja kwenye foleni ndefu, Atm kukosa fedha ni vitu vya kawauda kwa NMB
 
Binafsi sijawahi kuiona atm card isiyokuwa na expire date, kwa hiyo nina wasiwasi na huyu mleta mada kama hata alijiridhisha walau kidogo kuthibitisha kama card yake kweli imeexpire maana tarehe ipo wazi tu kwenye card imeandikwa. Pili sina uhakika nae kama wakati anafungua akaunti alitumia muda wake kusoma vinzuri vigezo na masharti ya kupewa atm card, inawezekana alisaini tu form huku hajui anachokisaini. Tatu wakati aitwa kupewa card mpya sidhani kama hata alijaribu kuomba tariff ili walau aone ni katika mazingira gani anapaswa kulipia card mpya.
 
kupata kadi kwa mara ya kwanza benki nyingine bure, lakini iki-expire / kupotea unalipia sh elfu10 had elfu15 kulingana na benk, na hii ni kawaida sana, sijaona cha maana hapo ulicholalamika.
 
unalalamika nini sasa au ndio ubahili tu kama unaona sio halali funga account tu na siyo kuanza kulalamika tafuta kopo uwe unaweka ili usiwe na makato kabisa mbona ndivyo wanavyofanya nakumbuka hata mimi niliwahi kulipia mwaka 2005 kipindi niko huko hii ni kawaida sana

Mbunifu wa dili la kula hela za watu kama si tatizo kwako mlipie
 
Binafsi sijawahi kuiona atm card isiyokuwa na expire date, kwa hiyo nina wasiwasi na huyu mleta mada kama hata alijiridhisha walau kidogo kuthibitisha kama card yake kweli imeexpire maana tarehe ipo wazi tu kwenye card imeandikwa. Pili sina uhakika nae kama wakati anafungua akaunti alitumia muda wake kusoma vinzuri vigezo na masharti ya kupewa atm card, inawezekna oalisaini tu form huku hajui anachokisaini. Tatu wakati aitwa kupewa card mpya sidhani kama hata alijaribu kuomba tariff ili walau aone ni katika mazingira gani anapaswa kulipia card mpya.
Teller 4
 
Mm yangu ya nmb ili expire 2013
Nilichofurahi kwanza sikutakiwa kujaza fomu yoyote ile
Pili niliikuta kadi ipo tayari inanisubiri
Nilichotakiwa kufanya ni ku activate namba ya siri tu
Ukweli ni kwamba kadi hizi zinazo expire zinakuwa tayari zimetengenezwa na mteja anatakiwa akaichukulie pale alipofungulia mara ya kwanza
Kosa lilipo labda ni ile kudhani kwamba mteja atohama kuishi sehem nyingine
Mtoa mada fanya tathmini ndogo tu, ni faida ngapi unazipata ukiwa na atm kadi ukilinganisha na hiyo elfu 15 unayotakiwa kulipa ambayo kiukweli ni gharama ya kusafirisha kadi huko ilipo na kukufikia ww mteja
Nafurahia nmb yenye matawi mengi tz na nmb mobile banking ya uhakika
 
Back
Top Bottom