NMB - Hii si sawa

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Nimepeleka cheki yangu NMB, aliyenilipa ana akaunti Barclays. Zimepita wiki 2 salio halisomeki. Haimaye nimeenda kuulizia wakabofya kompyuta na kuniambia kuwa nina elfu kumi tu kwenye akaunti. Nikauliza sasa elfu kumi na cheki yangu vina uhusiano gani? Wakanijibu lazima niwe na zaidi ya elfu kumi na tano kwa sababu gharama ya kuingiza cheki toka benki nyingine ni 15,000. Nikauliza mbona hawakuniambia jambo hilo wakati ninawakabidhi, wakaniambia 'pole'. Nikawajulisha kuwa, mbona CRDB huwa napeleka cheki ya benki nyingine na kupata kiasi kamili cha pesa, wakasema kama vipi wanirudishie cheki yangu. Nikakubali. Kuipokea ina mihuri yao nyuma na mbele - HII SI SAWA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kaka pole,hapo kuna tatizo ila siku izi Bank charges ziko juu kila sehemu.Unapopeleka Check Bank Outward clearing ina gharama baina ya bank na bank na ni sehemu zote.ilitakiwa waangalie kwanza balance vinginevyo wakipiga tuu itakataa.Kupigwa mihuri kwe check ni sawa ikipokelewa lazima iwe na mhuhuri wa recieved.na inapotoka inakuwa na muhuri wa kurudishwa.na hapo teller naye anakuwa na muhuri wake wa kwamba kaicheki.hivyo lazima uone ni mihuri mingi,hali kama hii hutokea pia kwa aliepewa check ila akaunt ya check haina pesa.Sema wamekuchelewesha hivyo wanatakiwa kukuomba radhi.
 
Kaka hata hiyo CRDB wanakata hela nenda kachunguze tena account yako utagundua. Ila pole sana
 
Nimepeleka cheki yangu NMB, aliyenilipa ana akaunti Barclays. Zimepita wiki 2 salio halisomeki. Haimaye nimeenda kuulizia wakabofya kompyuta na kuniambia kuwa nina elfu kumi tu kwenye akaunti. Nikauliza sasa elfu kumi na cheki yangu vina uhusiano gani? Wakanijibu lazima niwe na zaidi ya elfu kumi na tano kwa sababu gharama ya kuingiza cheki toka benki nyingine ni 15,000. Nikauliza mbona hawakuniambia jambo hilo wakati ninawakabidhi, wakaniambia 'pole'. Nikawajulisha kuwa, mbona CRDB huwa napeleka cheki ya benki nyingine na kupata kiasi kamili cha pesa, wakasema kama vipi wanirudishie cheki yangu. Nikakubali. Kuipokea ina mihuri yao nyuma na mbele - HII SI SAWA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

kwa hiyo akaunti haina hata 15000?..........pole squared
 
hawa jamaa wezi, mimi nina akaunti yangu ya kawaida lakini hawa jamaa wameigeuzkuwa a biashara ivyo wnanla 10000 kila mwezi, nimewalalaikia kila siku jibu lao ni lile lile tunashughulikia na ukifika mwisho wa mwezi panga kama kawaida. Miezi imekatika lakini bado wanaendelea na uhuni wao. Nawatafutia siku niwafungie kazi nifunge branch saa mbili asubuhi naona ndio tutaelewana.
 
Bank nyingi sasa hivi zina matatizo ya kubalance statement zao shauri ya matatizo ya kiuchumi yaliyoikumba Tanzania. Watu walikopa mabilioni na wakawa defaulters shauri ya hali mbaya. Na asset walizotumia kama collateral nyingi valuation zilikuwa za uongo. Hivyo bank charges zitakuwa kila mahali na pia wanachukuwa pesa kidogokidogo kama elfu 1,2 au 10 kutoka kila account, kama hujastuka wataendelea hadi utakapostuka halafu wanarudisha na kuomba samahani. Ila ni intentional
 
wezi sanaaa naomba habari ziwafikie NMB kuwa kunasiku nitafunga branch asubuhi asubuhi, nimeziesabu ten ten zangu sasa zinakaribia Laki! Watanikoma siku hiyo, sijui niwatafute alishababu nivae mabomuuu! Wananikeraaaa!
Wezi haooooooooooo weziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom