Mikasa ya Kupokea na Kutoa Rushwa

dog 1

JF-Expert Member
Nov 20, 2015
228
575
Wana jamvi wasalaam

Njooni hapa tupeane mazingira tatanishi ya rushwa tuliyowahi kukutana nayo, eidha kwenye kutoa rushwa au katika kupokea rushwa.

Mimi binafsi nilishawahi kupokea rushwa mara kadha, lakini sikumbuki kuwahi toa rushwa, labda shukurani tu baada ya huduma tena kwa hiari yangu mwenyewe.

Ngoja niwapee matukio kadhaa nilishayapitia yahusuyo rushwa. ifahamike kuwa nia sio kutukuza rushwa bali ni kuelezea mazingira halisi yanavyokuwa. Rushwa inabaki kuwa adui wa haki popote.

1. Nikiwa sina hili wala lile mara wanaibuka maDON wanipe mkwanja wa maana ili niwasaidie issue yao ktk ofisi niliyofanyia kazi. Mzigo ulikuwa wa maana kwa kipindi hicho, milioni Tano. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuahidiwa mzigo mrefu hivyo, kumbuka kipindi kile pesa ile unapata gx 100 (cresta) iliyosimama.

Nilikubali dili. Issue ikawa tunapeanaje huo mzigo. Jamaa wakasema niamue mwenyewe waniletee shehemu gani. Nikihofia kukamatishwa, nikawaambia nitamtuma mtu kesho yake asubuhi wamkabidhi huo mzigo, niliwapa description yake.

Nilimpata rafiki mmoja nikamtonya nina biashara na watu flan aende akachukue pesa yangu. Alikubali na mida ya saa tano asubuhi kaja na mzigo. Kwa uoga sikutaka kupokea pesa ile, nikamwambia twende tukaweke benki.

Tulifika benki ya NMB tukachoma ndani. Nilichukua deposit slip nikaanza kuzuga najaza ile form. Hapo jamaa hajui mpango wangu ukoje, anaamini ninaweka zile pesa kwenye akaunti. Wakati huo akili na macho yangu yapo kwenye upelelezi, kucheki kila anayeingia benkini. Ilichukua lisaa hadi jamaa akawa anauliza kulikoni?

Baada ya kujiridhisha kuwa hakuna chawa kaingia nikamwomba zile pesa, nikazihesabu zikatimia nikaziweka kwenye mfuko wa suti yangu nikasepa hadi nje ya benki na kumwacha jamaa yangu anashangaa tu. Nje nikachukua taxi hadi benki ya NBC nikaweka mkwanja kwenye akaunti yangu ya pembeni. Kumbuka sikutaka kuweka ile pesa NMB sababu akaunti ile ndo ilitumika kulipia mshahara wangu, so sikutaka any future suspicion. Kwenda NMB ilikuwa Geresha tu, kusafisha mazingira ili nisikamatike na Takukuru.

Baadae nilimwita jamaa angu, nikamtoa 20K ya asante.

2. Siku nyingine wehu wakajipendekeza na milioni mbili. Hapo nishakuwa mjanja eti... Nilikataa kupokea nikidai twende ofisini kwao, maana walikuwa ni watumishi wa kampuni fulani. Wakakubali. Safari hadi ofisi zao ikafanyika. Nilichukua ule mzigo ndani ya ofisi zao, nikasepa nao hadi kurasini kwenye mgahawa (pub) flan. Nikiwa njiani kwenye tax nilistua rafiki mmoja tukutane pale. Alipoibuka kakuta nakunywa malta guiness. Nikampa mchongo mzima, kauliza mzigo uko wapi? Huku nacheka nikamwambia achukue koti lililokuwa kwenye kiti cha meza iliyokuwa mbele yetu. Kuleta nikamwambia kagua, alivyoona mzigo hakuamini.... Matanuzi yakaanzia pale. Maji yalipokolea jamaa kaanza kunitania kuwa mimi ni muoga, eti nazugia malta huku mzigo nimeupaki mita kadhaa mbele yangu wakati mjini vibaka ni wengi.

3. Siku moja tajiri mmoja hapa bongo alikuwa na issue ofisini. Alitaka kazi ifanyike kama alivyotaka yeye. nikakubali nikijua sitakosa mtonyo. Bosi katoa kitita cha milioni kumi mjomba. Ebwana eeeeee! Mjini hapa huu mzigo niuweke wapi?

Kwanza sikuwa na wasi na huyu Don wa mjini nikiamini hawezi nichomesha wala hana huo mda. Nilichukua ule mzigo nikiwa ofisini. Alivyochomoka tu nikachezesha akili, jibu likaja siwezi toka nje na mzigo huo kwa vile ni mkubwa sana. Pia sijapata ona kuupeleka. Benki tulihofia kwa sababu monitoring.

Basi nikachezesha akili. Nikatazama juu darini. Nikaanza kucheka mwenyewe. Simple work. Jibu tayari. Nikafungua shehemu ya dari nikaweka ule mzigo, ambao kwa wakati huo ulikuwa umetoka benki, unanukia kipesa-pesa haswa. Mzuka wa kazi ukaisha. Nikatoka hadi town (posta mpya) nikazuga zuga kama nasoma magazeti. Mara nikanunua rasket (begi la mgongoni) nikarudi ofisini.

Mda wa kufunga ofisi ulifika. Hadi hapo washkaji wangu nikawa nawapotezea wasije nivurugia dili langu. Akili yote ilikuwa juu ya mwali wangu, 10M. Watumishi wote walipotoka mazingira ya ofisi nikachukua mkwanja wangu, milioni kumi, nikatia kwenye rasket. Nje ya ofisi nikaita boda boda ninayefahamiana naye, nikamwambia anipeleke home nimechoka sana na kazi.

Amini zile pesa niliziweka kwenye briefcase yangu chumbani kwangu, nikachomoa laki tano nikatoka nje, nikapigia washkaji kadhaa tukakutana kiwanja tukaanza kula bata.. kula bata.... kula bata.... yaanii kula bata hadi majogoo. Pesa ile sikuwahi kuipeleka benki. Niliitumia hadi ikaisha yote kwa kuchomoa kiduchu kiduchu. Wakati mzigo bado mnene nilikosaga sana amani. Kila nikiwaza naanza kuhofia mamilioni niliyoyaacha nyumbani. Basi full time nawaza habari za majambazi na nyumba kuungua moto

4. Basi bwana. Mfanyakazi mwenzangu aliwahi nipa mchongo wa milioni moja. Kwamba kuna jamaa zake wanahitaji msaada wangu ofisini, na kitengo changu ndio shehemu sahihi ya wao kupata misaada (feva). Sikuwa na imani naye sana japo alikuwa mshikaji wangu. Lakini pesa ile niliihitaji. Nikafikiri nikamwambia anikutanishe na hao watu wake jumamosi iliyofuata, siku ya wikendi.

Ilifika Jumamosi asubuhi jamaa kanipigia. Nikamwambia tukutane posta mpya saa tatu. Mimi nikasepa zangu hadi Buguruni. Alipopiga nikamwambia nimekwama waje Buguruni na mzigo. Saa tano ilipofika tukawa tumekutana wote kwenye pub moja pale Buguruni. Baada ya maelezo kadhaa nikaomba mkwanja wangu. Nilipoutia mfukoni tu mzuka ukapanda. Nikaagiza maji ya mende, na mashikaji wangu nilimwagizia as nilijua anatumia. Kama ujuavyo. Wanywaji hatubaguani. niliwaagizia hadi wale jamaa walionipa rushwa. Tulikunywa na kula hadi usiku.

Kurudi maskani nikapitia kwa kigrosary flan bata likaendelea. Katika hali ya utani jamaa zangu wananiambia siku hizi nimefulia. Basi nikatoka kitita cha laki nane au tisa hivi nikatupia mezani, wakabaki waaaaaaa. Nikawaambia maskini nyie pigeni gambe pesa ipo. Chenji iliyobaki najua mwenyewe.

Upi mkasa wako?
 
Unakaribia kuishilia ni dalili mbaya kutoa ya sirini mbele ya halaiki. Kumbuka jinai haiishi hata ipite miaka mingi kiasi gani. Badili mfumo wa maisha unadalili za kuugua magonjwa ya akili jaribu kuonana na wataalamu wa afya
 
Aiseee...Siku utakayo nasa nina nina imani
Utaandika uzi wako ukiwa jela.
 
Kweli jamaa haujui kula rushwa..principle ya kwanza usimuumize anaetoa hio rushwa igeuze kama unamsaidia atatoa kiroho safi kabisa..unakua hauna wasi wasi wa kuchomeshwa wala nini...😀😀😀
 
Kweli jamaa haujui kula rushwa..principle ya kwanza usimuumize anaetoa hio rushwa igeuze kama unamsaidia atatoa kiroho safi kabisa..unakua hauna wasi wasi wa kuchomeshwa wala nini...
Uko sawa. Lakini zipo zile za michongo, anakuja mtu na shida zake kumbe kaja kukukamatisha. Kamwe usimwamini mtu kwenye hii mambo. Hata ile asante tu inakukamatisha.
 
Duh, sijawahi toa wala kupokea rushwa au ndo sababu nahangaika kutafuta pesa kupita kiasi.!?

Lakini hapana moyo tulia.
Naamini rushwa umeshatoa, pengine bila kufahamu kuwa unatoa rusha. Kwenye kupokea ndo usiseme, unaweza mtu akakutoa lunch kumbe ndo rushwa yenyewe, wewe ukadhani ni mazungumzo tu.
 
Unakaribia kuishilia ni dalili mbaya kutoa ya sirini mbele ya halaiki. Kumbuka jinai haiishi hata ipite miaka mingi kiasi gani. Badili mfumo wa maisha unadalili za kuugua magonjwa ya akili jaribu kuonana na wataalamu wa afya
Karma imeshaanza kumuandama taratibu taratibu,ni swala la muda tu kila kitu kitakua wazi!!
 
Kweli jamaa haujui kula rushwa..principle ya kwanza usimuumize anaetoa hio rushwa igeuze kama unamsaidia atatoa kiroho safi kabisa..unakua hauna wasi wasi wa kuchomeshwa wala nini...
Rushwa ni Rushwa tu,hata uigeuze vp bado hiyo ni Rushwa tu!!
 
Back
Top Bottom