Nliamua kunywa sumu nikaokolewa kiajabu sana

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Nakumbuka siku hiyo nikiwa na miaka kama 12 hivi tukiwa Marekani mimi na familia yangu. Siku ilianza tu vibaya nikawa nimeamshwa na dada wa kazi saa 12:45 badala ya saa 1:00 (saa moja kamili) kweli nlikasirika sana. Sema tu yule dada wa kispaniola alikuwa mrembo sana ana shape hatari akaniomba msamaha. Nikaona nimsamehe tu maana angefukuzwa kazi mzee alikuwa hapendi ujinga kabisa.

Basi saa mbili nikawa nipo dinning naangalia angalia vyakula. Maana breakfast nayo ilikuwa ni buffet. Kulikuwa na vyakula vingi sana nakumbuka. Supu ya Papa, mayai ya mbuni ya kukaanga, n.k ilikuwa unachoka mwenyewe ule nini.

Mimi nikamuuliza yule Chief mbona hajaweka cassava. Nami nlikuwa nimesoma kwenye kitabu flani kuwa kuna jamii africa zinashindia tu mihogo. Sikuwa naifahamu kwa kweli. Nikamwambia nataka mihogo. Akaanza kujieleza pale nikaondoka.

Baadaye akaja yule housemaid toka Spain ndio alikuwa ananijulia hasira zangu. Wengine walikuwa wananiogopa sana akaja akaanza kunibembeleza nirudi dinning room. Nikarudi.

Ndio kumkuta mama akaanza kunisema kwanini nakuwa msumbufu. Akataka nichukuliwe chakula mbalimbali. Nikakataa kuwa sitaki cake, mayai, wala burger. Nataka tu cassava. Akawa mkali akataka nipewe na sausage kwenye sahani.

Nilikasirika sana. Nikaona mama ananilazimisha nile cake, mayai, burger na mavyakula vyakula mengine. Nikaondoka pale sebuleni. Nikaenda room....nililia sana kuona mama kama anaanza kunitesa. Nliwaza huyu ni mama yangu au nimebadilishiwa?

Nikaenda jikoni nikaanza kuchanganya sumu. Nikachukua asali nikaweka na maziwa kwenye kikombe, nikaweka na sijui mdollerseen nikachanganya nikanywa. Nikaenda room ya mdogo wangu nikalala ili nipitiwe na kifo nikiwa usingizini.

Nilikuja shtuliwa na yule housemaid wa kispaniola akinitaka sana nisamehe nikale some bites na drink za saa nne. Sisi huwa tunakula saa 2 ,4 ,8,10 na saa 12. Kisha saa 2 kunakuwa na vitu laini laini sana kama samaki au vyakula laini laini vingine.

Basi nadhani ndio yule sister aliniokoa nisife maana sijui ile sumu ingeniuaje. Nilihisi tu ilikuwa ndio sumu maana sisi kwetu mpaka leo hatujui sumu inakuaje. Hatujakulia mazingira ya kufahamu hivyo vitu. Huwa nawaza nasema je ningekufa ingekuaje? Maana hata experience yake sina.

Toka siku hiyo mama aliacha kutuingilia suala la kula akawa anawaachia madaktari washauri tuwe tunakula nini.
 
Screenshot_2022-12-28-08-29-34-750_com.android.chrome.jpg
 
Nakumbuka siku hiyo nikiwa na miaka kama 12 hivi tukiwa Marekani mimi na familia yangu. Siku ilianza tu vibaya nikawa nimeamshwa na dada wa kazi saa 12:45 badala ya saa 1:00 (saa moja kamili) kweli nlikasirika sana. Sema tu yule dada wa kispaniola alikuwa mrembo sana ana shape hatari akaniomba msamaha. Nikaona nimsamehe tu maana angefukuzwa kazi mzee alikuwa hapendi ujinga kabisa.

 
Back
Top Bottom