Njooni mnipe Muongozo wa kulea mapacha

Njooni mnipe Muongozo wa kulea mapacha

Mke wangu amejifungua waoto mapacha kwa sasa wana wiki 3.

Changamoto anayopitia ni.

1..watoto kulia sana na kutolala hasa wakati wa usiku kuanzia saa 7 hadi saa 11 ndo kuna kuwa na unafuu.

2.kuna mmoja aliyezaliwa na kilo chache yeye muda wote ni kulia sio asubuhi wala mchana,usiku.

3..Maziwa yanatoka ila yanamuuma sana.

Naombeni Muongozo shida inaweza kuwa ni nini wakuu!?
Mapacha ni baraka,jiandaeni kupiga hatua kubwa kimaendeleo mwaka huu sema amina
 
Mke wangu amejifungua waoto mapacha kwa sasa wana wiki 3.

Changamoto anayopitia ni.

1..watoto kulia sana na kutolala hasa wakati wa usiku kuanzia saa 7 hadi saa 11 ndo kuna kuwa na unafuu.

2.kuna mmoja aliyezaliwa na kilo chache yeye muda wote ni kulia sio asubuhi wala mchana,usiku.

3..Maziwa yanatoka ila yanamuuma sana.

Naombeni Muongozo shida inaweza kuwa ni nini wakuu!?
Mtafute mtaalamu na mshauri wa unyonyeshaji anapatikana Agakhan hosptal ila instagram yupo kwa jina la JJbreastfeeding alinisaidia sana

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu

Pole Sana na hongera pia!

Mama anywe uji uliochemshiwa na mbegu za maboga Ili maziwa yawe MENGI!zilizosagwa kama unga unga!

Wakati Mwingine azitafune!

Yale maji ya kuogea Watoto hayo ya vugu vugu tia chumvi kidogo ya mabonge ndani yake KWA utakaso na usiku uwaombee kama ni mkristo au dua kama muislamu!

Watoto wadogo HUWA anashambuliwa na pepo wabaya nyakati za usiku hasa mida ya saa sita Hadi tisa usiku!!hao ni wapya wanaowataka ni wengi Sana KWA malengo Yao!

Mengine soma comments za wadau!
 
Wewe! Tunawapaga uji watoto wasioshiba! Unaandaa uji unauchuja katika kitambaa unapata maji unamnywesha mtoto wa siku moja.
Wazungu wa Masaki washakwambia Mtoto anakosa mfumo wa afya ya akili, lol
Utadhani wakipewa huo uji hawanyonyi kwa Mama yao,

Mimi nina Mapacha sasa hivi ni vidada vya miaka 6,
Kwanza nilikua mdogo wakati najifungua, pili walizaliwa pre matured, tatu nilivyotoka hospital ilikua ni kulia kwa kupokezana, maziwa hayatoki mengi nakamua hadi nahisi natoa damu,
Maziwa ya Kopo waliyakataa ukiwawekea kwenye chuchu hawanyonyi, ukiwanywesha kwa kijiko wanatema, Nilikondaaaaaaaa

Mama alipokuja akawaanzishia uji, vilikua vinakunywa hadi vinalilia, vikishaoga ni kulala tu,

Sasa Mtu anakuja na hadithi za mnyonyeshe kwa miezi sita kama huna maziwa wafe kwa njaa!?
 
Wazungu wa Masaki washakwambia Mtoto anakosa mfumo afya wa akili, lol

Nashukuru, wengi wa hawa Vijana wa JF ni Watoto tu! Wasamehe bure! Kijana wangu mkubwa (37 years) alianza kupewa uji akiwa na siku moja, kwa vile mama yake Maziwa yalikuwa hayatoki.

Mpaka mtu apate shida ndipo hujifunza. Wengi hawajui kuwa mtoto kulialia sana ni njaa, ingawa inawezekana gesi etc.

Maziwa ya mama? Wengine wamenyonya maziwa ya Bibi zao mfano baada ya mama zao wazazi kufariki au Watoto wa IVF S26 inawahusu
 
Wazungu wa Masaki washakwambia Mtoto anakosa mfumo afya wa akili, lol
Utadhani wakipewa huo uji hawanyonyi kwa Mama yao,

Mimi nina Mapacha sasa hivi ni vidada vya miaka 6,
Kwanza nilikua mdogo wakati najifungua, pili walizaliwa pre matured, tatu nilivyotoka hospital ilikua ni kulia kwa kupokezana, maziwa hayatoki mengi nakamua hadi nahisi natoa damu,
Maziwa ya Kopo waliyakataa ukiwawekea kwenye chuchu hawanyonyi, ukiwanywesha kwa kijiko wanatema, Nilikondaaaaaaaa

Mama alipokuja akawaanzishia uji, vilikua vinakunywa hadi vinalilia, vikishaoga ni kulala tu,

Sasa Mtu anakuja na hadithi za mnyonyeshe kwa miezi sita kama huna maziwa wafe kwa njaa!?
pole na hongera kwa kukuza
 
Watu wengine bhana. Suala la mtoto kuja kuwa na akili kubwa ni kipawa tu cha M/Mungu anazaliwa nacho wala sio kunyonyweshwa miezi sita. Kama ingekua ni hivyo, basi watoto wote waliozaliwa kwenye mazingira magumu wasingekua wanafanikiwa shule.

Brother, kongole kwako kwa kuwa Baba wa mapacha. Hii miezi miwili ya mwanzo suala la kulia na kukesha haliepukiki, japo mara nyingi mtoto huwa halii bure. Kilio chake huwa ni ujumbe wa discomfort anayoipata sasa kazi kwako kujua shida ni nini na uitatue. Kama changamoto ni maziwa fuata ushauri uliotolewa na wadau huko juu kuhusu namna ya kumuongezea maziwa mama na kununua maziwa ya ziada. Kuhusu kuchoka, ni kweli unahitaji msaidizi ili mama awe anapumzika kidogo.

Kuhusu uji nashauri kama inawezekana walau wamalize hata miezi miwili kwanza ya maziwa tu peke yake then ndio uanze kuwapa kidogo kidogo ili mama apumue kidogo kwenye kunyonyesha. From there, utajiongeza na vitu vingine kama kuchemsha ndizi na kui blend na maziwa then unaichuja (unatoa zile solids) unawapa mdogo mdogo mpaka wanazoea.

NB:
1. Chochote utakachompa mtoto, make sure hapewi juice ya aina yoyote kwa kipindi chote anachonyonya.

2. Mjitahidi kadri muwewezavyo kumuangalia/shika/beba mtoto vizuri asije akaanguka.

Ukizingatia hayo mawili hapo juu yatakuepusha na matatizo mengi sana!

Kila la Kheri.
Umemaliza yote naongezea na kipengele cha joto,
Unakuta Mtu yupo Dar anamfunika mtoto kwa nguo nzito na kofia mbili mbili bado madirisha yamefungwa kwa vioo, mtoto ana sweat, basi ni kulia tu,

Wazazi tujitahidi kuendana na mazingira yetu, mazingira ya Dar si sawa na Mazingira ya Makambako.
 
Mke wangu amejifungua waoto mapacha kwa sasa wana wiki 3.

Changamoto anayopitia ni.

1..watoto kulia sana na kutolala hasa wakati wa usiku kuanzia saa 7 hadi saa 11 ndo kuna kuwa na unafuu.

2.kuna mmoja aliyezaliwa na kilo chache yeye muda wote ni kulia sio asubuhi wala mchana,usiku.

3..Maziwa yanatoka ila yanamuuma sana.

Naombeni Muongozo shida inaweza kuwa ni nini wakuu!?
Mimi pia pacha Mwenzangu wa kike ameshafariki zamani. Ninakupongeza kuniletea mapacha wenzangu je watoto wako wote ni wa kiume au wakike mapacha wenzangu? ninakusaidia swali lako la kwanza kulia mtoto kuanzia saa 7 mpaka alfajiri saa 11 kuna sababishwa wewe unapo ishi katika hiyo kuna wachawi wanaokuja usiku kuwatembelea watoto wako na kuingia ndani ya nyumba sas watoto wanawaona hao wachawi. Tumia njia hii ya kuwafanya watoto wasilie usiku mwingi kwanza kabisa usiwalaze watoto kwenye kiza kwani kiza kinasababisha watoto wpige makelele kwani wanainamiwa na mashetani usingizini na wachawi wanakuja kuwachezea watoto wako usiku. washa japo taa yenye muangaza hafifu karibu na watoto ili wasilale kwenye kiza. Jambo la pili waweke watoto chini ya mto wa kulalia kitunguu saumu japo punje 1 mkaa mkaa wa kuokota njiani, mvuje na kisu kisicho kuwa na mpini kila mmoja wao hao watoto wawekee hivyo vyote funga katika kitambaa cheusi cha kuokota njiani. Utakuja kunishukuru. NA Swali la 3 kama maziwa yanatoka kido mnunulie mke wako dawa moja inaitwa Uwatu upate ya unga dawa hiyo inauzwa katika maduka ya dawa za asili utakuwa ukimpigia uji anaweka kijiko 1 cha unga wa uwatu anakunywa kila mara anapo kunywa huo uji awe anatia huo unga wa uwatu kijiko 1 maziwa yake yatatoka kwa wingi sana.
Na kuhusu tiba ya wachawi wasiweze kuja usiku nitafute kwa wakati wako ili nikupe dawa ya kuwazuia wachawi wasiweze kuja kwako usiku .

SABABU ZINGINE ZA KITAALAM MTOTO KULIA USIKU MWINGI:
SABABU ZA MTOTO MCHANGA KULIA SANA NYAKATI ZA USIKU HIZI HAPA!

Kwa mzazi yeyote anaelewa usumbufu unaotokana na mtoto anaelia. Watoto wachanga wenye umri chini yua miezi 6 wanakuwa na matatizo haya zaidi.
Mtoto anapolia huwa inaleta hisia kuwa mtoto anashida na mara nyingi wazazi au walezi wanakuwa hawajui sababu au hata wakijua huenda wasijue jinsi ya kurekebisha tatizo na kumnyamazisha mtoto.
Ifahamike kwamba kulia ndio njia pekee ambayo mtoto anaitumia kuwasiliana na wengine juu ya shida ambayo anayo. Ni ujumbe kwa mzazi au mlezi kuwa hajisikii vizuri na anahitaji msaada.
Kwanini mtoto mchanga huwa analia? Soma sababu sita kubwa zinazomfamnya mtoto mchanga kulia na mbinu za kumnyamazisha. Namba sita ni muhimu kuijua kwa undani kwakuwa ndiyo inayosumbua wengi zaidi.
Sababu 6 Kubwa za Mtoto Mchanga Kulia

1. Njaa
Mtoto akiwa na njaa na anahitaji chakula anaweza kulia ili kutaka shida yake itatuliwe. Lakini kwa bahati mbaya hana namna ya kukujulisha kuwa ana njaa zaidi ya kilio. Ni vyema kufahamu aina ya sauti ya kilio inayoashiria njaa. utajua hili kwa mazoea yako ya kila siku na mtoto wako. Njaa ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa ya mtoto mchanga kulia.
Njia ya Kukabiri Tatizo:
Mpe mtoto chakula kila mara kutokana na ulivyompangia. Kumbuka mtoto anakula kidogo na mara kwa mara.
Kama mtoto anaendelea kulia baada ya kula au anakataa chakula basi kutakuwa na sababu nyingine

2. Joto au Baridi
Kama ilivyo kwa watu wazima,joto kali kupita kiasi au baridi inakufanya ujisikie vibaya na kutafuta jinsi ya kurekebisha kama vile kuvaa vazi zito kama kuna baridi au kuwasha feni au kiyoyozi,vivyo hivyo kwa mtoto mchanga, anahitaji kupata ubaridi kama kuna joto kali au kuvikwa nguo nzito ili apate joto kama kuna baridi
Njia ya Kukabiri Tatizo:
Hakikisha mtoto anavaa nguo sahihi kulingana na hali ya hewa. Mpunguzie nguo au kufungua madirisha kama kuna hali ya joto.
Kama kuna baridi basi hakikisha unamvikanguo nzito mwilini ikiwemo miguuni na kichwani.

3. Uchovu na Usingizi
Watoto wanalia wakiwa na usingizi. Hii inatokea mara nyingi sana. Watoto wengi wana tabia ya kulia kabla ya kulala.
Njia ya Kukabiri Tatizo:
Fahamu kuwa mtoto anahitaji kulala muda mwingi sana inakadiriwa kuwa masaa yapatayo
Mtoto wa miezi 1-3: Masaa 15 (Mchana-5,Usiku-10)
Mtoto wa miezi 3-6: Masaa 14 (Mchana-4,Usiku-10)
Mtoto wa miezi 6-13: Masaa 12-14 (Mchana-3,Usiku-11)
Kama ukifahamu mtoto analia kwasababu ya usingizi au uchovu basi muogeshe na kumweka katika mazingira ya kulala(kumlaza mtoto)
Watoto wengine wanalala vizuri wakiwa wameshikwa mikononi na kuchezeshwa badala ya kitandani.

4. Kubebwa na Kukumbatiwa
Watoto wanahitaji kubebwa na kukumbatiwa. Hii ni njia yaasili ya kunesha upendo kwa binadamu huyu mdogo.
Njia ya Kukabiri Tatizo:
Mtoto anapokuwa amelazwa kwa muda mrefu huwa anachoka na anahitaji kumbadirisha namna ya kulala napengine kubebwa mikononi na kukumbatiwa. Sauti ya mapigo ya moyo ukimbeba kifuani kwako inamfanya ajisikie vizuri na kujiona anajaliwa.

5. Kubadirishwa Nepi
Mtoto anapojisaidia katika nguo zake anajisikia vibaya na kukosa uhuru.
Anahitaji kubadirishwa nepi,kuoshwa na kuvikwa upya
Mtoto akilia fikiria huenda amejisaidia na anahitaji kubadirisha nepi
Njia ya Kukabiri Tatizo:
Mwangalie mtoto mara kwa mara kama amejisaidia na mbadirishe nepi zilizochafuka. Nepi zenhye mkojo au haja kubwa zinaweza kumsababishia mtoto kuungua ngozi hivyo ziondolewe kwa haraka.

6. Ugonjwa wa Tumbo na Maumivu Mengine
Watoto wachanga wanasumbuliwa sana na maumivu ya tumbo na wataalamu wanasema kuwa inaweza kusababishwa na chakula ambacho katika umri mchanga ni mziwa ya mama au maziwa ya bandia ambayo anapewa.
Kwakuwa mfumo wake wa chakula bado ni mpya na unaendelea kukua basi unapata shida kumeng’enya chakula.
Inaaminika kuwa gesi inajaza tumbo na kusababisha maumivu kwa mtoto.
Njia ya Kukabiri Tatizo:
Shida hii si rahisi kukabiliana nayo na imekuwa ikiwapa wakati mgumu wazazi kwa watoto chini ya miezi 3.
Kumlaza mtoto kifudifudi iliatoe upepo ni njia mojawapo inayoshauriwa lakini katika usimamizi(Ni hatari kumlaza mtoto mchanga kifudifudi kwa kuwa anaweza akajiziba hewa na kusababisha kifo).
Kumshikashika tumbo kwa mikono au kitambaa chenye maji ya uvuguvugu inaweza ikasaidia kumtuliza.
Kuna dawa za kusaidia kulainisha utumbo wa mtoto na kutoa gesi. Tafadhari onana na daktari wa watoto upate ushauri zaidi.

Mwisho..
Mtoto anaelia anahitaji msaada na anatoa mawasiliano kuwa ana shida. Kwakuwa hawezi kusema wala kuonesha ni nini unahitaji kuangalia mambo yote ya msingi kama yalivyotajwa ilikujua anasumbuliwa na nini.
Ugonjwa tumbo unachangamoto kubwa zaidi kukabiliana nao na kwa kweli unawasumbua watoto wengi na wazazi pia kwa kuwa hakuna kikubwa ambacho uaweza kufanya kuondoa maumivu kwa mtoto wako. Hata hivyo bado mbinu zilizotajwa zinaweza kusaidia kukabiriana na matatizo yanayosababisha mtoto mchanga kulia.

MTOTO  KULIA USIKU.jpg
 
Dream Queen unamuona huyu! Ndiyo wale ulokuwa unawazungumzia. Yeye anaongelea nadharia sie tunaongelea uzoefu maana mapacha wako walokunywa uji wana miaka 6 na wapo wanadunda. Wakwangu ni mbaba. Tuwape pole tu
Kila mtu abaki na anachoamini...wamama wengi hawana elimu sana kuhusu unyonyeshaji...mimi too nna twins!kila mtu abaki na analoamini
 
Kila mtu abaki na anachoamini...wamama wengi hawana elimu sana kuhusu unyonyeshaji...mimi too nna twins!kila mtu abaki na analoamini
Wanakaza kubisha wakati ulichozungumza uko sahihi hasa hapo kwenye elimu.. mama akila vizuri maziwa yanatoka mengi tu na km mtu hana uwezo ni heri mziwa ya ng'ombe kuliko uji.
 
Wanakaza kubisha wakati ulichozungumza uko sahihi hasa hapo kwenye elimu.. mama akila vizuri maziwa yanatoka mengi tu na km mtu hana uwezo ni heri mziwa ya ng'ombe kuliko uji.
Maziwa ya Ng'ombe kwa mtoto mchanga[emoji15]
Lol, hebu nenda kwanza kajipe elimu wewe ndio uje utoe kwa wengine
 
Dream Queen unamuona huyu! Ndiyo wale ulokuwa unawazungumzia. Yeye anaongelea nadharia sie tunaongelea uzoefu maana mapacha wako walokunywa uji wana miaka 6 na wapo wanadunda. Wakwangu ni mbaba. Tuwape pole tu
Clinic ndivyo wanavyowaambia hata maji hadi wafike miezi 6, halafu hao manesi watoto wao wanawapa maji [emoji3], za kuambiwa unachanganya na zako.
 
Back
Top Bottom