Njoo Kenya uone Mlima Kilimanjaro, kuna kosa gani?

Pius J. Kiwarya Lema

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
1,097
566
NJOO KENYA UONE MLIMA KILIMANJARO ina kosa gani ????

Niliwahi kufanya kautafiti kadogomwaka juzi kuhusiana Nchi ya Kenyakudaiwa kufanya utalii wa Kimataifawakidai Mlima Kilimanjaro uko Kenya,

Nilishawishika kufanya hivyo Baada ya kumsikia Rais Jakaya kikwete àkidai Sisi Tanzania tunapenda kula pasipo kuliwa

Namnukuu ,Wizara wanàniambia pale CNN tangazo moja ni dolami milion ngapi sijui 'wananiambia kurusha kwa sekunde ni gharama mno!

Nimewaambia muanze kutangaza kidogokidogo usiogope gharama ,Ukitaka kula lazima uliwe kwanza!

Mwisho wa nukuu

Nilipohoji kuhusu madai ya Kenya kudai Mlima Kilimanjaro uko Kenya nikagundua ni Uongo mtupu!

Ni MANENO ya watu walioshindwawajibu wao kwanMiaka 50 wanatafuta kisingizio. Kama ingekuwa ni Kweli pangekuwepoNa Mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi zetu mbili!

Lakini haupo kwa sababu Wakenya ni wazalendo na wametuzidi Ujanja wa kibiashara katika kuchukua fursa zinazoshangaza za kutangaza utalii.

Nakumbuka mmoja wa wahojiwa wangu ambaye àlidai kufika Zambia Na kukuta Kipeperushi cha Wakenya pale uwanja wa ndege alinifungua macho Akisema.

''Sio kweli kwamba wakenya wanasema mlima Kilimanjaro Uko kwao, Bali kipeperushi kimeandikwa: NJOO KENYA UONE MLIMA Kilimanjaro!

Ahahahh bao la mkono!

Je mtu akija Kenya atauona Mlima Kilimanjaro? Jibu ni Ndiyo, tena unaonekana vizuri mno mno!

Je, kuna kosa gani hapo? Kwahiyo hata linapoibuka hili la Olduvai ni sehemu ya tatizo lile lile la wizara ya Maliasili na serikali ile ile ya chama kile kile,
na watu wale wale, wakifanya Yale Yale, kwa njia zile zile!

Kukwepa wajibu na kusingizia tunaibiwa eti wajieleze! Tutaendelea kuwaambia wakenya wajieleze wakati wameshakupita!

Kwa Maoni yangu Nashauri tuache kulumbana Nao tujibu Mapigo kwa kutangaza utalii kimkakati kama wao!

Ni wakati wa Mabadililko!

Tumieni hii kauli Mbiu Nimeshaisajili: SHUKA KILIMANJARO UONE MLIMA VIZURI.

Kiwaryalema
 
Ilibidi wageni wote wanaokuja kwa utalii Tz destination iwe Dar,Mwanza,Mbeya au KIA hakuna cha Namanga na Dada zake.sasa hii ya kupanga magari JOMO itakula kwetu any way watu wa kaskazini ni wahujumu wakuu wa utalii Tanzania.
 
Weka ushahidi...Wakaskazini wamehujumu vipi utalii..
 
Ilibidi wageni wote wanaokuja kwa utalii Tz destination iwe Dar,Mwanza,Mbeya au KIA hakuna cha Namanga na Dada zake.sasa hii ya kupanga magari JOMO itakula kwetu any way watu wa kaskazini ni wahujumu wakuu wa utalii Tanzania.
Inawashinda nini watu wa Marketing nao kujibu mapigo "Njoo Tanzania,Upande Mlima Kilimanjaro"? Si ubunifu na fitna ya kimatangazo tu?
 
Umezaliwa lini, au unadhani ukisema umefanya "tafiti" utafanya uongo uwe ukweli? Huyo aliyesema kwenye video kuhusu olduvai gorge utafiti wako unasemaje?
 
Mimi nafikiri tunatakiwa kuwashukuru Kenya kwa kutusaidia kutangaza vivutio vyetu vya utalii badala ya kulalamika.
 
Kitu ambacho viongozi wetu ama hawakijui au hawwtaki kukifanyia KAzi ni kwamba
Kenya wamejenga hotel Na miundo mbinu ya kuvutia sio ajabu wakabadilisha hata jina LA barabara Na kiita Kuelekea Kilimanjaro ,, wanateengeneza mazingira ya watalii kushukia Na

kupanda ndege Kyle kule Kenya huku wanaletwa Na coaster tu
 
ukiwa upande wa kenya mlima kilimanjaro unapendeza zaidi.
Niliwahi kupita maeneo ya mbuga za Amboseli nation park zilizoko upande wa Kenya zipo karibu kabisa na mpaka miteremko ya mlima kilimanjaro inayoishia upande wa kenya kuna mji ulioko pembezoni mwa mlima unaitwa Leitoktok na Kimana

ki ukweli mandhari ya mlima inaonekana vizuri ukiwa maeneo ya mbuga za amboseli national park na kwa kupiga picha inapendeza zaidi huku kukiwa na wanyama live pembeni kama simba twiga swala n.k
Kwa bahati za kijiografia sisi tuna mlima na wao wana mbuga za wanyama ambapo wanyama kwa kawaida hawaingii upande wa Tanzania ingawa ardhi haina kizuizi cha kijiografia kuwazuia wasiingie upande wetu

Wakenya hutumia fursa hizo vyema kujitangaza kitalii kuliko sisi. kwetu watalii huja kuupanda tu mlima
 
Hata kwenye mlango wa KQ wameandika tu Mlima Kilimanjaro. Na hata ndani ya ndege yao wanakupa maji ya Kilimanjaro lakini sio ya bwana Mengi.
Hawa watu wanatumia ujanja sana kutumeza katika Utalii wetu. Wanapita katika njia za South Africa wanavyowafanyia Zimbabwe.
Lazima TTB iamke kwenye usingizi wake wa kuona watalii watakuja tu.

Ova
 
Ni ukweli kuwa ukifika Kenya unaweza kuuona mlima Kilimanjaro. Wangesema njoo Kenya upande mlima Kilimanjaro hapo wangekuwa wanadanganya.
 
NJOO KENYA UONE MLIMA KILIMANJARO ina kosa gani ????

Niliwahi kufanya kautafiti kadogomwaka juzi kuhusiana Nchi ya Kenyakudaiwa kufanya utalii wa Kimataifawakidai Mlima Kilimanjaro uko Kenya,

Nilishawishika kufanya hivyo Baada ya kumsikia Rais Jakaya kikwete àkidai Sisi Tanzania tunapenda kula pasipo kuliwa

Namnukuu ,Wizara wanàniambia pale CNN tangazo moja ni dolami milion ngapi sijui 'wananiambia kurusha kwa sekunde ni gharama mno!

Nimewaambia muanze kutangaza kidogokidogo usiogope gharama ,Ukitaka kula lazima uliwe kwanza!

Mwisho wa nukuu

Nilipohoji kuhusu madai ya Kenya kudai Mlima Kilimanjaro uko Kenya nikagundua ni Uongo mtupu!

Ni MANENO ya watu walioshindwawajibu wao kwanMiaka 50 wanatafuta kisingizio. Kama ingekuwa ni Kweli pangekuwepoNa Mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi zetu mbili!

Lakini haupo kwa sababu Wakenya ni wazalendo na wametuzidi Ujanja wa kibiashara katika kuchukua fursa zinazoshangaza za kutangaza utalii.

Nakumbuka mmoja wa wahojiwa wangu ambaye àlidai kufika Zambia Na kukuta Kipeperushi cha Wakenya pale uwanja wa ndege alinifungua macho Akisema.

''Sio kweli kwamba wakenya wanasema mlima Kilimanjaro Uko kwao, Bali kipeperushi kimeandikwa: NJOO KENYA UONE MLIMA Kilimanjaro!

Ahahahh bao la mkono!

Je mtu akija Kenya atauona Mlima Kilimanjaro? Jibu ni Ndiyo, tena unaonekana vizuri mno mno!

Je, kuna kosa gani hapo? Kwahiyo hata linapoibuka hili la Olduvai ni sehemu ya tatizo lile lile la wizara ya Maliasili na serikali ile ile ya chama kile kile,
na watu wale wale, wakifanya Yale Yale, kwa njia zile zile!

Kukwepa wajibu na kusingizia tunaibiwa eti wajieleze! Tutaendelea kuwaambia wakenya wajieleze wakati wameshakupita!

Kwa Maoni yangu Nashauri tuache kulumbana Nao tujibu Mapigo kwa kutangaza utalii kimkakati kama wao!

Ni wakati wa Mabadililko!

Tumieni hii kauli Mbiu Nimeshaisajili: SHUKA KILIMANJARO UONE MLIMA VIZURI.

Kiwaryalema

Shuka Kilimanjaro uone mlima vizuri..... a good marketing slogan! sasa ndege zipi zinazokuja directly Kilimanjaro from Europe zaidi ya KLM? Tutake tusitake tutaendelea na malalamiko haya mpaka pale tutakapokuwa na shirika la ndege reliable linalofanya safari directly kuja Tanzania. Swali langu mpaka leo ni kwa nini watu wa TANAPA, Ngorongoro Conservation Authority wasi- team na kununua hata ndege mbili za kuanzia? of course management ya airline inabidi iwe hired
 
Inawashinda nini watu wa Marketing nao kujibu mapigo "Njoo Tanzania,Upande Mlima Kilimanjaro"? Si ubunifu na fitna ya kimatangazo tu?
Mkuu sidhani kama hao wapo hapa, Kenya tutahangaika sana nao na hapo shirikisho halijaanza kazi tunayo.Ubunishi na utashi vimetushinda watu ndio kwanza wako bize kukandamiza demokrasia katika chaguzi za mamea huko ndio tunaweza.Wakenya wanakuja hapa wanapewa vibali vya kufanya kazi na wapo wengi mno,jiulize ni watanzania wangapi wapo Kenya nawafanya kazi za maana huko.
 
Hata kwenye mlango wa KQ wameandika tu Mlima Kilimanjaro. Na hata ndani ya ndege yao wanakupa maji ya Kilimanjaro lakini sio ya bwana Mengi.
Hawa watu wanatumia ujanja sana kutumeza katika Utalii wetu. Wanapita katika njia za South Africa wanavyowafanyia Zimbabwe.
Lazima TTB iamke kwenye usingizi wake wa kuona watalii watakuja tu.

Ova
Mkuu yale maji ni ya mengi usibishe
 
Tumelala sana,kama si wakenya kutusaidia kuutangazia ulimwengu kuhusu Olduvai Geoge nani angepajua,sisi tushukuru la muhimu ni kuweka mirija wakishuka Kenya si bado watalipa entrance fee????
 
Shuka Kilimanjaro uone mlima vizuri..... a good marketing slogan! sasa ndege zipi zinazokuja directly Kilimanjaro from Europe zaidi ya KLM? Tutake tusitake tutaendelea na malalamiko haya mpaka pale tutakapokuwa na shirika la ndege reliable linalofanya safari directly kuja Tanzania. Swali langu mpaka leo ni kwa nini watu wa TANAPA, Ngorongoro Conservation Authority wasi- team na kununua hata ndege mbili za kuanzia? of course management ya airline inabidi iwe hired
Hili LA Kuwa Na Ndege zetu
ni moja ya suluhisho LA kudumu
Ambazo zingetumika kufanyia /kuvutia wateja Nimelikubali !

By kiwarya Lema
 
ukiwa upande wa kenya mlima kilimanjaro unapendeza zaidi.
Labda hujazungukia huku
1363180734_1!!-!!ViewofKilifromthelodge.jpg

plains_below_kilimanjaro_1280x10241.jpg

Huu ni upande wa Tanzania.
 
Tumelala sana,kama si wakenya kutusaidia kuutangazia ulimwengu kuhusu Olduvai Geoge nani angepajua,sisi tushukuru la muhimu ni kuweka mirija wakishuka Kenya si bado watalipa entrance fee????
Mbona Dr.Leak alishatangaza sana hiyo Olduvai wakati amegundua fuvu la binadamu aliyeishi miaka mingi iliyopita! Kila msomi duniani alifahamu kuwa hiyo Olduvai ipo Tanzania kutokana na ugunduzi huo!
 
Back
Top Bottom