PENDEKEZO: Mlima Kilimanjaro uitwe mlima Tanzania

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Imekuwa ni kawaida kwa wakenya kutangaza kuwa mlima Kilimanjaro uko Kenya. Mlima Kilimanjaro ndiyo mlima mrefu kuliko yote barani Afrika ukiwa na urefu wa Mita 5,895 kutoka usawa was bahari.

Imekuwa ni kawaida ukisafiri na Kenya Airways, mnapopita kwenye anga la mlima huu lazima rubani atangaze kuwa abiria mnaweza kuuona mlima huu vizuri lakini kwa kuvutia watu wasiojua waamini kuwa mlima huo uko Kenya. "Now we are in the Land of Kenya" alisikika rubani wa ndege leo wakati tukisafiri kutoka Dar kwenda Nairobi leo asubuhi. Akasema kushoto kwetu mnaweza kuona mlima Kilimanaro, mlima mrefu kuliko yote barani Afrika " a beautiful mountain Kilimanjaro". Akaongeza muda mfupi ujao tutatua katika uwanja wa ndege wa Jommo Kenyata International Airport lakini pia utaona Hifadhi ya taifa ya Nairobi.

Mbwembwe zote hizo za rubani ni katika kuwafanya watu wasiojua waamini kuwa mlima Kilimanjaro uko Kenya. Propaganda hizi za kibiashara na kuvutia watalii zimekuwepo kwa miaka mingi, wakenya wakisema njoo Kenya uone mlima Kilimanjaro.

Nadhani sasa tufikirie nje ya box, njia nyingine ya kuufanya mlima huu ujulikane na kila mtu kwamba uko Tanzania. Tubadili jina la mlima huu na kuuita Mlima Tanzania. Nadhani hapo tutakuwa tumemaliza ubishi wa muda mrefu kwa wakenya wanaotaka watu waamini kuwa mlima Kilimanjaro uko Kenya.

Ni mawazo yangu tu, naomba kuwasilisha kwenu wadau wa Maliasili na Utalii.
 
Yeah, sisi tuchukue mlima Tanzania na wao wabaki na mlima Kilimanjaro.
 
Mkuu kutengeneza jina (brand)na ikawa maarufu sio kitu rahisi..
 
Watalii wa kizungu wanaujua mlima Kilimanjaro kuliko unavyofikiri, specially mountain climbing enthusiasts. Zaidi ya hilo, tunajua umepanda Kenya Airways kwenda Nairobi.
 
Ndege zote zinazoingia nchini na kutoka, zikipita chini ya MLIMA WA KILIMANJARO huwa zina wa alert abiria, iwe ni Swissair, Ethiopean Airways, Lufthansa, n.k, KLM wameenda mbali zaidi na kuita ndege yao MT. KILIMANJARO.
Hii ni nzuri sana kwetu.
Wakenya kwishney habari yao wamekula vibaya 50 yao upepo umegeuka
 
Mi ningependa tubadili jina na kuuita Mt Sizonje nadhani ungevutia zaidi watalii
 
Bora uitwe mlima Tanganyika. Sioni Muungano ukidumu hadi JPM amalize muda wake. Kuna sehemu atawakoroga CCM Zanzibar na huo utakuwa mwisho wake na Muungano.
 
Uitwe 'mtulia' kwa sababu ndo kipaumbele kikubwa cha mkulu
 
Kila kitu kina chanzo chake! hilo jina halikuja from no where! Inapendeza zaidi kutumia jina la asili hata vizazi vijavyo vijue historia yake
 
Jambo lililorahisi ni kuuhamisha mlima upelekwe Dodoma tu, huko kubadili jina hakutasaidia
 
Back
Top Bottom