Makamu wa Rais Kenya akiri nchi yake kufaidi Mlima Kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamu wa Rais Kenya akiri nchi yake kufaidi Mlima Kilimanjaro

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by BAK, May 17, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Date::5/16/2009
  Makamu wa Rais Kenya akiri nchi yake kufaidi Mlima Kilimanjaro

  Na Leon Bahati

  Mwananchi

  MAKAMU wa Rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka amekiri kuwa mlima Kilimanjaro umekuwa ukiisaidia nchi yake kukuza sekta ya utalii kutokana na Wakenya wengi kuutumia katika kujitangaza hasa wawapo kwenye nchi za ulaya.

  Pamoja na kufaidika huko, alisema kuwa hiyo haifuti ukweli kwamba mlima huo mrefu kuliko yote Afrika, upo Tanzania, ingawa pia huweza kuonekana kutokea Kenya.

  Musyoka alisema hayo kwenye hafla fupi ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Ali Mohamed Shein.

  "Wakenya wanapoenda Ulaya wanawaambia wazungu: Njooni Kenya ili muone mlima Kilimanjaro," alisema Musyoka katika ziara hiyo ya kiserikali kwa mwaliko wa Tanzania.

  Kauli hiyo ya Musyoka imethibitisha malalamiko ya siku nyingi kuwa Tanzania imeshindwa kuvitangaza vivutio vyake vya utalii, na fursa hiyo kutumiwa na majirani zao wa Kenya na kuufanya ulimwengu udhani mlima huo uko nchini humo.


  Lakini, Musyoka hakusita kueleza kuwa jambo hilo limekuwa likizua ubishi kati ya wananchi wa pande zote mbili, lakini akasisitiza kuwa halivunji uhusiano wa karibu ambao umeasisiwa na viongozi wa pande zote.

  "Huwa tunabishana hivyo… Lakini ukweli tunajua (Mlima Kilimanjaro) upo Tanzania," aliweka wazi Musyoka ambaye katika hotuba yake alisisitiza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Kenya na Tanzania ambayo yana faida kwa pande zote.

  Kwa mara nyingine, Musyoka aliwahakikishia Watanzania kuwa serikali ya Kenya haina mpango wa kuweka shinikizo la kuhamisha Makao Makuu ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kutoka Arusha.

  Kwa mujibu wa kiongozi huyo msimamo wa serikali ya Kenya ni kwamba Arusha itaendelea kuwa makao makuu ya EAC hasa ikizingatiwa kuwa imepewa heshima hiyo na viongozi waasisi.

  Akizungumzia nafasi ya nchi hizo mbili kufaidika kiuchumi na Jumuia hiyo, Musyoka alisema zote zinajivunia kuwa na idadi kubwa ya watu, hivyo kujihakikishia kuwa na soko kubwa la kibiashara.

  Tanzania ina zaidi ya watu milioni 40 na Kenya inaifuatia kwa karibu. Nchi nyingine za Afrika Mashariki ni Uganda, Burundi na Rwanda.

  Naye, Dk Shein aliisifu Kenya kwa kuwa nchi ya pili baada ya Uingereza kuwekeza Tanzania na sasa mitaji yao imefikia dola za Marekani 1,284.7 milioni.

  Dk Shein aliainisha fedha hizo kuwekezwa kwenye miradi 374 kwenye sekta za kilimo, ujenzi, fedha na katika maendeleo ya rasilimali watu.

  Mbali na kuifaidisha Tanzania kutokana na kodi mbalimbali wanazotoa serikalini, Dk Shein alisema kuwa miradi hiyo imetoa ajira kwa Watanzania 41,560.

  Alifafanua zaidi kuwa biashara kati ya nchi hizo mbili imekuwa kwa kiwango kikubwa na kwamba imekuzwa zaidi baada ya kuundwa kwa Umoja wa Forodha wa Jumuia ya Afrika Mashariki tangu mwaka 2005.

  Alitoa mfano kuwa kiwango cha biashara ya bidhaa katika nchi hizo mbili kimepanda kutoka dola za Marekani 117.7 milioni, mwaka 2005 hadi kufikia dola 214.2 mwaka 2007.

  Pamoja na mazingira hayo mazuri, Dk Shein alibainisha kuwa Kenya ndiyo imekuwa ikifaidika zaidi kwenye biashara hizo.

  "Biashara kati ya Tanzania na Kenya kila mara imeendelea kuongezeka, ingawa Kenya ndiyo inayofaidika zaidi," alisema Dk Shein.

  Kwa kutambua mazingira hayo, Musyoka alisema Watanzania wana nafasi nao kufaidika kwenye ushirikiano huo wa kibiashara kwa kujitokeza kwa wingi kuwekeza nchini Kenya.

  Alitoa mwaliko wa Dk Shein kuitembelea Kenya katika siku chache zijazo, akiwa na wafanyabiashara wa Tanzania ambao wako tayari kuwekeza nchini humo.

  Alisema kuwa Wakenya watawapokea kwa mikono miwili hasa kwa kuzingatia kuwa Watanzania ni wakarimu na wenye roho ya kiutu.

  Katika kuthibitisha hilo alisema kuwa Watanzania hata wanapoenda kununua kitu, hutumia lugha ya kiuungwana ya kutumia neno ‘naomba' jambo ambalo kwa Wakenya hulitumia tu pale mtu anapotaka apewe kitu bila malipo.

  Kuhusu amani nchini Kenya, alisema kwa sasa kuna utulivu wa hali ya juu huku akisema kuwa ni matunda yaliyotokana na juhudi za Rais Jakaya Kikwete.

  Alikiri kuwa baada ya uchaguzi mkuu uliopita, Wakenya walianza kuuana kwa silaha za jadi, lakini juhudi za siku mbili za Rais Kikwete ziliweza kuwarejesha kwenye amani.

  Alisema kwa sasa Kenya kuna amani baada ya kuundwa kwa serikali ya mseto inayoshirikisha pande zilizokuwa zinahasimiana.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hivi ni miradi ipi Kenya wamewekeza Tz?
   
 3. G

  Giroy Member

  #3
  May 17, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mojawapo ni tanelec arusha.
   
 4. Y

  YesSir Senior Member

  #4
  May 17, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  What is the big deal sasa. Na nyie si muutangaze watu waje..
   
 5. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Tunaanza na WEWE (Yessir) anza kuutangaza mimi nautangaza sana hasa nikienda nje ya nchi yetu. Au wewe si Mtanzania!!!
   
 6. Y

  YesSir Senior Member

  #6
  May 17, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ni mtanzania na nautangaza sana. ninachochukia ni kitu cha watanzania kukaa chini na kuanza kulalamika. tourism is a competition. an average family can probably afford one holiday per year. there are over 1000 destinations, every country is doing all that they can to attract more crowds. if that is how kenya goes about,then we might as well find means topromote ourselves too. after all its not as though kenya is going around saying mt kilimanjaro is not in tanzania, they use mt kilimanjaro name to attract people. they say come to kenya,and come see the mountain. tanzanians should start promoting its land. no one is forcing you not to say the mountain is not in kenya. if that will increase tourists, use that tool too!..sio mnakaa chini na kunung'unika..its time to wake up and do something about it.
   
 7. bongo-live

  bongo-live JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2016
  Joined: Jul 3, 2013
  Messages: 824
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 80
  oyoooo..
   
 8. I

  Ian Cruz JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2016
  Joined: May 4, 2016
  Messages: 1,525
  Likes Received: 851
  Trophy Points: 280
  Mlalapo, vyenu twavichukua, muamkapo hamtuoni! hehe
   
 9. MK254

  MK254 JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2016
  Joined: May 11, 2013
  Messages: 9,424
  Likes Received: 6,625
  Trophy Points: 280
  Njooni Kenya muone mlima Kilimanjaro, halafu tuwanyofoe visenti.

  [​IMG]
   
 10. Shepherd

  Shepherd JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2016
  Joined: Dec 14, 2012
  Messages: 1,486
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Can't believe this?.
   
 11. Raphael wa Ureno

  Raphael wa Ureno JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2016
  Joined: Jul 12, 2016
  Messages: 6,369
  Likes Received: 10,285
  Trophy Points: 280
  Huo mlima huo tusipokuwa makini naona mbeleni kuna ramani italetwa kama ile ya lake nyasa.
   
 12. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2016
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 4,021
  Trophy Points: 280
 13. nyangau mkenya

  nyangau mkenya JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2016
  Joined: Mar 26, 2015
  Messages: 722
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 180
  :D:D:Dmufunike huu mlima na curtain basi , we can see both kili and mt kenya from as far as nairobi


  .
  [​IMG]
   
 14. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2016
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 4,021
  Trophy Points: 280
  nyangau mkenya, sisi tunalala nao tukiukumbatia sio kuuona tu bali hata kuupanda
   
 15. chongchung

  chongchung JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2016
  Joined: Jun 23, 2013
  Messages: 3,708
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Unauona sio? Kama mnavyoyaona maji ya ziwa Victoria 50% ours only 6% on Kenya na kama nyumbu wa Serengeti wanavyoingia Masai Mara but 90% time spend in Tanzania ukiangalia hapo Kilimanjaro is more strictly inaccessible to you compare to other we are sharing on mountain geography allowed you only to see view but never touch it.
   
 16. MK254

  MK254 JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2016
  Joined: May 11, 2013
  Messages: 9,424
  Likes Received: 6,625
  Trophy Points: 280
  We enjoy the view and make lots money from it. Hatuna haja ya kuukaribia, tunawaleta wanaangalia kwa mbali halafu tunanyofoa visenti.
  Jinsi ilivyo ziwa Victoria, asilimia yetu ndogo lakini tunatengeneza hela zaidi ya nyie wazembe wa kutupwa. Mna kila kitu lakini tunawashinda kwa kujituma, tunatumia kidogo tulicho nacho na kupiga hela mwanzo mwisho. Ujamaa uliwalemaza na kuwafanya muwe wazembe sana.
   
 17. kilam

  kilam JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2016
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 1,439
  Likes Received: 1,361
  Trophy Points: 280
  Acha uzwazwa wewe, Tanzania inatengeneza pesa nyingi kwenye utalii kuliko nyie wazembe wazembe.
   
 18. MK254

  MK254 JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2016
  Joined: May 11, 2013
  Messages: 9,424
  Likes Received: 6,625
  Trophy Points: 280
  Kwa raslimali mlizo nazo za utalii, zingekua zinamilikwa na wachapa kazi wa kweli na sio mivivu, hiyo nchi leo hii mngekua mnaongoza Afrika kwa uchumi. Nyie kwanza hapo ni nchi mbili, kuna kule nje kuna nchi visiwa vidogo hata kuliko Zanzibar kwa mfano Mauritius lakini wanapiga hela sana kwa kutumia fukwe tu, wanapata wageni milioni.

  Nyie mnatia hruruma kwa uzembe, na ndio maana nchi za Afrika zinatumia raslimali zenu kunyofoa hela, leo hii hata Botswana wanalamba hela kwa kutumia mlima Kilimnajaro maana mivivu mumelala usingizi wa kiza kikuu. Nchi kubwa yenye kila kitu lakini maskini mwanzo mwisho.

  Hebu fuata hii mada ameanzisha jamaa hapa
  ==================================================

  Mount Kilimanjaro in Botswana

  Habari za Jioni wanajF,
  Muda sio mrefu nimweka series inaitwa "ZOO". Yani nilichokiona ilibidi nishangae . Series inaanza kwa kuandikwa BOTSWANA tena kwa maandishi ya herufi kubwa na baada ya dk kama tatu nne hivi inaonsha watalii wapo katika gari yenye plate number za botswana wakitembezwa Katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro,haikuishia hapo cz kuna mtu alitumia neno "Rafiki" katika scene hiyo ya Mt Kilimanjaro.

  Kiukweli imeniuma sana cz najua hizi muvi ni moja ya matangazo ya kuitangaza maliasili zetu.

  Ifike wakati sasa tuchukue hatua kuzuia mambo kama haya yasizidi kuendelea.
  siamini kuwa haya ni makosa madogo ya directors wa Movie ila naona hii ni kusudi na ni mbinu mojawapo ya kuitangaza Botswana kupitia mgongo wa Tanzania. Kwasababu Kabla ya muvi kutoka huwa inafanyiwa uhakiki kisha ndio inaachiwa.Yani hata mazingira ya muvi yenyewe yamekaa kitanzania zaidi na sio kibotswana cz Kuna camp inaitwa MSISIMKO Safari camp pamoja na KITUKO camp.

  Haya ngoja niendelee kutazama huwenda nikagundua mengi zaidi.
  Nawasilisha
   
 19. kilam

  kilam JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2016
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 1,439
  Likes Received: 1,361
  Trophy Points: 280
  Wewe endelea kuchonga tu, mapata yatokanayo na utalii Tanzania ni mara tatu ya mnachokipata. Umasikini jeuri wenu haufanyi muwe wachapakazi au matajiri. Kama Mauritius wanatumia fukwe hata nyie mna fukwe pia.
   
 20. chongchung

  chongchung JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2016
  Joined: Jun 23, 2013
  Messages: 3,708
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Nyie kweli waKUNYA yaani mtushinde kwenye lake victoria sasa mbona tunaleta dagaa za viwandani na majumbani kwa matani kila uchwao na samaki?

  Mnatushinda labda kwenye kugombania kisiwa cha migori Uganda na mkileta vyokovyoko lazima Uganda ieatembezee kichapo nasikia kila siku mnatandikwa huko mpaka your civil servants wenu wanacharazwa si mchezo.

  Kudos to Uganda teach these arrogance fools some lessons.
   
Loading...