Njombe: Taarifa ya kupotelewa mbunge wetu

Njombe: Taarifa ya kupotelewa mbunge wetu

Aisee hata wetu wa temeke nasikia yupo maeneo ya kinondo huku temeke alishahama muda mrefu
 
Huyu hapa chini anatafutwa na wana sumbawanga, atakaemuona atoe taarifa kwa ndugai au makinda
download.jpg
 
wa shinyanga mjini ndo usiseme sijui kafia wapi, toka aibe kura za shelembi akasepa mazima
 
Hata sisi wnainchi wa Kongwa tunatoa taarifa ya kupotelewa na Mbunge wetu JOB Ndugai, sisi wapiga kura wake wa mlali na ndulugumi hatujawahi kumwona tangu amechaguliwa tunasikia tu ni naibu spika anafukuza wabunge wenzie wliochaguliwa na wanainchi kama sisi vile vile tunasikia ana wake wawili wanaoishi TABATA Dsm hivyo akimaliza vikao vya bunge hao wanawake wanamficha Tabata kama vile memechagua wao hivyo yoyote atayemwona Tabata atoe taarifa kituo cha police chochote kilichopo karibu.

Wala usihangaike atakuwa na case karibuni ya kuvunja kanuni za bunge atapelekwa mahakama ya kisutu utamuona
 
na mimi naomba kutoa tangazo la kupotelewa kwa mbunge wetu wa Simanjiro anaitwa Olesendeka maarufu kwa jina la tikiti maji, yeyote atakaye muona atoe taarifa kwenye kituo cha polisi kilicho karibu naye, zawadi nono itatolewa.
 
Wananchi wa jimbo la Lushoto mjini wanamtafuta shekifu, huwa mara moja moja akionekana anawanunulia Pombe wanawake wacheza vidembwa ili wamtungie nyimbo za kumtukuza.
 
Sie wennyewe modestus kilufi amepotea kwa atakayemuona zawadi nono itatolewa
 
Hata sisi tunatangaza kupotelewa na mtoto wa mkulima,aliondoka akiwa na jembe,shoka na panga akasema anakwenda kung'oa visiki shambani lakini toka 2010 hajawahi kuonekana,ila huwa anaonekana mara chache hususani tarehe 25 dec-2 januari. kila mwaka kwa huwaarika marafiki zake kwenda kwake Kibaoni kwa ajili ya mwaka mpya na christmas!!
 
Kwa kweli kabisa sisi wananchi wa Ovada na ndugu zetu wa Sanzawa tunamtafuta mbunge wa guest house na bar Juma Nkamia.
Toka tumemchagua tunasikiaga tu kazi yake kubwa kuchonga pencel yake kwenye vichongeo vya vibinti vidogo vidogo.
Pia akiwaita binadamu wenzake mambwa. Kwa kweli tuna shida nyingi sana ila hata siku moja atujamsikia akieleza matatizo yetu bungeni. Nimesikia watu wanamuita Mnafiki sijui kwa nini.
 
Hata juzi kura lilpopigwa kwenye suala nyeti kama muswada wa katiba, wabunge walioafiki na waliokataa jumla yao ilikuwa kama mia mbili tu kati ya wabunge wote 356. hii ina maana hawakufika hata thelithi mbili, mwendelezo kama huu ukifika kwenye bunge la katiba maamuzi yatakuwa hayafikiwi kikanuni.
 
Hongera mleta uzi kwa hili. Hata wa kwetu Arumeru Magharibi sijui alikopotelea, ngoja nikatafute picha zake za kampeni nibandike atakaemwona aripoti JF.
 
Eti mbunge wa mwanza anaonekana mliman city samaki samaki kila siku jimboni kwake anakwenda kama kuna msiba na harusi tu
Hilo ni Bunge la nchi gani? Maana hili la Tanzania hakuna jimbo la Mwanza.

 
Jaman mbunge wetu wa Muleba kaskazin anaitwa MWIJAGE huyu ndo kapotea jimbon tangu azomewe na cha kusikitisha had bungen nako hayupo. Alitoka nyumban akiwa kavaa shati la KIJAN na kofia ya NJANO.
Natangaza zawadi nono kwa atakaye muona.
Ukimuona piga simu namba M4C au toa taarifa kituo chochote cha police karibu nawe.
 
Mmmhh kumbe tupo wengi hivi jamani??
Anaitwa Donard Max mbuge wa jimbo la Geita mjini kupitia ccm,toka alipopotea baada ya uchaguzi wa 2010 hatujamuona yeye wala ahadi zake!
Atakae muona amufikishie taarifa kwamba 2015 sio mbali kiasi icho!!
 
sisi wa kara2 tupo naye daily na kila kikao cha bunge kikiisha anaita mkutano na kutuambia nini kimejadiliwa huku wa ngorongoro vijiwe vyake ni kara2 kama wanamtafuta nitaripoti kituo cha polisi kar2
 
Back
Top Bottom