Njombe: Harusi yaahirishwa sababu mwanaume hana Nida

Njombe: Harusi yaahirishwa sababu mwanaume hana Nida

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,108
Reaction score
7,144
Kijana Abelnego Mgaya, mkazi wa Mlevela Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, mkoani Njombe, amejikuta katika wakati mgumu baada ya harusi yake kuahirishwa kufuatia kushindwa kukamilisha usajili wa ndoa kwenye mfumo kwa sababu hana Kadi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

Mgaya amesema awali hakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu taratibu za usajili wa ndoa, hali iliyomfanya aendelee na maandalizi ya harusi bila kufahamu kuwa angehitajika kuwa na nyaraka maalumu ili kukamilisha usajili huo.

Amesema baada ya kufahamu utaratibu unaotakiwa, alianza kufuatilia kitambulisho chake cha NIDA huku akiendelea na maandalizi ya harusihata hivyo,juhudi zake hazikuzaa matunda kwa wakati, kwani hadi siku ya harusi ilipofika hakuwa amepata kadi hiyo, hali iliyosababisha ndoa yake kushindwa kusajiliwa na kuahirishwa.

“Kwenye mfumo, kitu walichohitaji ni barua pepe (email), namba ya NIDA pamoja na kadi yake. Au kama una namba ya NIDA pekee, unatakiwa kuwa na kadi ya mpiga kura au leseni ya udereva. Mimi nina namba ya NIDA pekee, lakini sina vitambulisho hivyo vingine,” amesema Mgaya.

Kwa upande wake, Lameck Moto, msajili msaidizi wa masuala ya ndoa mkoani Njombe aliyepata mafunzo kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), amesema changamoto iliyomkabili Mgaya ilitokana na kutokuwa na kitambulisho chochote kati ya vile vinavyokubalika katika mchakato wa usajili.

 
Nini maana na malengo ya kuwa na NIDA yenye kubeba majina, tarehe ya kuzaliwa ya mhusika na wazazi wake; sehemu alikozaliwa na anakoishi zilizohidhiwa kwenye mifumo ya NIDA ambayo RITA wana access nayo 24/7?

Hayo makolokolo mengine kama kadi ya mpiga kura, leseni ya udereva na passport ndio yangehitajika tu kama NIN haipo kabisa na si kulazimisha uwepo wa kitambulisho halisi hali namba pekee inakupa hadi kopi ya kitambulisho halisi.
 
Back
Top Bottom