Njiwa atua kwenye meza ya wagombea UVCCM na kuzua tafrani

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Njiwa atua kwenye meza ya wagombea na kuzua tafrani

AMINA KINGAZI, KOROGWE

KATIKA hali isiyo ya kawaida njiwa amezusha tafrani ya aina yake, baada ya kuvamia ukumbi wa uchaguzi wa viongozi wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM), na kutua kwenye meza ya wagombea na kufanya umati mkubwa uliojaa ukumbini hapo kupigwa na butwaa.

Maajabu hayo yalitokea juzi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, wakati Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga, Emmanuel Kiondo, ambaye amemaliza muda wake, alipokuwa akitoa hotuba ya kuwaaga wajumbe kabla ya kuanza uchaguzi.

Njiwa huyo alitua kwenye meza mbele ya mwandishi wa habari hizi,aliyekuwa anawania nafasi ya ujumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa na ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.

Baadaye njiwa huyo ambaye aliingia katika namna ya ajabu, aliruka na kutua juu ya dari usawa wa sehemu hiyo walipokaa wagombea hao, na kuzusha minong'ono ndani ya ukumbi huo, huku Kiondo akibashiri njiwa ni dalili za baraka na wala sio uchawi.

Katika uchaguzi huo, Amina aliwabwaga washindani wenzake wawili katika nafasi ya Baraza Kuu Taifa kwa kupata kura 358, Omari Muya 82 na John Kingwa 45.

Kwenye nafasi ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, alishinda kwa kura 331 na kuwapiga chini David Chihwaga aliyepata kura 97 na Rajab Abdallah kura 17.

Katika nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga, ambayo ilikuwa na ushindani wa hali ya juu, Rodgers Shemwelekwa aliibuka kidedea kwa kura 268 na kuwabwaga Mathew Mganga aliyepata kura 229 na Salum Losindilo kura 13.
 
Mi na wasiwasi na huyo AMina atakuwa alimleta Njiwa huyo kwa manufaa yake.
 
Back
Top Bottom