Njiani kwenda kwa Rais! – 2

Njiani kwenda kwa Rais! – 2

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,251
Ndugu zangu,

Niliandika juzi, kuwa mwaka 1964 yawezekana kabisa ndio ulikuwa ni mwaka mgumu sana kwa Julius Nyerere katika kipindi chake chote cha Uongozi wa nchi hii.

Ni mwaka uliokuwa na matukio makubwa yaliyoitikisa nchi na Rais mwenyewe. Kulikuwa na Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12. Kukawa pia na uasi wa jeshi wa Januari 20, na matukio mengine yakafuatia.

Mwandishi Stig Holmqvist kwenye kitabu chake; Pa vag till presidenten – ' Njiani kwenda kwa Rais', anaulezea mkutano mgumu kati ya Julius Nyerere na Balozi wa Marekani Tanzania, Leonhart.

Julius Nyerere alikwenda mwenyewe kwa Balozi kufafanua kilichotokea na kupelekea kuridhia Balozi mdogo wa Marekani Unguja afukuzwe nchini.
Ujumbe wa siri kwa njia ya telegramu kutoka kwa Balozi Leonhart kwenda White House na CIA unabainisha jambo hilo.

Inaelezwa na Balozi huyo, kuwa siku hiyo ya mkutano wake na Julius, Januari 16, 1964, kuwa hali haikuwa nzuri.
Balozi Leonhart anasema; " ....Nyerere alitingisha kichwa na hakutaka hata kuniangalia...."

Tumeona, kuwa katika mkutano ule, Julius Nyerere, pamoja na kutambua mapungufu, lakini alikataa katakata kubadili msimamo wake wa kumfukuza balozi huyo mdogo wa Marekani.

Julius alikuwa na miaka mitatu tu kama Rais. Alikuwa kijana wa miaka 42 tu. Na Chama chake cha TANU kilikuwa hakijatimiza hata miaka kumi. Na yeye mwenyewe, Julius, kumbukumbu za kutumia chaki za ubaoni kama mwalimu wa pale Pugu Sekondari huenda zilikuwa bado hazijamtoka.

Lakini, pale kwa Balozi wa Marekani, alikaa na kuongea kama Rais wa Tanzania. Ndio, alikuwa Rais mchanga kwenye nchi changa. Julius hakuwa na uzoefu wa siasa za kimataifa na hasa inapohusu ' michezo ya wakubwa'- Marekani na Uingereza kwenye upande mmoja, na Soviet Union, China na Cuba kwenye upande wa pili. Yawezekana pale Ubalozini Julius alikumbuka usemi wa wahenga; " Kua uyaone!"

Ikumbukwe, Julius alimfanya rafiki yake wa karibu, Oscar Kambona kuwa Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje. Na Oscar naye hakuwa na uzoefu. Hivyo, wote wawili; Julius na Oscar.

Miezi michache tu baada ya tukio lile Ubalozini, marafiki wawili; Julius na Oscar walifunga safari ya kwenda China. Ilikuwa ni mara yao ya kwanza kwa wote wawili kwenda China.

Huko China Julius na Oscar waliiona China kwa ' miwani tofauti'. Ni nini kilitokea kwa marafiki wawili hawa, Oscar na Julius, waliporudi nyumbani?

Panapo majaliwa nitawasimulia...

Pasaka Njema.

Maggid,
Dar es Salaam
 
Kwanini Julius Nyerere alimfukuza balozi mdogo wa marekani Unguja?
 
maggid na wengine (off mada ila ningependa sana kujua)

mwalimu aligombana na watu wengi tu wakati wa utawala wake hasa baada ya kupata uhuru 1961, lakini haijawahi kuandikwa popote ni nini hasa kilichosababisha yaani zinabaki ni tetesi tu kwenye jamii; sasa kwa aliyekuwa karibu na system atujuze kilichotokea kufarakana kwa wakuu hawa hadi wengine wakakimbia n'gambo.

Mwalimu alikorofishana na:
Oscar kambona (RIP) - Katibu mkuu wa TAA / TANU
Chritopher Kasangatumbo (RIP) - Balozi wa kwanza nchi uingeleza baada ya uhuru.

je ni nini kilitokea watu hawa wakawa against mwalimu? (its good for our history, nauliza si kwa ubaya)
 
Ni kweli, mwenye data azishushe. Ila kwa miaka ile mfumo ulikuwa tofauti na kwa nchi za kijamaa mambo yalikuwa si hadharani kama sasa ambapo demokrasia imekua. Nilichokuwa nampendea Mwl Nyerere ni kimoja tu, alikuwa mkweli na alikuwa hamung'unyi maneno, hata kama ulikuwa rafiki yake uki-mess out you go! hakuwa mvumilivu kwa aliyekiuka makubaliano. Wapo wengi akina Fundikira pia usiwasahau.
 
. maggid,

Sijui kwa nini mpaka leo upo uraiani? wacha kibanda arudi...
Usitake kutumia mgongo wa Nyerere kutaka kujisafisha,
unamaanisha Nyerere na Kambona ni sawa na wewe na Ludo?
Damu ya Mwangosi, maumivu ya Kibanda hayatakuacha kamwe.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu,
Julius alikuwa na miaka mitatu tu kama Rais. Alikuwa kijana wa miaka 42 tu. Na Chama chake cha TANU kilikuwa hakijatimiza hata miaka kumi. Na yeye mwenyewe, Julius, kumbukumbu za kutumia chaki za ubaoni kama mwalimu wa pale Pugu Sekondari huenda zilikuwa bado hazijamtoka.

Wahandisi wa habari hamkosi vituko!
 
Kwa haraka haraka ukiangalia mlolongo wa historia huhitaji kuwa profesa kung'amua kwa nini Mwalimu Nyerere alikorofishana na watajwa hapo juu pamoja na wengineo.
Ki- uhalisia unaweza kuona wengi wao waliokorofishana na Mwalimu walikuwa na unaweza kubaini kuwa ni watu waliona Ubinafsi (Mimi na Familia yangu kwanza) kitu ambacho kwa Mwalimu ili kuwa ni kama Muisilamu na Kitimoto-(Haramu/Mwiko

Wengi wamemwita Mwalimu Nyerere kwa mabaya mengi lakini Mwenyezi Mungu ndiye anayeweza kupima na kuhukumu kama Mwalimu kweli yote aliyoyapigania na kuyafanya yana Chembe yoyote ya Ubinafsi zaidi ya kuijali Nchi yake na Watu wake hadi anakufa na ni wasi wasi wangu kuwa itachukua 50yrs kuweza kupatikana binadamu kama yeye.
 
Mwandishi Stig Holmqvist kwenye kitabu chake; Pa vag till presidenten – ' Njiani kwenda kwa Rais', anaulezea mkutano mgumu kati ya Julius Nyerere na Balozi wa Marekani Tanzania, Leonhart.

Asante Mjengwa naomba nisahihishe kidogo hapo pekundu kama: På väg till presidenten
 
Back
Top Bottom