Njia zingine za mapato hizi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
NJIA ZINGINE ZA MAPATO HIZI

Miaka michache iliyopita niliwahi kufanya kazi sehemu moja , moja ya kazi zetu zilikuwa ni kutengeneza Programu mbali mbali zinazoweza kutumika kufanya kazi kwenye computer , siku moja jamaa mmoja akaja na ombi moja anataka programu ya masuala yake ya mahesabu lakini isihusiane na TRA .

Huyu mtu alikuwa na Maduka mengi ya vipuri vya magari pale kariakoo na sehemu zingine nchini haswa Arusha na Mwanza , alitaka programu ya kuhifadhi mahesabu yake lakini TRA wasishtuke ili kukwepa mapato , Siwezi kuelezea kilichokubaliwa ila Nilishaacha kazi kampuni hiyo

Kuna watu watu wengi sana hapa Tanzania wenye blogu zinazopendwa sana hapa Tanzania , blogu hizi zinakuwa na matangazo haswa wale wanaotumia blogspot huwa wanatangaza matangazo yao mengi kutumia huduma ya Google Adsense , wengi ukiangalia thamani ya blogu zao na pesa wanazotengeneza kwa siku kutokana na matangazo yale utashangaa .

Wengi haswa wale walio nchini wanashindwa kupata mapato ya matangazo kwenye Blogu zao kutokana na kutokuwa na mfumo wa kodi na taarifa zingine za kuweka ili kuweza kudhibitika ili uweze kupatiwa mapato yako , ukiwa nchi za ulaya ni rahisi ukiweka taarifa zako wanakata kodi na kukupa pesa zako .

Utashangaa mtu anapokwambia anafanya kazi kwa njia ya mtandao haswa kwenye tovuti analipwaje , anajiwezeje ni kwa njia hizi , hapa kuna kitu cha kufanya ili watu wengi wasipoteze mapato pesa hizo , serikali pia itapata kiasi kikubwa cha pesa kutokana na makato ya kodi , sasa blogu zinaweza kutumika kama kazi zingine .

Kuna watu wengi sana wako mitaani huko , wana uwezo wa kutumia vifaa hivi , hawana kazi za kufanya , lakini wakipewa fursa na serikali kufanyia kazi suala hili naamini wengi watakaa majumbani kwao na computer zao zilizounganishwa na mtandao kufanya kazi zao na kuendelea na maisha mengine kama kawaida .

Pia kuna waandishi haswa wa riwaya za Kiswahili , riwaya zao zinapendwa sana maeneo mengi , ila wengi hawajui pia kutumia fursa hizi za ICT katika kufanya kazi , Lakini hili haliwezi kufikiwa kama Tovuti wanazoweka Riwaya na tungo zao zingine hazina viwango , kama hazina viwango maana yake hazivutii watu , hazivutii watangazaji .

Kwahiyo wadau wa ICT pamoja na serikali wanaweza kukaa pamoja kuangalia suala hili kwa makini sana , kuna mengi yanayoweza kuboreshwa kutengeneza ajira nyingi zaidi pamoja na mapato mengi kwa serikali ,
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom