Kuna kipindi nilikuwa nafanya kazi bandalini nilikuwa nashughulika na chakula nilikuwa kitengo cha upakuaji, sasa kaka fulan hv anafanya kazi hapo bandalini yaan huyo kaka ni mzuri, mrefu tu wakutosha, halafu ana mwili fulani hv sio mwembamba wala mnene yaan mwili fulani wenye mvuto yaan hata wanaume wenzie wanamkubali halafu alikuwa na muonekano fulani hv yaan mpole, mstaarabu na alikuwa mtu poa hana malingo ndio nilizidi kumpenda, yy ni kama staff akija pale kuchukua chakula hana haja yakuletewa huwa anakuja jikoni kuchukua, bhasi wee! Nilikiwa nampendeleaje! Alikuwa mpenzi wa maharage yy hataki mchuzi mtilie tu nyama kavu iwe ya kuku, ng'ombe ama samaki nilikuwa nampendelea sana. Sasa kuna siku mfanyakazi mwenzangu akampimia mm nilikuwa na shughuli fulani hivi sikupata muda wa kumpia yaan nilichelewa kidogo ila nilikuwa nafanya ile shughuli ima nimpimie mwenzangu akaniwahi nilimaindi nikaanza kufoka nani kakutuma umpimie mteja wangu kwani hiki tengo chako, wafanyakazi wenzangu wakaguna wakasema unampenda huna lolote
Sent using
Jamii Forums mobile app