Njia za asili za uzazi wa mpango(Natural birth control methods)

Best angalia post number 82 on this page kisha uende huko. Haya mambo ya kuingiza vitu mwilini bila kujua athari zake hayahusu kitu. Unaweza kubaki unajuta kwa kipindi kirefu katika maisha yako.

ofcoz itakuwa spermicide manake ni kemikali. lakini sidhani kama ni sahihi manake hiyo ph ya ukeni inajitosheleza na kuingiza vitu vingine hukawii kuharibu utamu.

mie huwa siafiki vitu visivyofanyiwa tafiti. kama anataka spermicide zinauzwa phamacy nadhani kwa jina hilo hilo
 
dr tulishakubaliana mie na weye usiniwekee mipicha yako ya kutisha bwana. mie bado mdogo, ntaota usiku.
plz niko serious :wave:
Bibie King'asti
common-vampire-bat_505_600x450.jpg

Popo huyoooooooooooooo



bat-anatomy.jpg
 
Kwa kawaida kuna siku 8 tu kila mwezi ambazo mwanamke anaweza kupata mimba ambapo siku hizi zipo katikati ya siku zake za kwenda mwezini, na huanza siku 10 baada ya siku ya kwanza ya kupata damu ya hedhi. Hivyo basi ikiwa mwanamke yoyote hataki kupata mimba ni lazima aache kukutana na mwanaume kwenye siku hizi 8! Naamini hili linawezekana kwani siku nyingine zilizobakia wapendanao wanaweza kujiachia kama kawaida kwani hakuna uwezekano wa mwanamke kushika mimba!

Kwa mfano: Unaingia kwenye siku zako tarehe 5 Desemba, weka alama kwenye tarehe hiyo kisha hesabu siku 10 na baada ya hapo pigia msitari siku 8 zinazofuata!

MziziMkavu kwanza heshima yako mimi naheshimu sana michango yako humu jf hasa katika maswala ya tiba,nimejaribu kulisoma hili lakini nimeshindwa kuelewa,hapo katika nyekundu umekusudia ile siku ya kwanza kupata damu ya hedhi una maana kuanzia tarehe hiyo ndio salama kwa maana nyingine kama mwanamke amepata damu ya hedhi kwa siku 4 basi kuna siku salama siku 6 au umekusudia hesabu inaanza pale anapo maliza hedhi ndio kuna siku kumi salama?

Ingawa sijui jibu lako ni nini na hasa lengo hapa ni kuelimishana sio vibaya nikikupa uzoefu wangu..mimi binafsi natumia kalenda na hii imenifanya mpaka rafiki yangu wa kike ananishangaa kwani hata siku zikikaribia basi mimi huwa nachungulia kama pads zipo na kama hakuna kuwa na nunua kabisa,lakini nadhani situmii kikamilifu ila mchango wako umenifanya nipate hamu ya kujua zaidi..kwa kawaidi mimi huzingatia siku baada ya damu ya hedhi na haijatoke issue yaa ujauzito.

kwanza nikiri mimi sio mtaalam wa hili lakini kama ulivyo tangulia kusema mzunguko au kalenda ya mwanamke ina siku 28 ndimo mnamopatika siku za Damu ya hedhi,siku salama na siku za kushika mimba.
Labda tuanzia na siku ambazo mimba inaweza kushika hii pale yai la mwanamke linapokuwa katika sehemu ambayo kama likikutana na mbegu za kiume basi linafunga na ndio hali ya ujauzito inatokea "Lile swali la mbona sipati siku zangu linapo jitokeza"na kama haikutoke kukutana na mbegu za kiume basi hutoka kwa njia ya damu kwa maana hiyo mimba hutunga kabla kupata damu ya hedhi na baada ya kumaliza damu ya hedhi inachukua muda kidogo mpaka yai la mwanamke kuwa katika sehemu ambayo kama likikutana na mbegu za kiume ndio inakuwa mimba...na pia kuna ile hali ya mbegu za kiume kukaa kwa zaidi ya masaa 48 ndani ya uke zikiwa hai na ujauzito kutokea sikumbili baada ya kujamiiana.
 
Habar waungwana Naomba Maelekezo ya Njia ya ASILI ya kuzuia Mimba ambayo ni salama kabisa.

The 'after day pill' is an abortion pill. Which means if you fertilized her egg, and life has started - that basically you just aborted the child by preventing it from being able to implant into the wall of her uterus. Way to go dad! S orry, anti-stupidity abortion.

Quoted by Sunny: "It is only after 14 days of period that ovaries are produced" ((please don't believe a guy who doesn't even know about ovaries, and who thinks the ovary is the freaking egg))
God, if I had a buck for every baby born from 'it's scientifically impossible'

Back to the Day After Pill, it works for most women, but it can cause birth defects in the child if it manages to implant anyway, and eventually get born. It can also cause severe cramping, bleeding, and throw her period off for months.

Since I went through fertility treatments, I'll let you in on a little secret most teenagers here don't seem to know. A woman gets pregnant 14 days BEFORE her NEXT period. Not 14 days after her period. This makes a difference in women who don't cycle (start their period) every 28 days exactly. (and mos't don't).

So, have your girlfriend (buy it for her since you're sleeping with her) a little purse sized calendar. Have her mark down the days she bleeds, and in about 2 - 3 months you will see her pattern (or lack of a pattern) for her period. Then what you do is figure out that she SHOULD START her period Aug. 28th, so you then back track 14 days and now know on that date (14 days BEFORE Aug 14th) you don't want to have un safe sex for 4 - 5 days. Because sperm can live up to 5 days in a woman's body.

If it sounds like to much work, you ain't ready for kids. If you ain't ready for kids, you ain't ready for sex.
 
Mkuu ZeMarcopolo Njia za kuzuia kutopata mimba Kwa kutumia njia ya Sayansi na Teknolojia ya Tiba Mbadala zipo nyingi na zingine siwezi kuweka hapa.

Nimeweka njia mbili hapa ya kwanza Mwanamke atumie shabu kuweka sehemu zake za siri kwenye uke kabla ya tendo la ndoa.

Husaidia Spam au shahawa ya mwanamme inapotaka kuingia kwenye mfuko wa uzazi wa kike huwa hiyo shabu inaharibu hizo spam

shahawa za huyo mwanamme zinakufa nguvu na mwanammke anakuwa hawezi kupata mimba. Na njia ya Pili ya kicxhwa cha Popo

anakiweka huyo Mwanamke amabaye anataka asipate mimba kwenye ndani ya Mto wake wa kulalia basi atakapo fanya tendo la

ndoa hawezi kushika mimba mpaka akitowa hicho kichwa cha Pop anaweza kushika mimba jaribuni dawa zangu kisha munipe

Feedback. Chanzo MziziMkavu ( "The Chemical")

sasa MziziMkavu hicho kichwa kikianza kuoza si chumba kitajaa harufu ya mzoga, au ulimaanisha fuvu la kichwa cha popo??
 
Last edited by a moderator:
Natafuta dawa ya kutowa
mimba. Mkewangu amenasa mimba akiwa anamtoto wa miezi mitatu. Niaibu
lakini imekuwa badi lak nawaombeni, mnishauri.

nakushauri usithubutu ni dhambi ;mm nilipata hivyo hivyo watoto sasa wakubwa wako kama mapacha;unaona aibu je ukijahitaji ukakosa; muangalie Mungu na sio wanadamu
 
je kufunga kizazi kwa mwanamke pia kuna madhara yoyote kama zile njia zingine za uzazi wa mpango?
cc: MziziMkavu Riwa meningitis King'asti
Jeji..kufunga kizazi hakuna madhara yoyote, bali unapofunga ni irreversible, yaani hautapata tena ujauzito kwa njia ya kawaida. Ni procedure ya upasuaji mdogo unaofanywa kuziba mirija ya mayai (fallopian tubes), hivyo hauna madhara yoyote.
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu hii njia kuhesabu tarehe naiogopa kama ugonjwa,nilikuwa mtaalamu sana lakini at the end ikaniumbua. Labda kama nitapata njia waliyotumia bibi zetu zamani
[h=2]Jamani kwa yeyote anayejua 'siku ya kushika mimba hapa ni ipi'??[/h]
Akianza kubleed siku hiyo anza kuhesabu siku tisa hawezi pata mimba hata kama utaenda dry
Siku ya 10 mpaka 14 hapa yai hua linapevuka kwa hiyo ukilala nae mimba inaingia
siku ya 15 mpaka 22 hapa fresh no mimba
siku ya 23 mpaka 27 hapa anapata mimba maana yai huwa linashuka
siku ya28 mpaka siku za bleed hakuna mimba
 
Habar waungwana Naomba Maelekezo ya Njia ya ASILI ya kuzuia Mimba ambayo ni salama kabisa.
QARNAFIL utapo twanga mbegu zake na akawa anakunywa mwanamke kila anapotoka katika siku zake hii huzuwia uja uzito kutoshika mimba na haina madhara chemsha kunywa au unaweza kila siku ukawa unameza mbegu moja.
 
QARNAFIL utapo twanga mbegu zake na akawa anakunywa mwanamke kila anapotoka katika siku zake hii huzuwia uja uzito kutoshika mimba na haina madhara chemsha kunywa au unaweza kila siku ukawa unameza mbegu moja.

hizi ni mbegu gani mzizimkavu?
 
[h=2]Jamani kwa yeyote anayejua 'siku ya kushika mimba hapa ni ipi'??[/h]
Akianza kubleed siku hiyo anza kuhesabu siku tisa hawezi pata mimba hata kama utaenda dry
Siku ya 10 mpaka 14 hapa yai hua linapevuka kwa hiyo ukilala nae mimba inaingia
siku ya 15 mpaka 22 hapa fresh no mimba
siku ya 23 mpaka 27 hapa anapata mimba maana yai huwa linashuka
siku ya28 mpaka siku za bleed hakuna mimba

basi mimi hapa naelewa tofauti kutokana na vitabu nilivyosoma. ukiaanza period tu siku ya kwanza unahesabu siku kumi.ile ya kumi unaianzia tena kuhesabu moja mpaka zifike siku nane hizo ni ovulation, ambazo ndo waweza kupata mimba tu katika mwezi.
 
Habari wakuu wote jamvini....

Nimepata kusikia kuwa binti akinywa juice ya majivu ndani ya saa 2 toka mbegu za kiume ziingie ktk papuchi ake basi anakuwa salama kbs kuepuka mimba bila kujali siku ya salama au hatari.
Mchanganyo uko hivi,

1. Weka majivu nusu glass

2. Jaza sehemu ya glass iliyobaki kwa maji safi

3. Koraga na ili upate mchanganyiko mzuri

4. Acha maji yajitenge na majivu

5. Kunywa maji ya juu

Zingatia: waweza andaa juice hiyo kabla ya kuanza tendo kwa usalama. Juice haina madhara. Japo yaweza sababisha tumbo kuuma kwa muda mfupi.

Juice ina ukakasi/uchachu.

Wewe wajua kinga ipi ya asili?

Tupeane mawazo wadau wangu. Wote mnakaribishwa

==============
Majivu yatumika kupanga uzazi na utoaji mimba Mbeya

January 7th, 2013 | Na Gordon Kalulunga

LICHA ya Serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoa elimu ya kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kote nchini, baadhi ya wanawake katika wilaya ya Mbeya Vijijini na Jiji la Mbeya wamekuwa wakitumia majivu kama njia ya kupanga uzazi na kutoa mimba zisizotarajiwa.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala hii katika mji wa Mbalizi Mbeya Vijijini na kata ya Manga na Foresti Jijini Mbeya umebaini kuwa wanaoongoza kwa kutumia njia hiyo ni pamoja na wake za watu na wahudumu wa Bar.

Wanawake waliohojiwa wakiwemo wawili kati yao ambao wakawa na mahusiano na mwandishi wa makala haya ili kukamilisha uchunguzi, walisema kuwa majivu hayo wanakunywa kikombe kimoja kila baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa na wanaume ambao wana mahusiano nao ya kimapenzi na wengine waume zao.

''Majivu unatakiwa unywe ndani ya masaa 12 baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa ili mimba isitunge'' anasema Mama Angel mkazi wa eneo la Mama John ambaye ni mke wa mtu.

Mama Angel anakiri kuwa amewahi kutoa mimba kwa njia za kisasa ambayo haikuwa mimba ya mumewe na alipoambiwa kuwa kuna njia zingine za kujikinga ikiwemo kunywa majivu baada ya tendo la ndoa ameendelea kutumia njia hiyo kwa miaka mitatu sasa.

''Kule hospitali nilitundikiwa maji ya uchungu ambayo yanaongeza njia na ndani ya masaa matatu mimba ikatoka'' anasema Mama Angel bila kutaja hospitali aliyotolea mimba.

Uchunguzi huo uliofanywa mwezi Octoba na Novemba 2012, umebaini kuwa kwa sasa wanawake wengi hawapendi kutumia njia za uzazi wa mpango wa kisasa mfano Sindano, vipandikizi na vidonge kwa madai kuwa huduma hizo zina madhara.

Wanawake 43 waliohojiwa wakiwemo wake za watu 13 walisema kuwa madhara waliyoyapata baada ya kutumia njia za uzazi wa mpango wa kisasa ni pamoja na kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Baadhi walisema kuwa wanaogopa kufanyiwa upasuaji (kusafishwa) kunakotokana na uvimbe unaosadikika kutokea baada ya kutumia kwa muda mrefu huduma hizo za kisasa hasa vidonge maarufu kama majira.

''Tarehe za Hedhi hubadilika na kutoeleweka baada ya kutumia dawa hizo za uzazi wa mpango wa kisasa zikiwemo sindano na vidonge'' anasema Naomi Haule ambaye ni mhudumu wa Bar.

Wengine ambao waliomba hifadhi ya majina yao, wanasema mbali na kutumia majivu kama njia ya uzazi wa mpango kuzuia mimba na utoaji mimba, baadhi yao wanatumia kisamvu, Vidonge vya uzazi wa mpango maarufu kama (Majira) na majani ya mti unaojulikana kwa jina la Songwa kutoa mimba zisizotarajiwa.

''Wake za watu wanaopata mimba ambazo si za waume wao, wafanyabiashara na wahudumu wa Bar siyo siri tunaongoza katika kutumia njia hizi na utoaji mimba kwa njia za kienyeji'' anasema Rehema Mwakitalu akiwa na wenzake eneo la Mwanjelwa ambaye pia ni muhudumu wa Bar.

Walipoulizwa kuwa kwanini wasitumie njia za kisasa katika utoaji mimba walisema kuwa kikwazo ni gharama za utoaji mimba kwa njia za kisasa ambapo mwanamke mwenye mimba ya mwezi mmoja hutozwa Shilingi 40,000 ili asaidiwe kutoa mimba hiyo.

Walizitaja hospitali ambazo zinahusika kutoa mimba hizo kwa siri kuwa ni pamoja na hospitali ya wazazi Meta na zahanati zingine za madaktari binafsi zilizopo eneo la Nzovwe, Mama John na Uyole.

Aidha mbali na hospitali hizo, wanawake hao walisema kuwa pia kuna waganga na wakunga wa jadi wanaowasaidia kutoa mimba hizo ambazo wanadai kuwa hazikutarajiwa na kwamba wakunga hao wapo eneo la Mapelele wilaya ya Mbeya na Iwambi Jijini Mbeya.

Kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi wanasema; '' Ni bora kupata ukimwi kuliko mimba kwasababu ukipata ukimwi unajulikana baada ya mud asana na unapata dawa za kurefusha maisha lakini mimba ukipata huwezi kuendelea na starehe na ukijifungua unalazimika kulea mtoto kwa muda mrefu huku na wanaume wengi hawaeleweki kwenye matunzo'' wanasema wanawake hao.

Wanawake wahudumu wa Bar walipoulizwa kuwa kwanini wanatumia zaidi majivu kama njia ya uzazi wa Mpango na utoaji Mimba walisema kuwa baadhi ya wanaume huwa hawapendi kutumia mipira (Condom) wakati wa kujamiiana hivyo baada ya tendo la ndoa wanalazimika kutumia njia hiyo kama moja ya njia rahisi ya kuzuia mimba kutotunga.

Walipoulizwa kama wanajua madhara ya kutumia huduma ya majivu na kisamvu kwa muda mrefu kama huduma ya uzazi wa mpango na utoaji mimba walisema kuwa hofu yao ni kwamba wanaweza kupata kansa au kutozaa tena.

''Ili kuepukana na kupata madhara ya kansa yanayoweza kutokana na majivu, huwa mtu akinywa basi siku hiyo anatakiwa kunywa maji kwa wingi ili kupunguza kemikali zitokanazo na majivu'' anasema Asha Juma.

Anasema yeye ni Mama wa watoto watatu na tangu amepata mtoto wake wa kwanza mwaka 1998 amekuwa akitumia majivu kila baada ya tendo la ndoa.

Na kwamba alipojaribisha kutumia vidonge alisumbuliwa na nyonga na kukosa hamu ya tendo la ndoa hatimaye akaenda kusafishwa na alipojaribisha sindano pia alipata madhara ya kukosa hamu ya tendo la ndoa ambapo mpaka sasa anatumia Majivu kama njia salama kwake ya uzazi wa mpango.

Baadhi ya madaktari waliohojiwa kwa sharti la kutoandika majina yao gazetini wamekiri kuhusika na biashara ya utoaji mimba kwa njia za kisasa na kuzitaja njia wanazotumia.

''Wenzetu kuna sheria za utotaji mimba lakini ajabu hapa Tanzania tunakataza wakati watu wengi wanatoa mimba tena hasa wake za watu na njia ambazo wengi tunazitumia kwa usalama zaidi ni kuwatundikia Drip za maji ya uchungu na vidonge vya uchungu vinavyoongeza njia kwa mwanamke''wanasema madaktari hao kwa nyakati tofauti.

Siku wanazotumia zaidi ni siku za Jumapili ambapo wanasema kuwa baada ya kumaliza utoaji huo wa mimba wanawake hao wanatoka wakiwa salama na kuwapatia dawa za kutuliza maumivu na kuwashawishi kula vyakula na vinywaji vya kuongeza damu.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa, katika sayansi ya akili watu wanaojamiiana huwa wanatumia kinga mara ya kwanza na ya pili baada ya kuanza mahusiano na huwa hawatumii tena kinga baada ya kukutana mara ya tatu na nne na kuendelea.

Sanjari na hayo imebainika kuwa wauguzi wengi huwa hawatumii njia za kisasa za uzazi wa mpango licha ya kuendelea kuwashawishi wananchi wengine kutumia njia hizo kwa madai kuwa vidonge hivyo huwa wakimeza haviyeyuki.

''Sisi wengi hatutumii kwasababu kuna madhara makubwa ukitumia kwa muda mrefu ambapo ukitaka kuzaa unalazimika kwenda kusafishwa kizazi na vidonge hivyo haviyeyuki na inatia hofu kuwa ukikwanguliwa unaweza usizae tena'' walisema baadhi ya wauguzi wa hospitali za Ifisi Mbalizi na hospitali ya wazazi Meta kwa sharti la kutotaja majina yao.

Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu, anasema kuwa mila na desturi ni tatizo katika utumiaji sahihi wa uzazi wa mpango na kwamba katika wilaya ya Mbeya Vijijini mwaka 2011 vilitokea vizazi hai 38 kati ya 100,000 na vifo 113.

Kwa upande wa Jiji la Mbeya mwaka 2011 anasema vizazi vilikuwa 109 kati ya 100,000 na vifo vilikuwa 363 ambapo katika uzazi huo hospitali ya wazazi meta ndiyo inahusika zaidi na inahudumia wanawake pia wanaotoka nje ya Jiji la Mbeya.


Chanzo: https://www.jamiiforums.com/blog/majivu-yatumika-kupanga-uzazi-na-utoaji-mimba-mbeya


=========
April 18, 2015:
Habari zenu wana MMU,

Habari za siku nyingi leo nataka nitoe ushauri kwa dada zangu au wadogo zangu, pia hata kwa kaka zangu kuhusu jinsi yakuweza kuzuia mimba kwakutumia njia ya asili tofauti na kama tujuavyo wengi wetu kwa sasa wamekua wakitumia njia kama vidonge vya kizuia mimba, sindano na vijiti ambapo njia hizo za za uzazi wa mpango zmekua na madhara makubwa kwa wanawake ikiwa na uke kua na maji na uvimbe tumboni.

Njia yenyewe ya asili ni majivu
Jinsi ya kutumia majivu ni unakoroga kijiko kimoja au viwili kwenye kikombe au grass sio lazima ijae maji unasubiri baada ya dakika tano ndio unakunywa na waweza kunywa majivu hayo lisaa limoja kabla ya tendo au baada ya tendo lakini yasizidi masaa sita baada ya tendo.

Ni njia nzuri sana na haina madhara pia ni njia ya asili na ni njia ambayo hata mimi nimekua nikiitumia na rafiki zangu pia.
 
Back
Top Bottom