Njia za asili za uzazi wa mpango(Natural birth control methods) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia za asili za uzazi wa mpango(Natural birth control methods)

Discussion in 'JF Doctor' started by Baba Mtu, Dec 22, 2010.

 1. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Habari wanaJF,

  Nimeleta kwenu bandiko lako ili tuweze kujadili njia mbalimbali za asili za kupanga uzazi.

  Tujadili...  2. Uzazi wa Mpango: Jinsi ya kutumia Majivu kuzuia mimba

  3. Matumizi ya mbegu za Mnyonyo kupanga uzazi
  4. Mwanaume kumwaga nje ya uke ( Pull Out Method )

   

  Attached Files:

 2. Tores

  Tores JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 425
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Asante mkuu!
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Asante sana, sasa nipo kwa mobile ya china siwezi pakua hiyo file, kama utaweza naomba nitumie kwene kwene PM maana nimechoka kupumzishwa kinguvu, yaani unatoka huko na nguvu kama nyati, ukija aaah unakumbuka kua hayo ni maeneo ya penati huruhusiwi kucheza rafu....unaishia kununa!
   
 4. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yaani huwezi amini mpaka leo siwezagi kusoma hayo majedwali.nimefungua la kwako lakini naona chuya tu.sijui hata nijisaidiaje
   
 5. M

  Muinjilisti Senior Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli sijalielewa kabisa? Labda kwa kutusaidia utupe maelezo. Maana najua mzunguko ni siku 28 au 21, sasa la kwako limeenda siku 33!
   
 6. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hizo siku 33 bado ni chache kwani mara nyingine inafika hadi 45 days kutegemeana na mwili wa mwanamke, na ndio maana familia zinakosa watoto au zinapata watoto wasiowatarajia; sababu wanapishana na OVULATION.

  Naomba ufute ile nadharia kuwa siku ya 14 au 15 ndio siku hatari kujamiiana.
  Msijali nitawaelezeeni vizuri wakti mwengine leo muda hautoshi, baba mtu niko kwa ajili ya kujenga na si kubomoa. Ntakutumieni ktk pm zenu.
   
 7. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Kama mwanamke mzunguku wake wa hedhi ni siku 28 ataweza vipi kufuata calender bila kutumia kinga tajwa hapo juu wakati akifanya mapenzi na asipate ujauzito.?
   
 8. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Chukua 28/2=14, chukua 14-5=9, 14+3=17, danger days zako ni kati siku 9 hadi siku ya 17. Siku zilizobaki enjoy na mmeo bila matatizo, kumbuka hizo danger days mmeo awe mvumilivu coz ni kama siku tisa hivi. Na siku tunahesabu kuanzia pale unapoanza kubleed kwa mara ya kwanza kwa mwezi husika, ukifuata hii calendar method is the best without side effects like other methods. Best wishes any question please do hesitate to ask.
   
 9. m

  majimbi Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hii mada ya huyu mkuu hapa juu nimeipenda,, na kama naenda siku 32 hadi 34? nagawanyaje? halafu nina ham ya kubeba baby girl doctor hem nisaidie ni siku ya ngap au siku nzuri ya kubeba mtoto wa kike? hem nisaidie plz
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hebu Mkuu mupirocin fafanua kidogo maelezo yako.
   
 11. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hebu Mkuu Mupirocin fafanua kidogo maelezo yako.
   
 12. m

  mANg'HOnDi Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilivyoelewa mimi ni kwamba 28/2 =14 means nusu ya mwezi (siku 14) ni salama na nusu nyingine ni danger. lakini itategemea na mwanamke. kwa wenye mzunguko pungufu ya siku 28 au zaidiya 28 kama hapo kwenye red, danger/safety zone yao itavary kutegemeana na mzunguko wake thats why tunachukua 14-5 or 14+3 ambapo siku 9 mpaka 17 ndo danger zone kuanzia siku ya kwanza ya kubleed.
   
 13. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Kwa kuongezea tu, si lazima hizo nane hapo kati kati ndo usifanye kabisa unaweza fanya kwa condom au km mtaweza mume apiss nje.
  Kwa mzunguko wa 28 days, zile nane za kati ndo unsafe days ktk hizo 4 za mwanzo ni baby girl na 4 za mwisho ni baby boy.
   
 14. m

  majimbi Member

  #14
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Oooh whao asanteni sana kwa ushauri mzuri JF doctor. nimeelewa
   
 15. N

  Nabihu JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2013
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Habar waungwana Naomba Maelekezo ya Njia ya ASILI ya kuzuia Mimba ambayo ni salama kabisa.
   
 16. Meljons

  Meljons JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2013
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 2,591
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Ni kutofanya lile tendo tu. Zingine zote utanaswa tu
   
 17. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2013
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Kwanza lazima ujue kuwa hakuna njia salama kabisa(100% safe)...
  Pili kwa kuwa unahitaji kujua njia ya asili, basi njia pekee ni kusoma mzunguko wa hedhi wa mwanamke na kuepuka kufanya mapenzi zile siku hatarishi...
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  KUTUMIA KALENDA KWA KUZUIA MIMBA


  [​IMG]
  Kwanza nataka niwaeleze wadau juu ya athari za vidonge vya kuzuia mimba:

  Wanawake wengi hujikuta wanakumbwa na machafuko ya tumbo au kutapika wakati wa asubuhi, kuvimba matiti kama siyo kukumbwa na dalili za ujauzito mara wanapoanza kutumia vidonge kwa mara ya kwanza!Hii husababishwa na vidonge hivyo ambavyo vina hormones zile zile ambazo mwanamke huzitia kwenye damu wakati akiwa na mimba. Hata hivyo wataalam wanasema kuwa dalili hizi hufikia kikomo baada ya miezi kati ya 2 hadi 3.

  Sambamba na hilo watumiaji wengine wavidonge hutokwa na damu nyingi wakati wakiwa kwenye siku zao.

  Athari kubwa anayoweza kuzipata mtumiaji wa vidonge vya kuzuia mimba ni kuganda kwa damu kwenye moyo, mapafu au ubongo!

  Wadau naomba muelewe kuwa kwa wanawake wengine mimba pamoja na kutumia vidonge vya kuzuia mimba vina hatari kubwa zaidi kwao. Hivyo basi wanawake hawa ni lazima watumie njia zingine za kuzuia mimba!

  Baada ya kutanabaisha hayo naomba sasa nimjibu dada yangu jinsi yakutumia kalenda kujikinga na mimba!

  Njia hii haina uhakika sana wa kuzuia mimba, lakini ni nzuri kwa sababu haigharimu chochote.Njia hii huwafaa zaidi wanawake amabo taratibu za siku zao za kwenda mwezini ni kawaida mara moja kila baada ya siku 28, na ili iweze kuzaa matunda, njii hii huhitaji mtumiaji awe tayari kukaa bila kukutana kimwili kwa muda wa wiki moja kila mwezi!

  Kwa kawaida kuna siku 8 tu kila mwezi ambazo mwanamke anaweza kupata mimba ambapo siku hizi zipo katikati ya siku zake za kwenda mwezini, na huanza siku 10 baada ya siku ya kwanza ya kupata damu ya hedhi. Hivyo basi ikiwa mwanamke yoyote hataki kupata mimba ni lazima aache kukutana na mwanaume kwenye siku hizi 8! Naamini hili linawezekana kwani siku nyingine zilizobakia wapendanao wanaweza kujiachia kama kawaida kwani hakuna uwezekano wa mwanamke kushika mimba!

  Ili kuepukana na kutatanikiwa, ni lazima mwanamke aonyeshe kwenye kalenda zile siku ambzo hatakiwi kukutana na mwanaume. Hapa inaweza kuwa ngumu kuchora kalenda ya ukutani kwa kuwa inatumiwa na wengi lakini ni rahisi kutekeleza hili kwa kutafuta pocket kalenda [kijikalenda ambacho waweza kiweka kwenye pochi yako]

  Kwa mfano: Unaingia kwenye siku zako tarehe 5 Desemba, weka alama kwenye tarehe hiyo kisha hesabu siku 10 na baada ya hapo pigia msitari siku 8 zinazofuata!

  Angalia mfano huu:-

  Kumbuka siku hizo nane utakazozipigia msitari ni hatari kwani ukikutana na kidume tu na kushiriki ngono bila kutumia kondom utashika mimba, hivyo ni vema usikutane na mwanaume hata kidogo, yani epuka hata akikubembeleza na lugha laini kuwa nitapizia nje sweetie, sijui nini na nini kama hataki tumia kondom kataa kwani kupizia nje ni bahati nasibu hasa pale mwanamke anapoamua kumpa mwanaume maujuzi ya kabatini ambayo ni adimu, yaani mwanaume hupewa kwa sababu maalum tu hali inayomfanya apagawe kwa huba na hivyo huweza msababisha ashindwe kupiziza nje!

  Nimalize kwa kusema kuwa, mwanamke anapaswa kuendelea na utaratibu huu kila mwezi lakini akumbuke kuwa, njii haina uhakika sana mbaka itumiwe sambamba na njia nyingine kwama vile kondom.cc.@
  Nabihu
   
 19. Meljons

  Meljons JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2013
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 2,591
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  MziziMkavu hii njia kuhesabu tarehe naiogopa kama ugonjwa,nilikuwa mtaalamu sana lakini at the end ikaniumbua. Labda kama nitapata njia waliyotumia bibi zetu zamani
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2013
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Tumia condom kwa siku za hatari lakini ziongeze kuwa kati ya 9 hadi 16 kwa usalama zaidi. Ungeenda kwa vitengo cha wazazi hospitali yoyote ungepata ushauri. Kuna uzi humu utafute wa kuhusu madhara ya njia za kuzuia uzazi. Alianzisha gfsonwin kama sio Kaunga
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...