Njia ya Kupokea Mzigo Wako Ulionunua Mtandaoni (Kikuu, Alibabaexples )

Rdj Shibo

Member
Jan 5, 2018
71
40
Ndugu zangu wengi tunapenda kufanya manunuzi ya vitu mtandaoni mfano Alibaba na Kikuu ila je tunapataje vitu

1:Njia gani salama za kutumia kuletewat mzigo

2:je anuani gani au utambulisho gani natuma ili mzigo ufike kwenye eneo husika

3:je gharama gani nitatoa au kulipia nitakapo pokea mzigo

4:je usalama wa hizo njia mfano posta je endapo mzigo wangu ukaibiwa

5:muda gani uchukua hadi nipate mzigo wangu.

6:je posta zetu zinapokea mzigo toka nje na je kuna ufanisi kweli wa usalama na ni mizogo gani,kiwango au uzito
Karibuni tusaidiane
 
Wewe ukishalipia tu mzigo ulioupenda kupitia mastercard au visa nk na baada ya kujaza anuani ya mahali pa kupokelea mzigo, basi we subiri mzigo wako.

Kama hutapokea, utapewa refund.

Lakini asimilia kubwa tunapata mizigo yetu, acha presha.
 
Kwa Moderato nawaomba musi unganishe Uzi huu katika Uzi wa kununua au kufanya manunuzi mtandaoni
Ndugu zangu wengi tunapenda kufanya manunuzi ya vitu mtandaoni mfano Alibaba na Kikuu ila je tunapataje vitu
1:Njia gani salama za kutumia kuletewat mzigo
2:je anuani gani au utambulisho gani natuma ili mzigo ufike kwenye eneo husika
3:je gharama gani nitatoa au kulipia nitakapo pokea mzigo
4:je usalama wa hizo njia mfano posta je endapo mzigo wangu ukaibiwa
5:muda gani uchukua hadi nipate mzigo wangu
6:je posta zetu zinapokea mzigo toka nje na je kuna ufanisi kweli wa usalama na ni mizogo gani,kiwango au uzito
Karibuni tusaidiane

Kwanza kikuu ni exceptional, wana njia za shipping ambapo hawatumii hiduma za posta. Wana office zao mikoani ambapo utaenda kupokea mzigo wako ukifika na wanakutumia meseji.

Tatizo la kikuu bidhaa zao ni za kichina sana (mbovu).

Kusubiria mzigo ni kuanzia mwezi mmoja na kuendelea na hawana protection nzuri kwa mteja. Yaani hawana mfumo mzuri wa kushughulikia malalamiko ya wateja wao.

Aliexpress: wanatumia huduma za courier kama vile Posta, fedex, Dhl etc.
Unaponunua mzigo Aliexpress unachagua shipping unayoimudu kulingana na gharama na uharaka wako.

Utapewa tracking number ya kukusaidia kujua mzigo wako umefika wapi. Mizigo inachukua kati ya wiki 2 hadi miezi 3. Na endapo mzigo wako hutafika, basi wanakurudishia pesa zako zote.

Posta hawana tatizo, mzigo ukifika unatumiwa sms na kupewa number ya mzigo wako.

Utalipia sorting fee kama ni mzigo mdogo usio na kodi na kama huna sanduku la posta. Kama una sanduku la posta basi hii sorting fee haitakuhusu.

Ila kama ni mzigo wa kulipia kodi utalipia kodi na sorting fee hapo posta kabla ya kuondoka na mzigo wako.
 
Mimi natumia kikuu nikishalipia tu nasubiri mzigo wangu mlangoni ghetto kama jamaa akiwa yuko bize Na mzigo Ushafika ndio naendaga kuufata mwenyewe
 
Nilitarajia wangetuonesha Njia za kufanya jinsi ya kulipia ,na mfumo gani unatumia kulipia bidhaa
 
Kikuu ni noma
Wapo vizuri kwenye delivery.... ila sasa kwenye roho ikipendacho ni kihoro tupu
 
Back
Top Bottom