Mtu Poa 2013
Member
- Mar 26, 2013
- 86
- 45
habari zenu
Leo nimeona niongelee suala linalowagusa vijana wengi wanaoanza maisha na kujipanga ili waweze kuwa na makazi yao binafsi ya kwanza. Vijana wengi wamekuwa wakitapeliwa hasa Dar wakiuziwa viwanja ambavyo wameshauziwa watu wengine, na matokeo yakw kijana huyu akishajenga nyumba yake anakuja kusumbuliwa na watu wengine walioshauziwa eneo lile. Nimekuwa nikifikiria ipi ni njia salama ya kununua viwanja kwa usalama ili kuepuka matatizo kama hayo hapo juu. Unaweza nunua kiwanja kutoka kwa mtu kwa bei ya chini lakini hakina hati anakwambia ukakipime wewe mwenyewe. Hii faida yake ni kuwa unapata kiwanja cheap sema unaweza kuta ashauziwa mtu mwingine. Option ya pili ni kununua kutoka viwanja vilivyopimwa na serikali ambavyo kwa hapa kibaha ni sh. 6000 kwa mita ya mraba ambayo kwa sisi vijana tunaobangaiza ni expensive.
Kwa watu walioshapitia ishu za kununua viwanja, mnatushaur vipi sisi vijana wenzenu ambao hatuna hela nyingi ila hatutaki kutapeliwa na kuingia kwenye matatizo yasiyo ya lazima?
Asanteni