Njia salama za kununua kiwanja kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia

Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,557
2,000
Mkuu, ukipeleka hizo coordinates, hao wahusika wanaweza kukuambia hapafai, afu wao wakamtamfuta mmiliki wakakinunua, afu wakaja wakawapiga watu hela ya maana.

Hapana Kaka, Ukifika Wizarani kama unajua kuangalia Ramani unaweza kuangalia mwenyewe bila ya hao watu, unachofanya ni kuwaambia unaomba eneo lenye hizo Coordinates, wao watakupa ramani na unaanza kuiangalia mwenyewe, la kama huwezi/hujui basi ndio unawashirikisha wale wafanyakazi kwenye kuangalia ramani na kukupa mafasilio.
Pia kama eneo linamaster plan, Ramani zinakuwa zipo wilayani unaweza kupata hizo ramani zenye coordinates husika hapo hapo wilayani bila kwenda Wizarani.
 

hekimatele

JF-Expert Member
May 31, 2011
9,897
2,000
Mimi binafsi naamini kutapeliwa ni jambo unalolipanga mwenyewe. Hivi kweli umehangaika miaka mingi kutafuta pesa halafu leo mtu tu from no where anakutapeli?!.

Viwanja vilivyopimwa kwa Dar kwa mfano ni aghali sana na watu wanataka rahisi. Hii kazi ya kuuza viwanja kwa Dar ina changamoto sana na si rahisi kihivyo. Mimi ninakutana na mteja anataka kiwanja cha milioni tano halafu maeneo anayokutajia anataka huwezi kupata hata cha milioni 15, ukimtajia wapi atapata hicho cha milioni 5 anaona unamdanganya. Kuna maeneo hapa kiwanja tu si chini ya milioni 100. Kama wasemavyo watu siku zote vizuri ni gharama.

Ni kweli utasisitiza kiwanja kiwe na hati lakini watakaomudu bei yake ni wachache sana na kwa mazingira ya sasa huwezi kwani sehemu kubwa ya ardhi haijapimwa. Kuna ofisi za ardhi ngazi ya kijiji/mtaa hadi wizara ya ardhi hapa hapa, ni rahisi kwa mkazi wa Dar kufuatilia mwenyewe binafsi kimya kimya na kufanikiwa kutambua iwapo kiwanja kina mgogoro au la, huwezi kutoka mwanza leo kwa kutumia tangazo la jf moja kwa moja unaenda kununua kiwanja Dar! utatapeliwa tu, chukuwa muda na peleleza vya kutosha kabla.

Nadhani wengine waendelee kuchangia hatua za kufuatwa iwapo utaamua kununua chenye hati au kisicho na hati kwa manufaa ya sisi sote.

Mkuu nimekuita pande ile kwa ajili ya viwanja. Tuongee basi PM bhana
 

SUKAH

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
798
1,000
Mimi nimenunua viwanja vingi sana lakini kwa bahati nzuri sijawahi kutapeliwa japo nilishakutana na viwanja feki lakini nashtuka sasa basi mie utaratibu wangu wakununua viwanja ambavyo havijapimwa ni kama ufuatao:

1.Naenda kuangalia kiwanja chenyewe kama nitarizika napo

2.Naangalia kama kuna barabara ambayo iko well defined

3.Naagana na dalali namwambia anipe siku kama tatu hivi nipate pesa

4.Narudi baadae kivywanguvyangu naenda kuonana na majirani wote wa pande nne wanihakikishie kuwa kiwanja kiko ok na hakina tatizo na pia kama ni kweli ni cha huyo anayeniuzia.

5.Naenda kuonana na Mjumbe wa eneo hilo anihakikishie kuwa kiwanja hakina matatizo.

6.Naenda kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa nae napiga nae story kuhusu hilo eneo lazima ntapata data

7.Baada ya hayo naenda ardhi nachukua yule jamaa wa GPRS namlipa hela kidogo hardly 50,000/= anakuja na chombo chake anapima pembe zote nne za kiwanja anarudi ardhi anacheck kwenye master plan ananiambia kama hiyo sehemu imekua planned kama makazi au sehemu za public kama kanisa barabara n.k

8.Kama iko poa naenda serikali za mtaaa tunaandikishana na mashahidi wanakula 10% yao nimemaliza biashara.

Na kwa kutumia njia hii nimeweza kununua viwanja zaidi ya 10 bila matatizo yoyote matatizo yanayotokeaga ni madogomadogo tu kama jirani kamega kwako kidogo ambayo hayaninyimi usingizi.

Umetupata muongozo mzuri sana, shukran kwa hilo
 

kabungu

Member
Dec 1, 2013
9
0
Mkuu [/MENTION]Ureni[/MENTION] nakushukuru sana kwa maelezo yako ya kina kuhusu ununuzi wa viwanja na kwamba una uzoefu katika biashara hii kwa sasa. Binafsi ninataka kununua kiwanja lakini kwa sasa niko nje ya nchi na nina rafiki yangu yuko Dar es Salaam ananiambia kwmba eneo la Kigamboni kuna viwanja na ekari moja inauzwa kati ya Mil. 6-7 na nusu inauzwa Mil. 3-5. Ananiambia bei ni maelewano.

Siku kadhaa zilizopita nilimuunganisha na mdogo wangu waende katika eneo hilo la viwanja na akanihakikishia ardhi haina mgogoro wowote na iko sawa kwa manunuzi. Hata hivyo roho yangu imekuwa nzito sana katiika kufikia maamuzi.

Unaweza kunishauri jambo katika hili hasa ikizingatiwa sipo nchini na ninataka kumtumia rafiki yangu huyo kwa manunuzi. Tupanuane mawazo mkuu

Hiyo bei ndogo sana siyo kweli
 

Sword

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
864
0
Kuna sehemu nyingine inaitwa Gezaulole huko Kigamboni napo ni pazuri tu sema bei ndio sijui japo nahisi labda haiwezi kuwa ghali sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom