Njia rahisi ya kupata mtaji

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1573827828368.png

Changamoto kubwa ya watu wengi katika kuanzisha biashara ni mtaji. Kuanza biashara kuna mambo mengi sana, kuna kufanikiwa na kushindwa hivyo kuchukua mkopo banki wakati ndio unaanza biashara sio busara hii ni kwa sababu unashauriwa kuwa kabla haujaweka fedha zako kwenye biashara yeyote ile ni lazima ufanya utafiti wa kutosha na ujiridhishe kuwa itafanikiwa.

Zifuatazo ndizo njia za kupata mtaji

Akiba yako binafsi

Unapokuwa na wazo la kufanya biashara au kufungua kampuni anza kujiwekea akiba kwa ajili hiyo ili ikifika siku unaanza unakuwa na hela ya kuanzia. Anzia pale ulipo na endelea kukua kidogo kidogo. Pia hapa ni lazima ukumbuke ule usemi mtamu usemao haba na haba hujaanza kibaba.

Kila kitu unachokiona leo tambua na elewa kina mwanzo wake, hakuna kitu ambacho hukua kwa mara moaja, kila kitu huwa kinaanza kidogo kidogo kisha kinakuja kukuua, ukisubiri mpaka uwe na kiwango kikubwa cha fedha ndipo uanzishe jambo fulani kumbuka utasubiri sana.

Ndugu na rafiki wa karibu
Kama una mahusiano mazu na ndugu na marafiki ni sehemu nyingine unaweza kupata mtaji bila masharti magumu. Ni muhimu kuhakikisha mnapeana katika maandishi na makubaliano yanayoeleweka.

Upo usemi fulani usemao mficha nanii mara nyingi huwa hazai, acha kukaaa kimya kama unao uwezo wa kuomba msaada kwa watu wengine ambap wanakuzunguka, kama una shida ya mtaji usione aibu kuomba msaada kwa ndugu na jamaa ambao wanakuzunguka, kuona aibu kwako ndiko kutakokufanya uzidi kuona maisha haya ni magumu.

Mshirika Mwenza wa biashara (business partner)
Mtu ambaye ana ndoto kama wewe na yupo tayari kufanya kazi pamoja anaweza kuweka hela zake akawa na hisa kwenye biashara / kampuni yako. Ushirika huu ni mzuri ila unahitaji umakini wa hali ya juu.

Kama unacho kianzio fulani cha fedha unatakiwa kuto kuona aibu kumtafuta mwenzako mwenye wazo kama lako bali unatakiwa kujifunza ni kumtafuta mtu mwenye wazo kama lako ili muweze kujenga malengo yenu kwa pamoja.

Chanzo: Muungwana
 
Asante
 
Safi sana. Post imejieleza vizuri kabisa.

Ningependa kuongezea njia nyingine.

Kujiajiri kwenye vitu visivyohitaji mtaji
Mfano mmoja wapo ni mtandaoni, kuna vitu vingi unaweza kujifunza na kuvifanya mtandaoni bila kuingia gharama. Tembelea mtandao wa www.ajiras.com uone mifano ya vitu watu wanafanya alafu ingia google uone mafunzo ya kufanya hivyo vitu.

Utagundua kuwa inawezekana. Unaweza pia kujifunza vitu kama kupiga picha, alafu ukaanza kuiza huduma hiyo kwenye mtandao wa www.ajiras.com ambao kujiunga ni bure na wana kusaidia kupata wateja.

Angalau nenda uangalie ikibidi uliza maswali pale kwenye chat wata kusaidia.
 
Back
Top Bottom