Njia rahisi ya kuhamia Australia na Spain

Trueboy

Member
Jul 9, 2012
98
72
Habari wana jamvi , imekua ndoto yangu ya muda mrefu kutaka kusogea mbele kidogo na kubadilisha upepo wa bongo kutokana na factors nyingi tu ikiwemo ugumu wa maisha pamoja na uvunjifu wa demokrasia nk.

Nashukuru Mungu nimeweza kupiga hatua moja na kutua nchi mojawapo Asia kimasomo ila sitamani kuishia hapa.

Nimejaribu kuchimba chimba hapa na pale kujaribu kujua wa Tz au Wakenya huwa wanafanyaje kuhamia nchi za Europe na kupata Citizenship/Residentship ?

Katika tembea tembea zangu kwenye nchi za hapa Asia nilibahatika kukutana na dada mmoja mu-Argentina ambae anafanya kazi Australia kwa muda sasa ila alikua ametoka kwaajili ya kushughulikia VISA.

Nilijaribu kumuweka karibu ili kupata details za namna gani alibahatika na ana survive vipi Australia. Niliyoyapata kutoka kwake ni; Kuna kitu kinaitwa “Holliday Visa” aina ya visa ambayo inatolewa na Serikali ya Australia, wanavyosema unaweza apply na ukabahatika kuipata ila kuna vigezo kama uwe na pesa kiasi, uwe na barua ya mdhamini ambayo ndio kazi uliyoipata n.k

Ukiipata sasa unapewa miezi mitatu ya kufanya kazi na baada ya hapo unaweza renew na kupewa miezi mi3 pia , then baada ya kuisha mchezo unakua ni kutoka nje ku renew visa baada ya miezi sita na kurudi kupiga kazi. Na ni nchi nyingi za Europe pia huwa wanafanya huo mtindo, mtu anafanya kazi miezi 6 ana save then anaenda ku relax Nchi nzuri za Asia huko. Isitoshe pesa ya Australia ipo juu kithamani uki compare na nchi za ukanda wa Karibu na Asia.

Anyways nimeandika huu uzi ili kupata mchango wa mawazo , kukosolewa pia kuhusu njia niliyoambiwa hapo juu. Kama kuna mtu mwenye ufahamu zaidi please share uzoefu wako naamini kuna watu wana ndoto kama zangu.

PS: Namna ya ku migrate Spain nitaiweka hapa hapa kwenye uzi mwingine. Tupate mawazo juu ya hili la Australia kwanza. Nawasilisha.
===
KUHUSU SPAIN SOMA HAPA
 
Australia??! Kweli??!! Kuna ubaguzi na crime ya kutosha. Spain labda wana upendo kiasi ni open book lakini Australia sikushauri.
My opinion tu
 
Sijafanikiwa bado kufika Australia.

Ni pazuri pa kutafutia maisha. Zamani walikuwa wanaencourage immigration particularly skilled immigrants bila kujali unatoka kona gani ya dunia.Waliojua kutumia chance wanatumia.Kwa huku kwetu Africa walionufaika zaidi ni South Africans sababu ndo wapo wengi kule.

Huo utaratibu wa kutafuta skilled immigrants walishaacha.Nadhani ilichangiwa pia na pressure kutoka kwa wananchi walioitaka serikali iache kupokea wimbi kubwa la immigrants. Serikali nayo ikakaza kidogo. Kwa hivi sasa wanamfumo wao hivi(nimesahau jina) ambapo wanatoa list ya occupation zao wanazozihitaji kwa sana kwa mwaka huo.Sasa kama na wewe kazi yako imeorodheshwa pale unaweza kuapply hiyo visa yao.Hii ni kwa wale wanaotafuta kazi waishi huko.Kuna tozo zao pia utatakiwa utoe kwenye huo mchakato.

Kuhusu wages wanalipa vizuri mno.Nadhani kwa nchi wanazolipa vizuri wapo.Sarafu yao ni stable pia.

Kwa msaada na maelezo zaidi ingia kwenye website yao wameeleza kila kitu vizuri kabisa.

Sifahamu kitu kuhusu Spain.Hata kupaota bado.
 
Muendelezo....

Kwenye kila hustle huwa kuna vikeazo vyake , Baada ha kuelezea mawazo yangu juu ya namna mtu anaweza hamia Australia wacha niongelee niliyosikia kwa upande wa Spain.

Yafuatayo Ni maelezo pia niliyopata toka kwa mtu ambaye rafiki yake alishatumia hiyo njia. Ni Mtu wa Morocco ambaye sasahivi amebakiza muda mchache apate Residentship ya Spain.

Kuna njia inaitwa “Arraigo Social” unaweza itafiti zaidi. Hii imekaa hivi: kama unataka kufika Spain itakubidi ucheze na VISA yeyote ile either Tourist Visa au Esucation Visa , hii inakubidi uwe na senti kidogo na wengine hutafuta admission za vyuo na kulipia kiasi kama nusu semester n.k nia ni kupata visa tu.

Baada ya hapo ukishapata nafasi ha kuingia Spain sasa unakua mchakarikaji unatafuta kazi za kufanya na kazi ni nyingi ila za kawaida na pia kama una qualifications nzuri hnaweza bahatisha kazi nzuri. Sasa hapo inategemea kama utaweza kuendelea kusoma sawa kama utataka kufanya kazi tu sawa. Na pia ni vema kabla ya kutumbukia Spain uwe na ka connection ka kuanzia pamoja na Vihela kiasi (fanya research).

Then baada ya hapo unaweza ku overstay na kutafuta kazi , hio ni hata baada ya visa yako kuisha unaendelea kupambana na hakuna bugudha sana kama nchi zingine (kwa maelezo aliyonipa) , kwa upande wa Tourist visa ambayo huwa mara nyingi haizidi miezi Mi3 inakupa kipindi cha hiyo miezi mi3 cha wewe kutafuta pa kujishika, kutafuta kazi au connection. NB: Ni poa zaidi ukiwa na connection kabla ili mambo yakikaza una pa kujitetea au uwe na kanauli kakurudi ulipotokea.

Sasa baada ya kukaa kwa miaka mi3 either legally or illegally unakua qualified na hiyo “Arraigo Social” , hii imekaa hivi huwa wanaitoa kwa mtu yeyote aliekaa Spain kea miaka mi3 na zaidi.

Arraigo Social ina masharti yafuatayo;
1: Uwe umekaa Spain kwa muda usiopungua miaka mi3 ILLEGALLY.

2: Uwe una mkataba wa kazi , sasa inabidi uwe umejitetea na kupata kazi kwa muda huo.

3: Utatakiwa ku prove muingiliano wako kijamii na waSpain wenyewe , hii ina maana uwe na ndugu, jamaa, rafiki, jirani, mke, mme, mpenzi, au yeyote ambaye anaweza kuku backup.

4: Au pia kuna njia ya kufanya mtihani wa lugha ya Spain kama kigezo kimojawapo nadhani ni kama TOEFL au IELTS.

Kwa maelezo zaidi naambatanisha link pamoja na picha kadhaa za maelezo in details.

NB: Lengo la uzi huu na ule wa kwanza ni kuhabarisha ninayoyajua juu ya kutaka kuhamia nchi hizo mbili, nahitaji maelezo zaidi pia kea anae jua zaidi. Usikosoe tu weka inputs zako pia watu tuangalie fursa kwa upande huu.

Nawasilisha


9 Tips on How to Immigrate to Spain and Get Your Residence Permit

10d959fc-1bcf-453d-9351-f07eefa72c3a.jpg

7de64c91-0006-44a1-90b7-42d44ebe4553.jpg
 
Back
Top Bottom