Dumelang
JF-Expert Member
- Aug 11, 2011
- 3,203
- 5,704
Utafutaji wa Watanzania kwenda ulaya au nje ya nchi kutafuta maisha umekua kwa kasi sana hivi sasa. Thread nyingi sasa hapa JF zina watu wanaotafta kufika nchi walizodhamiria wakati mwingine wasijue watafikaje, tabu kubwa ni pakufikia na kupata mwenyeji. Leo nitasaidia kwa upande wangu katika sehemu hii ya kupata mwenyeji (host) kiurahsi kule unapotaka kwenda.
Uzi huu niliahidi kuuleta kutoka kwenye uzi mwengine (sio wangu) ulioletwa kama mada maalumu kwa wanaotafta ajira nje.
(baadhi ya watu nita watag kama walivoniomba kwenye uzi ule).
Twende sasa kwenye Mada
WORKAWAY - hii ni taasisi (Organisation) ya kimataifa inayowasaidia wasafiri waliotayari kufanya kazi za kujitolea nje ya nchi zao kwa kuwasiliana na mwenyeji katika nchi husika (mwenyeji aweza kuwa mtu binafsi, familia au kundi/kikundi cha watu).
Wale wanaosafiri kujitolea wanatarajiwa kutoa muda wao kule wanapoenda (kadri watakavyo kubaliana na mwenyeji wake) masaa kadhaa kwa siku. Huku mwenyeji akikupatia malazi na chakula. (Volunteer your time in exchange of housing and food).
Nadhani mnaanza kunipata tuendelee. Hawa WORKAWAY wanalenga wasafiri wenye kipato cha chini au wastani na wale wenye malengo ya kusafiri kujifunza utamaduni, lugha katika nchi waliodhamiria wakati huo mwenyeji akitarajia kutoka kwako mgeni usaidizi wako katika eneo analohitaji.
Baadhi ya nafasi za kujitolea zinahtaji ujuzi na nyingine hazihtaji ujuzi zipo nyingi kulingana na mwenyeji atakavyohainisha, kutengeneza bustani, kufua, kutunza wanyama, kulea watoto, migodini na usafirishaji nk nk.
Muda wakujitolea ni kulingana na makubaliano na mahtaji ya mwenyeji kuna wanaohtaji usaidizi hadi wa mwaka mzima.
Wazo hili lilianzishwa na David Milward mwaka 2002 alipopata changamoto za kuishi katika moja ya safari zake huko Hawaii mwanzoni mwa miaka ya 90.
Sasa unaanzaje? Hawa jamaa wana website (nitaiweka mwishoni) unaingia unajisajili. Katika kujisajili uta hainisha wewe unataka kuwa mwenyeji (host) au volunteer (mgeni wakujitolea).
Hapo utaanza kukutana na wanaotafta kujitolea na wanaotafta watu wa kujitolea.
Zipo nyingi na si za kusubiri hata sasa ukisoma tu site ile utaona wenyeji wakitafta watu wakujitolea.
Sasa kwanini nimeleta hii ni njia rahsi ya wewe kufika nchi unayotaka bila wasiwasi wa maradhi na makazi, ukijisajiri, tafta mtu anaetaka mtu wa kujitolea nchi uliokusudia. Wasiliana nae, kisha safiri, atakupokea na utakaa kwake buree na chakula bure kama nilivoeleza hapo juu, muda wako wa kujitolea ukiisha utatakiwa kurudi nyumbani.
Sasa ni vema ukatafta wale wanaotoa muda mrefu wa kujitolea kama miezi 8 mpaka mwaka. Hapa ukiwa pale eneo husika waweza jipatia uzoefu wakujua uanzie wapi kisha ubaki nchi husika.
Usalama: workaway wanakuwa watu wa kati kuhakikisha upo salama daima.
Uthabiti: hii taasisi ni halisi, waweza soma habari zake mpaka Wikipedia na anuani zake halisi, imefanya kazi tangu 2002
Mamilioni ya watu wamejitolea na katika website yao utakutana na successful story za kutosha.
Disclaimer : ila nawe wapaswa kujiridhisha na maelezo haya na uthabiti wao kabla hujachukua hatua. Mimi sio agent wala sihusiki vyovyote na workaway nimeleta kukusaidia wewe Mtanzania mwenzangu kufika nchi yeyote unayotaka kwa kujitolea tena kihalali.
Njia hii si kwa wanaotaka kwenda nje tu, hata wewe waweza kuwa host ukaomba watu kujitolea kuja Tanzania kukusaidia kazi yeyote, wewe ukiwahudumia mkazi na chakula tu. Pia shule na taasisi mbali mbali waweza faidika na na mfumo huu katika miradi inayohtaji ujuzi.
Kuhusu nauli na vitu vingine kama passport. Unatakiwa uwe navyo, mwenyeji (host) kazi yake ni kukupokea anakupa makazi na chakula. Vitu vyote hivi ataviainisha katika tangazo lake hata kabla hujaanza wasiliana nae.
Kukiwa na swali usisite kuuliza
Tembelea website yao hii kupata maelezo zaidi nakuona post zilizopo
Workaway.info the site for cultural exchange. Gap year volunteer for food and accommodation whilst travelling abroad.
Waweza kusoma pia Wikipedia maelezo zaidi. Workaway - Wikipedia
-Dumelang
...................
Daby STUNTER Kang agness s obedi ganja gal sherberry ghetopuzzle 24hrs G.25