Izato
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 5,414
- 11,610
Utumwa mamboleo (modern slavery) ni tatizo kubwa la kijamii na kiuchumi linalo wakabili vijana wengi waliohitimu vyuo vya elimu ya juu. Wahitimu wa elimu ya juu nchini Tanzania wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoathiri kupata fursa adimu ya kushiriki katika ajira rasmi, shughuli zakuaminika za maendeleo, na ustawi wao kwa ujumla.
Hii ni hali ambapo vijana wetu hawa wanalazimika kufanya kazi au vitendo fulani kwa njia ya udanganyifu, vitisho, au nguvu. Zipo aina anuai za utumwa mamboleo kama vile biashara ya binadamu (human trafficking); utumwa wa madeni (debt bondage); ndoa za lazima; ajira za watoto kwa unyonyaji; pamoja na watu kulazimishwa kufanya kazi bila malipo au kwa malipo duni sana.
Lengo la andiko hili ni kuangalia kwa undani kuhusu wahitimu wa elimu za juu kulazimika kufanya kazi bila malipo au kwa malipo duni sana. Hii hali kwa sasa imetamalaki na kugusa kundi kubwa la vijana huku likijificha katika sura ya kazi za kujitolea ndani ya makampuni na taasisi zenye kujiendesha kwa malengo ya kupata faida.
Kazi za kujitolea (volunteering) ni shughuli zinazofanywa kwa hiari kwa lengo la kupata uzoefu. Hizi kazi ni muhimu sana hasa kwa kujenga ujuzi na kuongeza uwezekano wa vijana wahitimu wa elimu ya juu kupata nafasi za ajira za baadaye. Ingawaje lengo zuri kutafuta uzoefu na, lakini matumizi yake ya kibiashara yanapaswa kudhibitiwa ili kuepuka unyonyaji maeneo mbalimbali ya kazi.
Licha ya uwepo wa faida luluki wa kazi za kujitolea ndani ya makampuni na taasisi zenye malengo ya kupata faida, lakini ya madhara makubwa hasa pale zinapotumiwa vibaya au bila mipaka sahihi. Haya ni baadhi ya madhara hayo:
a. Wanaojitolea hutumiwa kama njia ya kupata nguvu kazi ya bure, hii hupunguza haki za ajira rasmi na kugeuzwa kuwa fursa ya utumwa mamboleo.
b. Kampuni kutegemea kwa kiasi kikubwa wanaojitolea, hupunguza nafasi za ajira rasmi hivyo kuathiri ajira kwa rasmi vijana wengi waliopo sokoni.
c. Wanaojitolea wapopewa majukumu sawa na wafanyakazi wengine rasmi wanapoteza motisha, hujisikia kudharauliwa, au kutothaminiwa.
d. Makampuni huepuka majukumu ya kisheria kama vile, kulipa mishahara stahiki, kutoa bima ya afya, uhakika wa usalama kazini n.k.
e. Anayejitolea hawafungwi na mikataba madhubuti, akikatishwa tamaa kiwango chake cha uwajibikaji na ubora wa kazi kinaweza kushuka.
f. Ni wahitumu wachache sana wanoweza kumudu kufanya kazi bila malipo ama malipo duni, hali hii huongeza pengo la kijamii na kuwanyima wengine fursa.
Kazi za kujitolea kwa vijana waliohitimu elimu ya juu zinapaswa kuwa za muda mfupi tu katika mashirika ya kibiashara. Msukumo mkubwa kwa makundi ya wahitimu wa elimu ya juu kuingia katika aina hii ya utumwa inachagizwa na lindi la umaskini, ukosefu wa ajira, rushwa na udhaifu wa sheria za kazi.
Utumwa huu una athari hasi nyingi sana ikijumuisha kuvunjika kwa haki za binadamu, unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia, kukosekana kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kuongezeka kwa uhalifu. Ili kupambana na kadhia hii kunahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa serikali, vyama vya wafanyakazi, waajiri, na jamii kwa ujumla hasa kupitia maoni yapatikanayo katika majukwaa ya vijana.
Zifuatazo ni njia muhimu za kuweza kudhibiti hali hii.
a. Uwepo wa sheria za zinazotofautisha kati ya kazi za kujitolea na kazi za kulipwa, ambapo sheria kwa uwazi zizuie makampuni kutumia wanajitolea katika kazi zinazozalisha faida bila malipo stahiki.
b. Kuwepo na mkataba wa wazi unaoeleza majukumu ya mhusika, siku na saa za kujitolea, pamoja na mipaka ya mafunzo au uzoefu
c. Uwepo wa muda maalum wa kazi za kujitolea, mathalani ukomo wa kazi za kujitolea iwe kati ya miezi 3 mpaka 6
d. Uwepo wa posho zenye kukidhi haja, ikijumuisha usafiri, chakula, bima ya msingi. Kwa wahitimu wa elimu ya juu angalau malipo ya awali yawe ya kima cha chini kitolewacho katika sekta ya umma katika wakati husika.
e. Uwepo wa uwiano wa wafanyakazi rasmi na wale wanaojitolea, idadi kubwa ya wale wanaojitolea kuliko wafanyakazi rasmi huatarisha ajira rasmi.
f. Mamlaka husika zifanye ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha hakuna matumizi mabaya ya wanaojitolea na kuhakikisha haki zao za msingi zinazingatiwa
g. Vijana waelimishwe kuhusu mipaka ya majukumu yao ya kazi za kujitolea mahali pa kazi ili kuweza kutofautisha na zile za ajira rasmi, hii itawasaidia kuepuka mazingira ya unyonyaji.
h. Makampuni yahamasishwe kuwa sera nzuri kuhusu rasilimali watu (wakiwemo wanaojitolea)
i. Vijana wapate fursa ya kuwa wanachama wa vyama vya wafanyakazi wapate sauti ya kulinda haki zao za msingi na kupinga matumizi mabaya ya kazi za kujitolea
j. Ukomo wa ajira za kujitolea ukifika, vitolewe vyeti vyenye kuelezea ujuzi halisi walioupata, kuonyesha thamani zao halisi zao sokoni, na kupendekezwa kupewa ajira rasmi.
Hitimisho
Njia bora ya kupambana na madhara haya ni kuweka uwiano kati ya kupata uzoefu na kulinda haki za binadamu na ajira. Kujitolea kisitumike kama mbadala wa ajira rasmi bali kama nyongeza ya kujifunza. Uwepo wa ushirikiano kati ya majukwaa ya vijana wasio kuwa na ajira rasmi, vyama vya wafanayakazi, serikali na mashirika ya kimataifa kama International Labour Organization ndiyo njia muhimu na ya pekee ya kuweza kukabiliana na utumwa huu mamboleo.