Njia nzuri ya kupunguza gharama za ujenzi

moah

Member
Oct 2, 2018
58
59
Wakuu nipo katika mchakato wa ujenzi wa Nyumba yangu maeneo ya mile moja kibaha lakini Nina shauku ya kujua Sana njia ipi nzuri ya kupunguza gharama ya ufundi Kati ya kumtafuta fundi na kumkabidhi kazi na ukubaliane nae Bei au utafute mafundi uwalipe per day ipi inapunguza gharama wakuu.
 
Tafuta ramani yako nzuri, kubaliana na Fundi ukubaliane bei ya jumla Kwa pagale zima. Ila mkubaliane ya kuwa advance utampa tsh ngapi, baada ya msingi tsh kadhaa, akifikia level ya madirisha utalipa tsh kadhaa, linta tsh kadhaa na Yale Matofali ya juu ya kumalizia baada ya linta ni tsh kadhaa. Uwe mwaminifu katika kutoa hela pia. Nakutakia ujenzi mwema.
 
Safi...
 
Mkuuu the best Option ya kupunguza gharama za Ujenzi ni kujipa likizo ya mambo yako ikasimamia wewe mwenyeweeee Vifaa vya Ujenzi nenda kwa Wazalishaji wakuuzie kwa bei za jumla. Mf.Cement nunua mifuko yako 100 toka Twiga kiwandani, mabati nenda Alaf hapo Tazara nk at the end likizo inaisha umemaliza kazi. Note. Kumpa fundi fedha ajisimamie nyumba itajengwa chini ya kiwango hasa ratio ya Cement itakuwa poor ili fundi apate faida. So komaa nao mwanzo mwisho
 
Wakuu nipo katika mchakato wa ujenzi wa Nyumba yangu maeneo ya mile moja kibaha lakini Nina shauku ya kujua Sana njia ipi nzuri ya kupunguza gharama ya ufundi Kati ya kumtafuta fundi na kumkabidhi kazi na ukubaliane nae Bei au utafute mafundi uwalipe per day ipi inapunguza gharama wakuu.
Alafu siku ikikuangia ukiwa chumban na mchepuko wako usilalamike ukaanza kusema cement za siku hizi hazina nguvu.
 
Tafuta ramani yako nzuri, kubaliana na Fundi ukubaliane bei ya jumla Kwa pagale zima. Ila mkubaliane ya kuwa advance utampa tsh ngapi, baada ya msingi tsh kadhaa, akifikia level ya madirisha utalipa tsh kadhaa, linta tsh kadhaa na Yale Matofali ya juu ya kumalizia baada ya linta ni tsh kadhaa. Uwe mwaminifu katika kutoa hela pia. Nakutakia ujenzi mwema.
Pia naongezea kwa kusema hivi.Tafuta mafundi kama 5 wote waulize gharama ya kujenga hilo pagale ila uwe una uhakika wa kazi zao zipo vizuri.Pia vifaa usimpe fundi hela akakununulie yeye ahusike kukuandikia na uongozane nae na ikibidi tembelea maduka kama ma5 tofauti kuuliza kifaa kile kile chenye ubora na size ileile then fanya maamuzi.Huwa wanapangana na wauza vifaa vya ujenzi kwa kukuongezea bei then wanagawana baadae
 
Usiwalipe per day wanakuwa wavivu kazi itachukua muda mrefu wapate hela nyingi tena bila kuchoka.
 
Mbinu zangu!
Gawanya ujenzi kwa phases!
Phase 1: Fondation/kiti/msingi
Unapiga hesabu na fundi gharama na material husika na muda wataojenga. Unaomba ruhusa au unajipa ruhusa ya kile kipindi ili ushide site mwanzo mwisho mpaka phase 1 ikamilike.

Phase 2: Kupandisha kuta
Unaandaa gharama za hii awamu na unatafuta nafasi vile vile ya kuwepo site kwa siku zote asubuhi hadi jioni!

Phase 3: Kupaua, vile vile unaandaa mahitaji yote katika bajeti then unajipa muda wa kuyapata mahitaji na kusimamia site mwenyewe!

Phase 4: Finishing, vile vile kama kawaida unamalizia ujenzi wako tayari kwa kuhamia.

Urahisi au uzuri wa kugawanya kwa phases ni hautaumia kwa gharama tofauti na yule anayejenga bila mpangilio atakuwa anauhitaji wa fedha nyingi wakati mmoja bila mpaka na hivyo kuumia sana.

Kwa waajiriwa kugawanya likizo yako ya mwaka kwa wiki wiki kila baada ya mwezi au miezi ni rahisi kuipata kuliko kuchukua likizo nzima na unarudi kazini hujakamilisha ujenzi.

Pia kwa phases ni rahisi kwako ku-monitor gharama halisi na ujenzi wako tofauti na ukijenga bila mpangilio ambapo utahitaji mavitu meeengi kwa wakati mmoja.

Mwisho unakuwa na uhakika kujua nyumba yako mpaka lini itakuwa tayari! Mfano uliandaa bajeti ya kiti m4 pale pale kabla hamjatawanyika mnapiga hesabu ya kupandisha ujenzi so unajua wazi muda fulani nitakuwa na hii bajeti tutaanza kupandisha na hivyohivyo kwenye phases zingine.

NB: usisahau kuweka mlango wa dharura mkuu
 
1. Fanya uchaguzi sahihi wa fundi kwa kazi husika ikiwa ni pamoja na kupata rekodi yake ya utendaji na uaminifu
2. Fundi atoe hesabu yake pamoja na muda wa kukamilisha kazi.
3. Tafuta na linganisha gharama za mafundi kama watatu kwa kazi ya aina moja
4. Shirikisha mtu mwenye taaluma ya ujenzi katika kuweza kumtambua fundi anayefaa( Engineer au Architect)
5. Usimpe fundi pesa bila ya mkataba
6. Nunua vifaa kwa jumla
7. Hakikisha kuna usimamizi wa uhakika hasa kuhusu vifaa
8. Kuwa makini wakati wa ununuzi wa mbao za kupima kwa futi.
 
1. Chagua design rahisi isiyo na nafasi kubwa bila sababu, mfano size za vyumba ziwe za wastani
2. Epuka au punguza vibaraza vya zege na mapambo yasiwe mengi.
3. Kodisha baadhi ya vifaa au nunua vilivyotumika kama mbao za lenta nk.
 
Wakuu nipo katika mchakato wa ujenzi wa Nyumba yangu maeneo ya mile moja kibaha lakini Nina shauku ya kujua Sana njia ipi nzuri ya kupunguza gharama ya ufundi Kati ya kumtafuta fundi na kumkabidhi kazi na ukubaliane nae Bei au utafute mafundi uwalipe per day ipi inapunguza gharama wakuu.
Ukimlipa per day atakaa hata miezi ili aendelee kupata pesa zako, njia nzuri ni kumlipa kwa kazi mfano kupiga plaster utamlipa kiasi flani, hapo kazi itaisha haraka sana
 
Usiweke paa na usikate vyumba ili kuokoa matofali,bati na mbao....

😂 😂 😂 😂 😂 dah! we jamaa umetisha.
 
Back
Top Bottom