Mulokozi GG
Member
- Jul 14, 2021
- 34
- 44
Uwepo wa kila kilichopo semehu kilipo ni matokeo ya muunganiko wa mihimili kadhaa. Hivyo hivyo maisha ya binadamu katika hii dunia yanayo mihimili yake, moja kati ya mhimili wa mhimu katika haya maisha yetu ya leo unaotufanya tuishi tunavyo ishi ni uchumi.
Uchumi katika ulimwengu umekuwa nyenzo mhimu ya kuinua au kuangusha mtu au Taifa lolote. Katika mchakato wa kuinua na kuimalisha uchumi watu na Mataifa mbalimbali hutumia nyenzo tofauti tofauti, moja wapo ni mikopo au madeni.
Mwaka 2020 deni la Tanzania lilikuwa trilion 59 shilingi za kitanzania, serikali ya Tanzania ilitangaza hili kupitia bunge lake (Jamii forums, February 2021). Hizi siyo million au billion ni trillion, je ni nani anaidai Tanzania.!?
Kwa mjibu wa ukrasa wa visualcapitalist ripoti ya IMF iliyotolewa mwezi wa nane 2019 China ilikuwa na deni la trillion 6.8 dola za kimarekani, Uingereza ilikuwa na deni la trillion 2.5 dola za kimarekani, Marekani ilikuwa na deni la trillion 21.5 dola za kimarekani ( baadhi ya vyanzo na waandishi binafusi wanadai deni halisi la Marekani ni zaidi ya trillion 100 dola za kimarekani) na deni la mataifa yote duniani lilikuwa trillion 69.3 dola za kimarekani. Asilimia tisini ya deni lote lilikuwa katika mabara yenye mataifa yaliyo endelea kiuchumi.
Hivyo unaye waza labuda Mataifa yaliyo endelea ndiyo yanaidai Tanzania tu na hayadaiwi tafakari tena!.
Hivi umeisha wahi kujiuliza, nani anayadai haya Mataifa hizi trillion za pesa zinazo ongezekaga kila kukicha.?
Ukifuatilia chanzo na mzunguko wa pesa duniani kwa umakini itakuwa rahisi kuona kuwa taasisi binafusi na za kimataifa kama benki ya dunia(WB), IMF na benki nyingine kubwa duniani ndio waanzilishi na wakopeshaji wakubwa Duniani.
Maswali, je hizi taasisi za kimataifa kama WB na IMF mmiliki wake ni nani, kama serikali za Mataifa karibia yote duniani zinadaiwa?, hivi huyu mkopaji wa serikali za mataifa karibia yote duniani yeye pesa anazitoa wapi.?
Wanao kopwa(serikali) hawawezi kujichukulia wenyewe pesa wanapo zichukua wao(wakopaji) hadi wachukue wao wawakope?, hivi mwisho wa haya madeni ni upi?.
Madhala ya hii mikopo ni makubwa sana kwa binaadamu hasa wale wa kipato cha kati na kipato cha chini. Gharama za maisha hasa zile za mahitaji ya muhimu zinaongezeka kila siku, siyo kwa sababu thamani ya mahitaji hayo inaongezeka bali wenye dhamana ya usimamizi wa mahitaji hayo wanaongeza gharama ili kupata pesa ya kuendeleza mzunguko wa mahitaji husika.
Mfano, Tanzania mwaka 2013 ilikuwa na deni la trilion 27 shilingi za kitanzania(ukurasa wa demokrasia, January 2014). Hapa majukumu ya kila siku ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yalikuwa yanaendelea kawaida kutokana na kodi za Watanzania.
Kutokana na uhitaji wa miundo mbinu na mazingira yanayo endana na mabadiliko ya dunia(modernity) zilihitajika pesa za ziada ili kutekeleza maboresho hayo. Badala ya serikali inayo endesha shughuli zake kwa jasho la Watanzania, kutengeneza karatasi (pesa) zitakazo tumika kama nyenzo ya kutimiza mahitaji yake ilienda kwenye taasisi inazo zisimamia yenyewe(kama benki) kukopa na matokeo yake deni likaongezeka.
Deni lilivyo ongezeka serikali ilihitaji pesa(kodi) zaidi ili kuendeleza shughuli za kila siku na wakati huo huo ikifanya marejesho ya deni la nyuma na lile ililo liongeza, matokeo yake serikali ikapandisha kodi kwenye baadhi ya vitu kukidhi mahitaji.
Machakato huu unafanywa kwa kujirudia rudia kila linapo tokea hitaji lolote, huku madeni ya nyuma yakiwa yanazidi kuongezeka riba sababu ya malipo yake kutokamilika.
Hivyo mfumuko wa bei, ongezeko la gharama za maisha na umasikini kwa masikini ni suala ambalo halikwepeki ndani ya huu mfumo. Hata iwe serikali gani masikini wataendele kuwa masikini huku wakiongezeka na matajiri watazidi kuwa matajiri huku wakipungua. Sababu daraja/nafasi iliyopo kutoka kwenye umasikini kwenda kwenye utajiri ni kubwa, ndefu na inazidi kurefushwa kila iitwayo leo sababu ya huu mufumo unao tumika.
Unaweza ukajiuliza kama wengine wengi kuwa, je wanauchumi wetu hawaoni kuwa mfumo tunaoutumia sahivi una mapungufu mengi kiasi hiki!?
Jibu la hili swali na mengine mengi ya hivi ni jepesi. Mashuleni (formal education) wanafunzi hawajifunzi kile wanacho kitaka au kile kitakacho wasaidia bali wanafundishwa na kuaminishwa kile kilichopo kwenye shule na kwenye mfumo husika.
Kwahiyo wenye mamlaka zaidi kwenye mfumo wa elimu ndio wanao amua kipi kifundishwe na kifundishwe je?, wengine wote wanaitikia tu.
Sababu lengo kuu la kusoma au kupata elimu(kwa walio wengi) ni kuajiriwa, kupewa mishahara mikubwa n.k. Inakuwa ni vigumu kwa Jamii na wasomi(walio wengi) walio kesha wakikalili kile walicho pewa tu kwa ajiri ya mishahara kwa miaka zaidi ya 16 kubadilisha mtazamo wao na kuanza kusimama kwa ajiri ya masilahi ya wengi na jamii kwa moyo mmoja.
Katika uhalisia inaumiza na inashangaza kuwa njia ya kubadilishana huduma tuliyo nayo sahivi (pesa). Licha ya ukweli kuwa haina thamani yoyote ndani yake(intristic value), watengenezaji wake pia wanaitengeza kutoka hewani. Kwa maneno mengine inawagharimu sufuri(gharama ndogo sana) kutengeneza karatasi wanazo zipa thamani ya mabilioni ya rasilimali halisi za jamii ndani ya akili za watu.
Pia tupo ndani ya mfumo ambao leo hii watu wakiacha kukopa, pesa zote zinapotea ndani ya Taifa husika. Kwa maneno mengine ili karatasi yoyote iliyo chapishwa kama pesa iingie kwenye mzunguko ni lazima akopeshwe mtu hiyo karatasi (karatasi inakuwa na inabaki kuwa karatasi hadi pale tu anapo ikopa mtu). Madeni yote yakilipwa hivyo hivyo pesa inaisha katika mzunguko. Kwahiyo kwa njia yoyote wakopeshaji lazima wawashawishi, wawabembeleze au hata wawalazimishe wakopwaji kwa njia zilizo au zisizo halali madeni yaendelee kuwepo.
Kizazi cha binaadamu sahivi kinatumia nguvu na juhudi kubwa kuutumikia na kuuendeleza mfumo uliopo. Mbaya zaidi hizo nguvu na juhudi zinaishia kuwanufaisha watu wachache kama malipo yenye sura ya riba, kodi au mfumuko wa bei na kuacha wimbi kubwa la binaadamu wakitaabika katika Taifa, Bara na dunia hii yenye kila aina ya rasilimali.
Ni mfumo mwepesi lakini jamii inafichwa ukweli kuhusu mfumo huu katika njia na maneno ambayo siyo rahisi walio wengi kuyaelewa. Watu wanatumikishwa, Mataifa ni vibaraka, umasikini kwa walio wengi na machafuko vinaongezeka kwa manufaa ya wachache.
Njia kubwa maalumu zinazopaswa kutumika kutatua changamoto hii kwa gharama yoyote ni; Moja; kuwaelimisha watu na jamii juu ya mapungufu ya mfumo wa kubadilishiana huduma (monetary system), mbili; kupata viongozi majasiri na makini wanao uelewa huu mfumo na tatu; kutengeneza mfumo utakao wafanya Wanachi kuzifanyia kazi Nchi na serikali zao. Siyo kuzifanyia kazi taasisi binafusi (kufanya kazi, kulipa kodi ili kulipa madeni).
Hapa serikali zidai au idai mamlaka ya kutengeneza pesa zake yenyewe na kusambaza kwenye taasisi zenye mamlaka (kama benki) kulingana na uwezo au mzunguko wa Taifa husika.
Kwa njia hii serikali zitakuwa na uwezo wa kuendesha shughuli zake zenyewe na Wananchi watakuwa wanafanya kazi kwa ajiri ya Mataifa yao na siyo kuwafanyia kazi wakopeshaji wa Mataifa yao.