Njia 6 za kupunguza mionzi ya simu ya mkononi

josephmasamaki

Senior Member
Apr 27, 2011
163
84
Hakujawa na utafiti wa kutosha na wa muda mrefu kufanya hitimisho wazi kama mionzi kutoka simu za mkononi ni salama, lakini kulikuwa na data za kutosha kuwashawishi WHO juu ya uhusiano uwezekanao.

Simu za mkononi hutumia mionzi isiyo-ionize (non-ionizing radiation), ambayo haiwezi kuleta uharibifu wa DNA kama ambavyo ingeweza kufanya mionzi ambayo ni ionizing. Mionzi ya simu ya mkononi inafanya kazi kama microwaves zenye nguvu ndogo (low power microwaves), lakini hakuna mtu ambaye angependa hata kusogeza uso kwenye hizo low-powered microwave.

Kama WHO inahusisha matumizi ya simu kama "yenye uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu!!" Hujashtuka bado?! Vifuatazo ni baadhi ya vidokezo vya haraka na vya msingi vya kupunguza exposure.

1- Kuwa wired

Sio bahati mbaya kwamba simu nyingi huja na wired earpiece (yaani sehemu ya kuweka sikio ina waya au metali).

Wired headset moja kwa moja hupunguza exposure ya mionzi kwa sababu simu huwa mbali na mwili. Kila inch simu inapokuwa mbali na mwili hupunguza kiasi cha mionzi unayoweza kunyonya (absorb).

Wired headset bado husambaza mionzi kupitia waya - lakini ni kiwango cha chini sana, kama bado una wasiwasi, unaweza kununua bead ferrite katika maduka ya elektroniki (kama headset yako haina). Hii huunganishwa na waya na inachukua mionzi yoyote inayosafiri kwa njia ya waya, hivyo kupunguza kiasi kinachoingia mwilini mwako.
imagess.jpg images.jpg

Kwa lugha nyingine, kuwa wired, maana yake ni penda kutumia wires kama headset (earphone kwa lugha nyingine) kwa maongezi marefu, ili upunguze kiwango cha mionzi kinachoingia mwilini kupitia masikio (kichwa kwa ujumla)

2- Matumizi speakerphone (loudspeaker)

Hii inaweza kuleta usumbufu (kero) kwa watu hasa kama uko sehemu ya mkusanyiko wa watu. Lakini wataalam wanasema kwamba kutumia loudspeaker ni muhimu kwa sababu inaweka simu mbali na ubongo wako. Kumbuka Kila inch simu yako inapokuwa mbali na mwili wako inapunguza mionzi. Kwa mfano, kuweka simu inch mbili mbali na wewe hupunguza mionzi kwa kiasi cha mara nne, Magda Havas , profesa katika Taasisi ya Afya katika Chuo Kikuu cha Trent Ontario, Canada, anathibitisha hilo kwa CNN.


3- Usipende kuvaa Bluetooth earpiece wakati wote

imagesfg.jpg vdfd.jpg

Wireless Bluetooth earpieces zinakuweka kwenye hatari ya mionzi. Hata hivyo, inakuwa ni kiasi kidogo cha mionzi kuliko simu yenyewe.

Tatizo ni kwamba watu wengi huvaa vifaa vyao vya Bluetooth wakati wote. Na hii si nzuri

Kama unatumia kifaa cha Bluetooth wakati wa mazungumzo, badili kutoka sikio moja hadi jingine kila mara ili kuepuka mionzi kwa muda mrefu (long exposure). Kama huongei na simu kitoe kifaa hicho

4- Mionzi ya kuunganisha na minara ya simu (radiation hot spots)

Simu za mkononi hazitoi kiwango sawa cha mionzi wakati wote. Kwa mfano, simu yako hutoa mionzi zaidi wakati kuunganisha na minara ya simu za mkononi (connecting to cell towers).

Lakini simu iliyo kwenye mwendo (kama unapokuwa unazungumza wakati unaendesha gari/uko kwenye gari) daima itakuwa inaungisha na minara mbalimbali - na hii moja kwa moja huongezeka nguvu kwa kiwango cha juu kwa vile simu itakuwa inajaribu kujiunganisha na minara tofauti tofauti inakuwa kwenye coverage wakati huo. Mawimbi dhaifu (weak signal) pia husababisha simu yako kufanya kazi kubwa zaidi kwa kutoa mionzi mbali zaidi. Epuka kutumia simu yako katika elevators, majengo na maeneo ya vijijini. Utafiti unaonyesha simu hutoa mionzi Zaidi wakati wa kutuma (transmitting) kuliko wakati kupokea (receiving).

5- Soma manual

Wengi wetu hupuuza kusoma manuals zinazokuja na simu au vifaa vyetu, Lakini manual za simu huelezea kutokuweka simu karibu na kichwa au hata mfukoni. Apple iPhone 4 inasema ni vizuri kuweka simu mbali na mwili kwa inchi 5/8 wakati inatuma (when transmitting). Na BlackBerry Bold inasema angalau simu iwe inch 0.98 mbali na mwili wako wakati ikiwa katika matumizi.

6- Usizungumze, tuma message

Kama huhitaji kushikilia simu karibu na sikio lako wakati wote, tuma ujumbe wa maandishi (sms) au tuma email au ujumbe wa huduma yako kama una smartphone. Kwa njia hii wewe utaepuka kuweka simu karibu na kichwa kabisa.

Remember the general rule of thumb is that the smarter the phone, the more radiation
 
sikuhizi ukinunua simu za mchina wala hupewi manual book. Unafungiwa tu kama maandazi unaondoka.

kwa kweli the more the technology, the more the mazingira hatarishi.
 
Afu nilishasikia na hii ya kuzungumza na simu wakati IPO chaji na wakati iko low battery hasa iki onesha alama nyekundu kw (smartphone) n sawa hili mkuu
 
Je kuzungumza na simu muda mrefu hakuna madhara mkuu? Kwa mfn zaidi ya dk 5
Kaka kama nilivyoelezea hapo juu, kwa mazungumzo marefu ni bora sana kutumia headset au bluetooth devices nilizoelezea hapo juu! Siyo kwamba ziko free of emission ila ni kwamba inakuwa imepunguzwa kwa kiasi kikubwa.. Na pia loudspeaker ni njia bora kwa mazungumzo marefu ukiwa sehemu tulivu na unachokiongea sio confidential mfano uko mbali ba familia yako na unataka umsalimie kila mtu!
 
Afu nilishasikia na hii ya kuzungumza na simu wakati IPO chaji na wakati iko low battery hasa iki onesha alama nyekundu kw (smartphone) n sawa hili mkuu

Kiutafiti hakuna madhara wala uhusiano wa moja kwa moja na madai hayo..
Kumekuwepo na mifano mingi ambayo mingine inapotosha, mfano wa hivi karibuni ni ule wa kijana wa Mumbai, India. Ambapo ilisambaa message iliyokuwa ikidai watu wasitumie simu zao zikiwa zinacharge au hata kupokea simu kama ina low battery sababu (mionzi) radiation inakuwa mara 1000 zaidi.

Habari ya huyu kijana ililipotiwa na gazeti la Indian Express (unaweza kupitia habari yenyewe hapa.) Ambapo hiyo simu ilikuwa ni china-made (Mchina) na kesi nyingi za ulipukaji wa simu ni kwa simu au charger ambazo ni fake (faulty or counterfeit phones or charges) zinapotumika! Mfano unaweza pitia link hii pia ukajionea matukio tofautitoauti ya simu kulipuka! Lakini karibu yote utaona kuna madai ya matumizi ya simu au charger fake/faulty.

Ukweli ni upi?
Charger ya simu inafanya kazi ya kuchukua umeme ukutani ambao ni Alternating Current (A.C) ambao una nguvu kubwa (high voltage) na kuubadili kwenda kwenye Direct Current (D.C) ambao una nguvu ndogo (low voltage). Lakini kama charger inafanya kazi sawasawa hakuna high volt itakayokufikia mtumiaji wa simu.

Lakini pia kama system za charging hazina viwango au simu haina kiwango/ubora au baadhi ya part zake ni vimeo, then kuna kila sababu ya charging mechanism kutofanya kazi vizuri na hivyo kuleta madhara au hata kifo kwa mtumiaji. Na ukweli ni kwamba hii inaweza kutokea kwa kifaa chochote kilichochomekwa kwenye umeme mkubwa.

Lakini, kwa ujumla hakuna hatari ya moja kwa moja ya kutumia simu inayofanya kazi ipasavyo (properly) huku ikiwa kwenye charge na charging system iko ok. Otherwise tahadahri ni muhimu juu ya hili ili kuwa na uhakika na charging system kuanzia ukutani, charger na simu yenyewe.. kama huiamini sana ni bora usiitumie ikiwa charge. Ingawa kimsingi ni ngumu kukwepa kutumia simu ikiwa charge hasa kwa simu hizi za kisasa (Smartphones, Phablets, Tablets, Ipads etc) hasa kwa matumizi mengine zaidi ya maongezi (games, chatting, Kuperuzi JF etc..)

Kwenye upande wa low charge
Madai ya kwamba ukitumia simu yenye charge inayoishilia inasababisha kuongezeka kwa mionzi SIO kweli hata kidogo maana hamna utafiti wa moja kwa moja unaothibitisha hilo, ila ni kuwa signal inapokuwa hafifu (weak signal) ndo simu inatumia nguvu nyingi kuapata strong signal matokeo yake ni kwamba ina emit mionzi kwa wingi zaidi. Ndio maana katka maelezo yangu kwenye thread kuu nikasema sio vizuri kutumia simu kwenye maeneo ambayo hayana network ya uhakika. Pia kuthibitisha kama simu inatumia nguvu nyingi maeneo yenye network hafifu ni kuwa huwa inamaliza charge mapema zaidi ya kawaida.
There is no direct causative link between handset battery charge level and handset transmit power level.

 
Back
Top Bottom