Mheshimiwa, nakuomba ueleze kwa kina ni jinsi gani ulikwenda nje ya Tanzania na ni nchi zipi ulipitia au kuishi na ni mafanikio gani umepata.
Pili, unakosea unapojumisha kwamba wote wanaokwenda nje ya nchi wanakimbia nchi yao na kwamba hawana elimu ya kutosha, kwa hili natofauitana nawe na naona - "you have lost the plot".
Kuhusu "point" yako ingine kwamba watu wawe makini wanapokimbilia nje ya nchi, hii pia wewe hauko makini kwa kuzingatia hujaeleza ni umakini gani wewe uliufanza kabla ya kwenda nje ya nchi na ni vipi umekuwa makini kwa miaka 16 nje ya nchi.
Pia unasema katika nchi ulizotembelea hujaona kilicho kizuri kama vile vya nyumbani Tanzania, hapa nakuomba uwe "very serious" na kauli hii.
Sikatai kwamba kuna baadhi ya mambo ya kupamba Tanzania hasa Dar-es-Salaam, ili ionekane kwamba hio ndio Tanzania lakini watu wamekosa hata miundo mbinu mizuri ya hata kulela mazao yao kwenye masoko kwa muda unaotakiwa. Angalia "blog" ya Maggid Mjengwa utaelewa namaanisha nini.
Mwisho, hakuna anaekataa kwamba Tanzania alikozaliwa ni nyumbani kwake ila kutokana na utofauti wa mambo mazuri na mabaya kwa pande zote mbili bado mtu ambae anaruhusiwa kuishi majuu kihalali, ana uchaguzi kwamba ni wakti gani aje nyumbani iwe likizo tu au kuhamia kabisa.
Naomba kutoa hoja.