Watanzania wamekuwa wakimbilia nje kuhangaika na maisha maruri lakini kumbuka maisha mazuri yako nyumbani kwako- kwani wengi wao wanaokimbilia nje hawana kisomo kilicho makini na huishia mitaani na kujikuta kwenye matatizo makubwa mno
Nawaambeni watanzania wenzangu kuwa makini kabla huja amua kukimbilia nje
Mimi nimeishi nje ya nchi kwa takiribani miaka 16 sasa na sijaona kuliko kuzuri zaidi ya Tanzania nimetembea nchi zaidi ya 12
Bongo bado bomba Nyumbani ni nyumbani tuu
Papa kula nao
Kuna kipengele katika katiba ya Tanzania kinachosema kwamba "Mtanzania yuko huru kwenda mahali popote pale duniani ili mradi havunji sheria." Watanzania wengi walio nje wametumia kifungu hiki na hawakuvunja sheria yoyote.
Hii dhana yako ya kwamba "wamekimbilia nje" ni ya mwaka 47 sasa hivi tuko 2007 na mambo yote ni utandawazi (globalization). Mtu anayekimbia kwao ni muhalifu ambaye anaogopa kukamatwa kwa makosa aliyoyafanya. Watanzania wengi walio nje si wahalifu na ni wachapa kazi wazuri tu na baadhi ya nchi wanataka Watanzania zaidi wenye utaalamu wenye soko katika nchi.
Watanzania wenye elimu ya juu katika fani mbali mbali wamegundua kwamba kuna nchi nyingi hapa duniani ambazo zinahitaji utaalamu wao na mishahara ni mizuri kabisa inayokuwezesha kulipa gharama zako muhimu za kila mwezi na pia kuweka akiba au kuinvest baadhi ya mapato yako.
Pia Watanzania walio nje huwa wanakuja Tanzania kwa likizo na pia wana ndugu zao, jamaa na marafiki ambao huwapa habari zote zinazojiri ndani ya Tanzania, hawahitaji msaada wako kujua kama Bongo ni bomba au la. Kama mambo ni bomba inakuwaje Watanzania katika kona mbali mbali wameanza kuwazomea viongozi? tabia ambayo hatujawahi kuiona tangu tupate uhuru karibu miaka 46 iliyopita. Je kulikoni?
Waswahili wanasema, "bahati ya mwenzio usiilalie mlango wa wazi" hizo nchi 12 ulizopitia wewe labda hazihitaji fani uliyosomea hivyo ukawa unapiga lami tu, baadhi wameishi nchi moja tu na wanapeta kama kazi na matunda ya elimu yao wanayaona na wana vyeo vikubwa tu lakini wengi wao hawapendi kupiga tarumbeta ili kujisifia mafanikio yao.