Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,596
- 5,584
:smile-big: Kwa kinywa wasema...What are you trying to say?
My God is Jehova!
Umeshaanza na sentensi zako zisizoeleweka!:smile-big: Kwa kinywa wasema...
Imani bila matendo...? Simama katika kweli, nadhani Juma amekuelewesha vya kutosha ila kwa kuwa ulishaamini utakavyo ngumu sana kuukubali ukweli ndicho nilichokigundua kwako.:smile-big:
Mpendatz! uliyozungumza ni propaganda tu tena za kitoto.
Habari za Okech zipo nyingi na huwa zimekusanywa kwa malengo maalum kama hayo ya kuwachochea watu.Wewe mwenyewe hushangai kuwa habari zake zilirekodiwa kikamilifu na kuhifadhiwa hivyo.
Haya mashirikia ya Save the children,Mwezi na misalaba mwekudu moja ya kazi zao ni kuendeleza ukoloni na hayapo kuwasaidia watu.Zaidi ni kuwa mengi yanashiriki kuupiga vita uislamu.Kule afghanistan,Pakistan wanawachukulia kama maadui sawa na majeshi ya America ndio maana mara nyingi hutekwa na hata kuuliwa.
Mwanzoni mwa mchango wako hapo juu umesema
Mimi nadhani katika Afrika kati ya nchi zitakazokua na historia ndefu ya binadamu kumfanyia binadamu mwenzie unyama Sudan Kaskazini inaweza kuongoza. Hiyo hapo chini ni mifano michache tu. Halafu bofya "Lostboys". NATAKA WOTE MKUMBUKE MUNGU IBARIKI TANZANIA! .
Hakuna unyama mbaya wa kumfanyia mwanadamu mwenzako kuliko kumuwinda na hata kumla.Hivyo ndivyo eskimo wa Congo na sehemu nyengine za Afrika wanavyofanywa.Watekelezaji wa hayo ni wazungu na makabila mengine ya kiafrika.Hakuna mwarabu aliyeshiriki.Jee utakubali kuwa unyama haufanywi Sudan ya kaskazini kuliko kusini ya Afrika.
Angalia vipande hapo chini.
1. Besides a small number of so-called "wild" Khomani San Bushmen living their ancestral live as hunters-gatherers, a truly stone-age way of life, to which they have clinged for at least 20 thousand years, this traditional Bushman way of life is now very scarce, and becoming scarcer by the day. The Khomani San Bushmen have maintained their way of life against all odds, and yes, against many dedicated extermination campaigns! For many years the San or Bushmen were actually hunted as wild animals or "vermin"! Possibly by your forefathers or mine. White, Black and Coloured people, both together and separately, were involved in these exterminations, and there is ample historical evidence of this.
2.In South Africa, the Bushmen were hunted and killed by Nguni Tribes moving south in search of new grazing. The Nguni tribes like the Zulu and the Xhosa, originally came from central Africa and are not indigenous to South Africa. The poor Bushmen, used to living by hunting found the Nguni people's cattle very easy to 'hunt' and this obviously upset the Nguni people, and they retaliated by hunting the Bushmen. As the Bushmen fled the advancing Nguni tribes, they met the European trekkers and farmers moving north, also in search of grazing. The Bushmen hunted the European's cattle and oxen which they didn't take lightly either. Bushmen hunting parties were organised. Both the Nguni tribes and the Europeans, did not view the Bushmen as being human beings. They thought they were animals, something like the missing link. This forced the Bushmen to move into and adapt to the dry, more desert-like areas, of Southern Africa.
Ukipenda unaweza ukasoma zaidi hapa.
na huyu mnaweza mkaendelea bila ya kumtaja 'Juma' mbona siku nzima mme elewana bana, kwenye mi thread yote mliojibizana acheni zenu.:smile-big: Kwa kinywa wasema...
Imani bila matendo...? Simama katika kweli, nadhani Juma amekuelewesha vya kutosha ila kwa kuwa ulishaamini utakavyo ngumu sana kuukubali ukweli ndicho nilichokigundua kwako.:smile-big:
Umeshaanza na sentensi zako zisizoeleweka!
Hebu eleza hapo:
1. Imani bila matendo inaingiaje nawe hunijui?
2. Ukweli upi unaouzungumzia?
3. kipi Juma kanielewesha?
Sudan haijauwa watu kama inavyofanya Marekani na umoja wa mataifa ya Ulaya magharibi-NATO.Hawafanyi hivyo kwenye eneo moja tu bali nchi zote za waislamu.Wanavunja miundo mbinu na kuangamiza mazingira.Kwa vile wanaouliwa ni waislamu sijakusikia ukilaumu.
Ukiwapongeza watu wanaojitetea hadhi zao za kibinadamu na kwamba hawawezi kutulia mpaka wahakikishe kuheshimika kwao naamini uko pamoja na mashujaa wa kiislamu wa Iraq,Taliban wa Afghanistan na Hamas wa Palestina.Ikiwa si hivyo basi hujui unachokisema umekuwa kama kasuku tu.Huwezi kuaminika hayo unayoyaeleza kuhusu Sudan.Ni ukasuku tu unaoukufanya uandike.
Mimi ninachotaka ni uweze kupanua wigo wako wa kufikiria kwa mapana zaidi. Hiyo historia ya bushmen mbona umeiamini na mimi unataka nisiamini kitu ambacho wamesimulia wahusika wenyewe? Nimeshasema nimekaa sana Sudan, naielewa sana haswa Darfur. Ninachoongelea nimekiona kwa macho. Nimekihisi ndani ya damu yangu.
Ukizungumzia Western countries kuwa na interests zao, that is true, it has always been like that, hata vita ya Afghanistan walishakaa upande wa Taliban wakiwapa silaha na mafunzo na leo ndiyo hao hao wanawachapa. Na amini usiamini hata huko Darfur wanazo interests kibao. Ile sehemu inasemekana ina Uranium deposits nyingi sana. Kuna mawili kuwa wanaogopa kuwa itatumika vibaya na zaidi kuwapiga, haswa kwa kuona mambo yanayotokea Iran nk. au wanaitaka pia.
Lakini ninachotaka ulelewe ni kuwa sisi tubishe tusibishe watu wa Kusini mwa Sudan wanahamu isiyoelezeka ya kujitenga na Kaskazini. Na katika maongezi yao yote nia yao ni kujiunga na nchi zetu za Afrika Mashariki. Hayo ndiyo maongezi yao halisi ya kila siku. Tatizo kubwa la mawaidha yako ni pale yanapoegemea zaidi mambo ya udini. Mtu ambaye amelewa dini huwa haelewi wala hafikirii mawazo ya mtu mwingine ambaye anawaza bila nia ya kutetea dini yake. Hili ndilo tatizo ninaloliona kwako. Wengi wamajaribu kuchangia kwa kuonyesha kujali zaidi maisha ya binadamu ili kukutoa kwenye hilo pazia au niuite 'ukungu' lakini umeshindwa kutuelewa.
Ninaikumbuka hotuba moja ya Mwalimu aliyosema aliwahi kualikwa kwenye sikukuu ya Wakristo akawaambia Serikali ya Tanzania haina dini, Maaskofu kwenye ile sherehe kusikia hivyo wakahamaki Yesu wangu! Halafu akaalikwa tena kwenye sherehe ya Waislamu nao akawaambia hivyo hivyo napo Mashehe wakaruka Astakafir lah!. Unafikiri alikuwa anafanya utafiti gani hapo? Hapo alikuwa anatuelewesha jinsi ambavyo dini inalewesha haswa pale ambapo haitumiki inavyopasa.
Ukisoma historia ya Elimu ya sayansi ilivyoanza utawaonea huruma wakina Galileo Galilei, walipotangaza kugundua mambo kisayansi walitengwa na kanisa. Waliitwa makafiri wakanyanyaswa sana na jamii yao ya Kikristo. Hilo lilitokea kwa kuwa wakati huo ilikuwa hakuna kingine zaidi ya dini. Watu walitakiwa kuzungumzia mambo ya dini tu kwenye maisha yao. Sasa na leo pia Ami ndiyo unatutaka tuwaze kama wakati wa kina Galileo? Haiwezekani hata chembe! Mtu anatakiwa aibebe Dini yake moyoni mwake, ifungashe ndani ya roho yako ndipo watu wataiona kwa matendo yako yatokanayo na ulicho nacho moyoni mwako. Kinyume chake ni kuuana tuu tukisingizia dini.
Hayo ndiyo mawazo yangu.
Nadharia yako unayotuletea hapa inafanana kabisaa na huyo mama. Are you related?Ipo sababu ya kutokuiamini hadithi yako ya Ajak Dau Akech.
Sisi katika dini yetu hatuukubali ushahidi wa mtoto mwenye umri kama wa Ajak wa miaka 8.
Mimi binafsi kuna vitu ambavyo nakumbuka niliwahi kusimulia nikiamini ni kweli.Nilisema nimemuona jinamizi nilipokuwa na umri kama huo.Hii ni kwa vile daima tulikuwa tukitishana na wenzangu kuhusu mdudu huyo.Hivi sasa nikikumbuka najuwa sikumuona kweli.
Mtoto mdogo kama yeye anawezaje kutofautisha makabila ya watu kwamba huyu ni mwarabu na huyu ni kabila jengine.Kumbuka rangi za watu na mavazi Sudan haviwezi kutumika kama kigezo cha kumjua mtu kabila lake.Halafu katika hadithi yenyewe kuna ladha kamili ya maneno ya kutiliwa mdomoni mwake na mafisadi wa kizungu wakristo.
Unamkumbuka mwanamke huyo hapo chini?.Huyo ni Ayaan Hirsi Ali ,tapeli aliyewahadaa wazungu wenye kupenda matusi kwa uislamu na akaweza kupata vyeo vikubwa katika serikali ya Nertherlands.Yeye ni mwenye asili ya kisomali.Ili kujipatia faida ya kidunia aliamua kuutukana uislamu kadiri alivyoweza.Wazungu wakamuona mtu wa maana na kumkumbatia.Hatimaye ilipogunduliwa kwamba wamedanganywa bunge na serikali vikavunjika.
Kwa malengo yao na kupenda kuupiga vita uislamu hadithi za Akech huchaguliwa na kutumika muda ukifika kama huu wa kura ya maoni ambayo wao ndio waasisi wake.
Kuna taarifa kwamba shirika la msalaba mwekundu lilisaidia kufanikisha mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwakimbiza wazanzibari wenye asili ya kiarabu huku wenyewe wakidhani wameokolewa na shirika hilo.Hii ndio sababu inayofanya Kiswahili nchini Oman iwe ni lugha ambayo kila unapokwenda utaizungumza.
Kukaa kwako Sudan hakukufanyi ujue kila kitu kinachoendelea humo.
Jiulize CHADEMA ambao ni watu wa humu humu walivyotiwa mkenge na CCM katika uchaguzi uliopita.Kabla uchaguzi haujafanyika walikosa viti na kubaki kuduwaa tu.Wana jamii forums walijitia kujua sana na kutoa takwimu nyingi kumbe nyingi za kudanganyana wenyewe kwa wenyewe.
Maalim Seif ni makamo wa kwanza wa rais huko Zanzibar.Kuna mambo ya uchaguzi yaliyofanyika ndani ya jimbo analoishi na amebaki kushangaa tu,itakuwa wewe mgeni wa kupita huko Darfur?.
Nyerere kama Marekani hawapaswi kufanywa rejea ya jambo lolote la maana.Wameshindwa na kudanganya sana katika uongozi wao.
Perhaps there is some truth kwa yule aliyesema kwamba "religion is the opium of the poor".
kuanzia mwaka 1956 mpaka leo, hakuna kiongozi wa Sudan ambaye amewatendea haki raia wa Sudan kusini..kuanzia kwa Gen. Abood, Nimeir, Al Mahd na Bashiri mwenyewe..wamewanyanyasa sana raia wenzao wa kusini. Jamani kwa kweli nitafurahi sana nikiona Sudan ya kusini inaondoka kivyake kutoka kwenye utawala wa Khartoum. Hapana, lazima tufike mahali tutetee utu wa binadamu mwenzetu especially mwafrika. Hizi dini zisituzibe nyuso na macho.
Huwezi kuwa mkatoliki bora zaidi ya Papa kiongozi wa Vatican.
Ami's hero!
Ami, nadhani hujafahamu maana ya uwepo wa JF ndiyo maana unashindwa kutuelewa. This is where we dare! Hiyo habari ya huyo mama ni yako umependa kuileta hapa japo haina mantiki kabisa kuja hapa, haitabadilisha mawazo ya watu waelewa hapa JF kwamba referendum ya Sudan ni makosa kuwepo. Na ningependa uelewe wazi kuwa ninapojadili jambo hapa sifanyi hivyo kwa ushindi, la hasha ni kutoa mchango wangu wa mawazo. Kama wewe upo kwa ushindi basi nakutangazia "UMESHINDA!!!".Mimi sina uhusiano na huyu mama
unaposema tunafanana .Fafanua
Usipofanya hivyo nachukulia umeshindwa na hoja za kuendelea na huu mjadala.
Ama kweli kaazi kweli kweli!
Ukiristo kaleta Mzungu, Uislamu kaleta Mwarabu! Wajapani, Thailand, China n.k wamebaki na Imani zao..mnaona walipo sasa?
Ni Africa tu tulikataa imani zetu za jadi..tukaambiwa za Kishenzi na tutakubali!!! Leo hii tunashabikia imani ambazo mara nyingi zimezeta vita na taabu kwa ubaguzi kwa watu badala ya kufanya dunia yetu pawe mahali bora zaidi!
Let us think kwa mapana zaidi Waafrika wenzangu!