NJAA YAJA: Dear Mr. President, On a Serious Note...

Hapa nimekubaliana nawe mkuu,Sisi tupo hapa kwa ajili ya masilahi ya watanzania kwa ujumla na sio kupinga sirikali.Siku itayofika sirikali yetu ipo swafi kabisa basi hapa utaanza kuona mapongezi kwao au siyo wajameni...so twende kazi
 
mwanakijiji usianze kuwatisha watu. Tunachokitengo cha Maafa katika ofisi hii, na kinajiandaa kwa lolote litakalokuwa. Mzee anafahamu matatizo yaliyoko nyanda za juu kusini na wiki chache zijazo utatangazwa mkakati wa kujiandaa na tatizo la chakula na njaa.

asante.
 
Food prices to surge higher, UN report warns
Last Updated: Friday, April 11, 2008 | 12:51 PM ET Comments20Recommend37CBC News
Price controls, tariff reductions and export restrictions have done little to offset dwindling reserves of rice and wheat around the world, according to a UN report released Friday.

'People are dying because of their reaction to the situation. People will not be sitting dying of starvation, they will react.'
—Jacques Diouf, Food and Agriculture OrganizationAccording to the Rome-based Food and Agriculture Organization, strong cereal demand in the last two months has driven up prices significantly. By the end of March, wheat and rice prices had doubled from the previous year. Maize prices jumped by one-third, according to the report.

"All indications we have is that this is not a short-term effect … where the first year you have price increases and the following year there is an increase of supply that brings the prices down," FAO director general Jacques Diouf said at a news conference.

Protesters riot in Cameroon, Egypt, Haiti
Within the past month, rising food prices have sparked riots in Cameroon, Ivory Coast, Ethiopia, the Philippines and Haiti. The UN noted troops in Pakistan and Thailand were deployed to guard against theft from farm fields and warehouses. In Egypt this week, where prices of cooking oil and rice have doubled since January, thousands of protesters took to the streets. One person died in the two days of rioting.

"People are dying because of their reaction to the situation. People will not be sitting dying of starvation, they will react," Diouf said.

The Crop Prospects and Food Situation report estimates that world cereal production in 2008 will rise 2.6 per cent to 2,164 million tonnes. Meeting projected targets would relieve the current food shortage, though the UN agency says the outlook is precarious.

"Any major shortfalls resulting from unfavourable weather, particularly in exporting countries, would prolong the current tight market situation; contribute to more price rallies and exacerbate the economic hardship already facing many countries," the report said.

Wheat production in Canada to rise 11%
The report said wheat production in Canada is expected to increase 11 per cent in 2008 over the previous year, owing to wheat's lucrative status.

"Current high wheat prices are expected to be a strong incentive to recovery in the wheat area," the report said.

"However, rather than reversing last year's shift, a further expansion on 2007's already relatively high oilseeds area is also expected because of attractive returns in this sector."

The UN report noted food inflation is hardest on developing countries where food represents as much as 60 to 80 per cent of consumer spending. By comparison, food accounts for 10 to 20 per cent of consumer spending in industrialized countries.
 
Kilimo Cha Kufa Na Kupona​
​
Ni kweli kuna hali ya kupanda vibaya kwa bei ya chakula duniani. Dunia imekuwa ndogo; chakula tutakachovuna siku za karibuni, hasa mchele, kitahitajika na watu wa nje vile vile.

Kuna haja ya kuangalia mbele, na kuwa na akiba ya chakula cha kutosha. Hakutakuweko njaa kubwa mwaka huu. Kuna mafuriko, lakini sikumbuki sisi kupata njaa kubwa kutokana na kuzidi mvua: mafuriko yakipungua kidogo mazao mbalimbali yataota haraka haraka kwenye udongo wetu mzuri.

Sina hakika kama akina Mizengo Pinda wako equipped kuona hatari iliyoko mbele yetu. Inabidi kupanga kupata chakula kingi, kukinunua na kukihifadhi kwenye maghala ya taifa. Huu ni wakati muafaka kwa Rais kuzunguka kila mahali nchini kwetu, akihimiza KILIMO CHA KUFA NA KUPONA.

Nakumbuka mwaka 1974, nikiwa mwanafunzi Mkwawa Most High School, Mwalimu alivyokuja Iringa na kumwambia kila mtu “tusipolima tutakufa”. Taifa lilimwitikia kikamilifu: Kila mahali, vitalo vya maua viligeuka vitalo vya mahindi. Kila mtu, hata mpangaji tu, alilima mahindi mbele na nyuma ya nyumba yake.

Can JK rise to the challenge? There is a real challenge here. Lazima kila mtu (including ministers) alime. Jioni baada ya kazi, na siku za wikendi, watu washughulikie vitambi vyao, sio kwa kula nyama choma tu, bali kwa kwenda vibustanini mwao na kulima. Asiyelima afukuzwe kazi. Si vema kufanya mzaha wakati huu. Kuna mabadiliko makubwa yanatokea duniani. Ni kweli kwamba tunaingia kwenye kipindi cha “Tusipolima tutakufa”.
 
🙂 🙂 😀 Pundit, YOU ARE ONE FUNNY............F....., i assure you, this is one of the fewest posts that i have had the loudest outburst of laughter from reading it..... absolutely sick mad...... lol, metaphorically you somewhat penetrated my cranium and managed to set off part of my brain that constantly feed on this kind of Armageddonian cogitations as it was just about to snooze. 🙂
 
Mwkjj, hiyo $500billion (sijui million) waliyo itaja jana kwa ajili ya chakula duniani wataigawa vipi..... marekani kama ilivyokawaida, naona wameshatoa fungu lao, ambalo litaonekana kubwa kuliko nchi au benki kuu ya dunia yoyote... lakini ukiweka uwiano na uchumi wao... (nafikiri) litakuwa dogo kuliko nchi nyingine nyingi....


Source: http://allafrica.com/stories/200804040246.html

Source: http://www.theglobeandmail.com/servlet/story/RTGAM.20080414.wfood14/BNStory/International



SteveD.
 
Mwnaakijiji kama utarudi home urudi na tractor utafute shamba ukalime!
 
Msolla alishindwa kusimamia watoto 29 pale Ukraine.... wakaishi bila chakula katika baridi la Kiev... hivi huyu ataweza kusimamia maisha ya watu karibu milioni 40? Nawahakikishia mwaka huu tutasikia watu wengi wakifa na njaa! yapigieni mstari maneno hayo. Msolla kama Mungai kabla yake hawezi kusimamia maslahi ya watu zaidi ya mmoja!
 

Dada kama uijui Tanzania vile ujawahi kusikia Musoma wanashindia maembe ka msosi wakati kilombero wana mpunga unamiaka kumi wanamwaga, sasa huu ni wakati ambao chakula kipo lakini hakipatikani na kitengo hicho hicho cha maafa kipo sasa kama chakula hakitakuwepo itakuwaje.
Hicho kitengo hakifanyi kazi sahihi kwani wanategemea mkuu wa mkoa na wilaya wawaletee data wakati wakuu hao hawataki kuonekana hawafanyi kazi kiasi kwamba kuna njaa kwenye mikoa yao. siasa zimetawala zaidi kazi zetu za kila siku badala ya utendaji.
 
NJAA YAJA, BEI YA MAFUTA JUU, tuna mpango gani? Tafadhali Rais Kikwete liandae taifa sasa huko tunakokwenda ni giza..!!! Wenzetu mmeshiba msiwasahau wenye njaa. SGR should be full; akiba ya mafuta iwe imejaa; chakula kianze kusogezwa mikoa ya kusini na pembezoni... mtandao wa misaada uwekwe tayari sasa. Tusije tukawa kama wale wanawali kumi!!
 
katika mikoa ambayo hawajafanya upandaji, serikali kuu iziamuru serikali za Mitaa ziwashawishi wananchi(siyo kimabavu maana wakati mwingine vijijini watu wanatendewa mambo ambayo hastahili binadamu kutendewa) wapande chakula(kwa dharura) hata kama kikawaida hawapandi katika nyakati hizi.

mazao yenye kuhimili ukame kama vile muhogo yahimizwe
 
NJAA YAJA, BEI YA MAFUTA JUU, SGR should be full; akiba ya mafuta iwe imejaa; chakula kianze kusogezwa mikoa ya kusini na pembezoni... mtandao wa misaada uwekwe tayari sasa. Tusije tukawa kama wale wanawali kumi!!

Maghala yapi? Si tulishauza/kuyatelekeza zamani. Vihenge (silo)nazo ni hivyo hivyo.

Matanki! Nenda pale TIPPER uone yanavyooza baada ya kutelekezwa kitambo. Sidhani kama nchi tuna sehemu ya kuhifadhia mafuta. Kwanza hio strategic reserve ya mafuta ni msamiati mpya na haipo kwenye policy au utekelezaji wo wote.
 
CCM na Lipumba sijui mmesikia!? Njaa...watu wataandamanaje?
 
Taifa lisilojiandaa kwa majanga, linajiandaa kwa maafa. Rais Kikwete aitishe kikao cha dharura cha baraza lake na wadau wengine (wafanyabiashara n.k) ili kwa pamoja wapange mkakati wa kupigana na njaa. Hakuna adui anayedhalilisha utu wa mwanadamu kama njaa..

chonde chonde...!
 
Ahsante mkjj, ni kweli tupu sisi tulio huku ndo tutakao kufa na njaa wakati ninyi huko mtakula na kushiba. Napendekeza kwamba tuwasaidie wananchi wetu kuhusu jambo hili. Tahadhari itolewe na elimu ya kuhifadhi chakula itolewe pia la sivyo tutajikuta pabaya.

Gembe umeelewa!?
 
msongoru, usidhani watu walioko majuu hawakabiliwi na njaa hiyo hiyo. Hata hapa (US) chakula sasa kinapanda bei na mafuta ndio usiombe.

Wenzetu hata hivyo wana mtindo wa kujiandaa mapema kweli na wana kila aina ya misaada kuhakikisha watu wanapata chakula. Na serikali yao haisiti kuingilia kati uchumi wa soko na kuhakikisha chakula kinapatikana.

Sisi tumeng'ang'ania mafisadi tu wakati hatari kubwa inayowakabili Watanzania sasa hivi ni njaa inayotweza.
 

Mwanakijiji,

wenzako huko labda wanaombea njaa ije ili wahonge vizuri vibaba viwili vya unga kwa kura mwaka 2010. Haiingii akilini kama hakuna mipango mahsusi inayofanywa sasa hivi ya kushughulikia hili.

Kama kawaida ya JF, tumewaonesha njia na wanaopondea kuwa hapa JF ni kijiwe cha kulalama (Mama balozi wa kule UK) inabidi wasome vitu kama hivi.

Asante kwa kuonyesha njia.
 
naona hapa kwenye cnn south africa wanaandamana kuishinikiza serikali ifanye kitu kuhusiana na bei ya vyakula kupanda, na pia nadhani mnakumbuka wiki mbili hivi zilizopita huko Haitiwatu walipigana mitaani kwa sababu ya misosi kupanda bei. sasa sijui kwetu hali itakuwaje
 
Watanzania tumezoea kuishi in the "now" kiasi kwamba hatufikiri muda mrefu baadaye.

Sasa hivi mtu unaenda sokoni unapata chakula cha leo, yamekwisha. Binafsi naamini watu watakaopata shida sana ya chakula watakuwa ni Dar kwenyewe kwani wengi wanategemea chakula kutoka mikoani.

Sasa mwaka huu "ompunga" toka Kyela hakuna na nafaka nyingine zikawa za shida. Itakapotokea kuwa kuwa mikoa ya pembezoni na nchi jirani zinaanza kufa njaa na mikoa yetu yenye kuzalisha chakula itakapoanza tena kuuza chakula nje, ndipo viongozi watapiga marufuku kuuza nafaka nje.

Matokeo yake ni mgongano wa uchumi wa soko, usalama wa chakula na mahitaji ya kipato cha watu wetu.

Sasa tufanye nini:

a. Serikali ifute kodi za mazao ya chakula karibu yote ili watu waweze kuagiza chakula kwa wingi.

b. Idara ya Maafa ya Waziri Mkuu waanza mara moja kutembelea maghala yetu ya Taifa na kuhakiki ni kiasi gani cha nafaka na vyakula tulivyonavyo na vinaweza kuhimili kwa muda gani.

c. Pindi mvua zikianza kupungua au maeneo ambayo hayana mvua kubwa kwa kuangalia hali ya hewa tuanze kusogeza chakula karibu na maeneo yanayoweza kuathirika. Tusisubiri hati tusikie "mahali fulani watu wanakufa njaa" halafu ndio tuanze kuomba misaada.

c. Naamini tukipanga vizuri hatuhitaji msaada wa senti hata moja kuweza kuwalisha watu wetu. Jifunzeni wakati wa Nyerere na hatua alizochukua kuepusha nchi na njaa mwaka 1962, mwaka 74, na mwanzoni mwa themanini. Msiache watu wetu wadhalilike kwa kukosa Chakula.

Chonde Chonde...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…