Nizinusheni wakuu wa luhga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nizinusheni wakuu wa luhga

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by WANGU MTENZI, Jul 9, 2012.

 1. WANGU MTENZI

  WANGU MTENZI Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lahaja ya Kiunguja ndiyo ilo sanifishwa kuunnda Kiswahili kulingana na historia yake.Kulikuwepo na lahaja nyingine nyingi ikiwemo;Kimvita,Kijomvu,Kimtangata n.k.Ni sababu zipi hasa zilizochangia kupendekezwa kwa Kiunguja?
   
 2. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  lahaja = dialect.


  Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainika kijamii au kijiografia. Lahaja za lugha moja zatofautiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati.

  Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi na siyo lahaja. Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la isimujamii.


  Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo:


  vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu)
  vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika (k.m. lahaja maarufu)
  vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka)
  vipengele vya eneo (kitarafa)


  Mfano wa lugha yenye lahaja mbalimbali ni Kiingerezana lahaja zake zinavyozungumzwa tofauti Uingereza, Marekani, Uhindi, Australia na maeneo mengine.

  Tena, lahaja za Kiswahili hutofautishwa kulingana na maeneo yake kama Kiamu (kisiwani kwa Lamu), Kimvita (mjini kwa Mombasa), Kiunguja (kisiwani kwa Zanzibar, Kingazija (visiwani kwa Komoro) na kadhalika

  ==

  Lahaja za Kiswahili


  Kiswahili kimepatikana kwa namna au lahaja mbalimbali. Wakati wa ukoloni wa Uingereza azimio lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar. Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi katika Uganda.


  Kati ya lahaja za Kiswahili ni zifuatazo:


  Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili cha Kisasa.
  Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
  Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
  Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
  Kimvita: eneo la "Mvita" au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya pili pamoja na Kiunguja.
  Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)
  Kingwana: Kiswahili cha Kongo
  Shikomor: Kiswahili cha Komoro
  Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)
  Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)
  Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu
  Kimwani: Kaskazini ya Msumbiji na visiwa vya Kerimba
  Chimwiini: eneo la Barawa, kusini ya Somalia

  Sheng
  : Kiswahili cha mtaani Nairobi (Kenya) chenye maneno mengi ya asili ya Kiingereza, Gikuyu na lugha zingine za Kenya  ==


  Kurudi kwenye swali la mleta mada WANGU MTENZI


  Swali:

  Jibu:
  kuhusu sababu sijui .... ila nachofahamu ni kuwa Wakati wa ukoloni wa Uingereza AZIMIO lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar

  Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi katika Uganda..

   
 3. mtemiwaWandamba

  mtemiwaWandamba JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 536
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
   
 4. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  mtemiwaWandamba
  ... Kimtangata ... ni cha mwambao wa Tanga
   
 5. mtemiwaWandamba

  mtemiwaWandamba JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 536
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Ahsante mkuu.
   
 6. li sheng

  li sheng Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Asante, Mim binafsi nahisi labda kwanza niongezee Unguja mjini, mana akisema Mdonge au mkojani au Mmakunduchi utaondokea patupu.
  Sababu
  !. Kiunguja lugha yake haina lafdhi (TONE) iko mshazari (Straight) mfano haina ma re re re au le lele au kuimba kama watanga
  2.Kuinguja kimechanganya maneno mengi ya kujaliza kama kiiengereza Baskeli=Bicycle, kiarabu halwa =Haluwa , kihindi paisa = pesa etc ni lugha rafiki inakubalika
  3. Ina madaha au mayaaghani mfano, "Mmh yakhee unajua kama leo Ijumaa kuna harusi!", maneno ya mkato mfano twende zetu = twenzetu, etc
  4. Makao makuu ya utawala na kituo kikuu cha biashara au uchumi kilikuwa Unguja watu wengi walikuja Unguja hivyo kuongea kiunguja ni rahisi kuongea na waswahili wote.
  Natumai sijui utakuwa umeridhika?
   
Loading...