Nizar Khalfan aitwa Tottenham | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nizar Khalfan aitwa Tottenham

Discussion in 'Sports' started by BAK, May 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,905
  Trophy Points: 280
  Nizar Khalfan aitwa Tottenham
  Imeandikwa na Anatazia Anyimike; Tarehe: 13th May 2009 @ 10:37

  KIUNGO mahiri wa timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’, Nizar Khalfan ameitwa na timu ya Ligi Kuu ya England, Tottenham Hotspurs kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa na Mkurugenzi Mkuu wa Moro United, ambayo mchezaji huyo anachezea, Azim Dewji jana, ilieleza kuwa Nizar mwenye umri wa miaka 21, anatarajia kuondoka mwishoni wa mwezi huu, tayari kwa majaribio yatakayoanza Juni mosi chini ya kocha Harry Redknapp.

  “Tumefurahishwa na mwaliko wa Tottenham iliyoahidi kutoa nafasi zaidi kwa wachezaji wa Kitanzania kujaribiwa. “Ni bahati na heshima ya pekee kwa klabu kama Moro United na Tanzania kupata nafasi hii. Wametuahidi hawataishia kwa Nizar, bali watashirikiana nasi kutoa nafasi ya mara kwa mara kwa wachezaji wetu.

  ''Nasi kwa kuwa lengo letu ni kuona nchi hii inavuka milima na mabonde ya mafanikio katika soka, hatutaichezea bahati hii,'' ilisema taarifa hiyo ya Dewji. Taarifa ilieleza kuwa moja ya mikakati ya Moro United ni kusajili wachezaji wengi wenye umri mdogo, ili wakulie mikononi mwao wakiamini wataweza kufundishika na kuwa rahisi kuwapeleka katika klabu za Ulaya na kwingineko.

  Tottenham ni moja ya timu maarufu zinazocheza Ligi Kuu England na imewahi kutamba na nyota kadhaa kama Gary Lineker, Teddy Sheringham, Paul Gascoigne `Gaza’, Jurgen Klinsmann, Sol Campbell na Dimirtar Berbatov.

  Kama akifanikiwa kupata nafasi katika timu hiyo itakuwa bahati ya pekee, maana Tottenham ni moja ya timu za juu zinazoshiriki Ligi ya England, ambazo hazioni tabu kutoa fedha nyingi kununua wachezaji nyota na wenye uwezo.

  Baadhi ya nyota ambao inao hivi sasa, wengine wakiwa wamerudi tena baada ya kwenda katika baadhi ya timu maarufu barani Ulaya ni Robbie Keane, Ledley King, Jermain Defoe, Darren Bent, Aaron Lennon, Didier Zokora, Carlo Cudicini na Pascal Chimbonda.

  Hiyo itakuwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi miwili kwa mchezaji wa Tanzania kwenda kufanya majaribio kwa timu inayoshiriki Ligi Kuu ya England, baada ya mwezi uliopita mshambuliaji wa Taifa Stars na Yanga ya Dar es Salaam, Mrisho Ngassa kwenda kufanya majaribio katika timu ya West Ham United, ingawa hakufanikiwa, badala yake imeelezwa anatakiwa aende tena mwezi Julai.

  Nizar ambaye timu yake ya Moro United ilinusurika kushuka daraja, ikiwa ndiyo ya mwisho baada ya timu tatu zilizoshuka daraja katika Ligi Kuu Tanzania Bara iliyomalizika mwezi uliopita, aling’ara katika fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zilizofanyika Ivory Coast mapema mwaka huu.
   
 2. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Muda si mrefu wachezaji wa kitanzania wataanza kucheza soka ulaya wasikate tamaa
   
 3. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2009
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kila la kheri Nizar. Pia nawapongeza ma-agent mnao fight wachezaji wetu watoke.
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  oii hiki mbona kijeba chaApril 5,1975 lini tena kawa an 21yrs old?

  http://www.national-football-teams.com/v2/player.php?id=13316

  [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/2009_African_Championship_of_Nations_squads[/ame]
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Tunamtakia ushiriki mwema ajitume ili achaguliwe maana west africa wenzetu wanashinda huko kila siku ajili kujaribiwa tuu...tena wanajipeleka wenyewe kwenye free trials....hawachezi mbali na uwanja wa mazoenzi hata kwa mwaka mzima wanakomaa......ndipo wanatokea hapo hapo....
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  lakini mkuu nizar kijeba 34yrs old totenham unafikiri wajinga wamchukue kweli?
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Inawezekana mwandishi wa gazeti anataka kutuingiza kingi, yaani watu wame-stuck kwenye enzi zilee za kudanganya umri..poor us! lakini hata hicho chanzo cha habari ulichotupa nacho kinaonekana muflis hoi bin taaban na hakina tofauti na hilo gazeti..lol
   
 8. N

  Nampula JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona hii haijakaa sawa.....spurs wakachukuwe mchezaji over 30....haielekei..maana sidhani kama watamchukuwa hata kwa majaribio,maana wanajuwa fika kuwa tz ni nchi chovu kabisa ukija kwenye maswala ya soccer.nizar kaka yangu ongea na jamaa wa tff wakusawazishie kuhusu hiyo age yako sio.maana kama upo over 30 basi sahau kwenda spurs ya uk labda uende spurs ya mwananyamala.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160

  Belo,

  i always admire your sportsmanship but this one must be a hoax.... NIzar plays a very poor footbal in the premier na hata taifa stars, hawa madalali watatuua...
  I would be happy kama angeanzia leeds or belgium au hata MK dons na si tottenham!!!! atachukua namba ya nani?? hivi uliangalia gemu na congo??

  Sina nia mbaya but its all bad when we have 10 failed trials in the premier as compared to 5 passed trials in league one
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  ulitaka chanzo toka wapi?
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Chanzo chako kinachekesha..thats was the pwenti brazakaka..
   
 12. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  aaarrg wewe nae unakuwa kama X-paster....
   
 13. A

  Alpha JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Good News, and good luck to Nizar
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mimi sio PASTER bana.. Hapo ntakuwa naingilia 'kazi' za watu za ku-paste :D

  Sasa wewe unashindwa kuona chanzo chako kilivyo famba..yaani data pekee walioweka ni umri.

  Picha ya kuchora, na takwimu nyengine zooooote ni SIFURI..sasa hiki unaweza kukiita chanzo cha habari cha kuaminika?
   
 15. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Duh! Sie wa ubongo kwanza critics! Lakini ndo raha yetu! Habari ndo hiyo nizar anatakiwa na vijogoo wa varandani! Na miaka hiyo 34 wao wanamtaka tu! Nizar ni bonge la player na kesha turudisha sana senta. Kapiga kitale cha ukweli sana chan! Gemu ya tz na ivr.coast, alipiga mido ya kazi kichwani ribon white, si hilo 2 gemu ya kwanza weld kapu kwolifaya! Katupa raha shamba la bibi,tz 2-1 bukinabe, na gozi analijua mnoo! Mwache apande pipa! Niza go!
   
 16. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  YOYO ,Nizar Halfani nimesoma nae primary hata kama amedanganya umri nina uhakika hafiki hiyo miaka 34, atakuwa between 23-27
   
 17. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Hao mawakala wangewatafutia timu nchi kama Sweden,Denmark,Uswisi,France kuanzia England ni kugumu sana
   
 18. N

  Nampula JF-Expert Member

  #18
  May 14, 2009
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  well said bello
  kwa sababu atenda spurs kuuuza sura tu then arudi kijiwe ni bora angelianzia hata cyprus.nimeona ile anayofundisha ketsabaia ina mrwanda mmoja anacheza ss unaon alikoanza huko usijeshangaa nextseason tukamuona hata kwenye ligi hizi za kati kama france au hata holland
   
 19. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #19
  May 14, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  NIZAR hana miaka 34 kwani uliwahi kupitishwa mchujo wa wachezaji walipokuwa serengeti boys, yeye hakuguswa aliyepatikana ni NURDIN BAKARI.

  kwani hata kama ana miaka 34 kama wao wanamtaka hakuna tabu,nimeona comments michuzi blog juu ya kipa wa Man united VAN DER SAR kuwa alijiunga na machester akiwa na miaka 35 nimepitia website ya man united na kuona ni kweli.

  Yoyo hatua ya Nizar KWENDA Spurs ni ya kupongezwa hata kama hatapita kwani jina la nchi litaanza kuonekana.Drogba alifanya trials zaidi ya mara saba kabla ya kufanikiwa.

  ila kwa Nizar kwenda Spurs sio rahisi kwake ku break through kwani kuna Zakora na Jenas hawana permanent namba kwenye timu hiyo.
  kama alivyosema mdau mmoja hapo juu kuwa wangeanza na timu za ligi one au two huko wangetoka.

  umefika wakati wa hawa maajenti ku focus kwenye timu ndogo.leo hii tukiwaomba liverpool kuwa kuna mgosi anataka kufanya trial watampa nafasi lakini reality ni ngumu yeye kupenya.
  kila la kheri NIZAR
   
 20. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  mkuu mimi kuna jamaa wa musoma nilisoma nae tuko from one ana miaka 24!

  tehe tehe mkuu unanichekesha.....serengeti boys wale wengi wao vijeba...

  mkuu van de sar namba ingien ile kaanza soka la kimataifa tangu akiwa na 20 Ajax kacheza club kubwa juve fulham ndio man u......sasa huyu 34yrs old straight to toten?anyway namuombe kwa mungu afanikiwe ili iwe njia kwa wengine....
  goo nizar goo
   
Loading...