Niweke taa za watts ngapi? 3w, 6w au 12w?

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
502
938
Wadau, salaam!

Ceiling ya sitting room ya nyumba yangu ina ukubwa wa eneo wa 36m² (yaani urefu ni mita 6 na upana ni mita 6).

Nataka kuweka taa za surface. Nimeenda dukani nikakuta kuna taa za watts 3, zipo za watts 6, zipo za watts 9 na nyingine ni watts 12.

Baada ya kukuta hivyo, nikapata kigugumizi. Kigugumizi kilikuja kwa kuwa kwanza sijui watts kubwa/nyingi inamaanisha nini? Je, watts nyingi humaanisha ulaji wa umeme, humaanisha mwanga mwingi, humaanisha nini?
 
Mimi nimeweka za 13 Watts japo sijazingatia ukubwa wa sebule yangu.

Mimi nadhani ni chaguo lako tu kama mtu wa kupenda mwanga mkali weka hizo 12 Watts kama mtu wa giza kidogo weka angalao hizo 6watts.
 
Taa/bulb holders kwa hapo sebuleni ziko ngapi?

Bulb za LED za watts 3 zina mwanga wa kutosha na zinatumia umeme kidogo

E.g. una taa 4 za watt 3 kila moja ni sawa na 12w kwa saa 1. Kama taa hizo zitawashwa kwa saa 5 kwa siku ni sawa na 12w x 5hr = 60wh . Na kwa mwezi ni 60whx30 = 1800wh = 1.8kwh


Kama unataka mwanga mwingi basi tumia LED za watts 5 , ila umeme utatumika kwa kiasi kikubwa kidogo ya 3w.

Kwa hiyo: 4x5 =20x5 = 100 x 30 = 3000wh = 3kwh kwa mwezi.

Kutumia bulbs za zaidi ya watts 5 siyo muhimu kwani utaongeza gharama ya umeme bila sababu.
 
Back
Top Bottom