Niwatahadhirishe watawala wetu kuwa uamuzi wenu wa kuwaondoa wamachinga na kuwaacha "solemba" ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,156
Serikali hii hii iliyokuwa ikiwalea na kuwaacha wamachinga wafanye watakavyo bila kuzingatia taratibu za miji, ndiyo hiyo hiyo imewafukuza na kuwavunjia vibanda vyao, bila kujali kuwa watafanya wapi shughuli zao.

Siyo siri kuwa ni serikali hii hii ya CCM ndiyo iliyowalea wamachinga na kuwafanya wengi mno, ambao wamekuwa wakijipangia bidhaa zao popote pale, hata mbele ya maduka yanayolipa kodi TRA, bila wao kulipa kodi yoyote!

Ambaye alikuwa mstari wa mbele, kuwakingia kifua wamachinga, alikuwa ni Hayati, Rais Magufuli.

Bado wengi tutaendelea kukumbuka maneno yake aliyokuwa akitoa kwenye hotuba zake mbalimbali, kuwa Hawa wamachinga, ndiyo wapiga kura wangu, kwa hiyo wasiguswe, hata kama shughuli zao wanazofanya, wanavunja sheria za nchi!

Sasa inashangaza kwa serikali hiyo hiyo inayongozwa na CCM, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imekuja na msimamo tofauti, baada ya kufariki Rais Magufuli, kwa kuwaondoa kinyama wamachinga hao, bila kuwapangia sehemu nyingine za kufanya shughuli zao.

Matoleo yake ndiyo haya tunayoyaona kwa wamachinga hao kukaidi maagizo hayo ya serikali na kurejea kwenye maeneo yale yale na kuendelea na biashara zao!

Hii serikali ambayo haitoi ajira kwa mamilioni ya vijana wanaomaliza shule na vyuo mbalimbali, kila mwaka hapa nchini, hivi serikali inafikiri hao vijana watafanya nini, kama siyo kujitafutia Maisha kwa kuwa wamachinga??

Serikali hiyo hiyo ndiyo viongozi wake wanapokuwa kwenye majukwaa ya kisiasa, hawaishi kuhubiri kuwa vijana wasitegemee kuajiriwa na badala yake wajiajiri wao wenyewe.

Sasa Hawa vijana wanaotekeleza "maagizo" hayo ya viongozi wao, iweje leo waonekane kama wakosaji na kuadhibiwa kwa kuvunjiwa vibanda vyao vya kufanyia biashara??

Tutaendelea kuyakumbuka maneno ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, aliyesema kuwa suala la wamachinga wa nchi hii ni sawa na bomu, ambalo wakati wowote litaweza kulipuka na kutuletea maafa makubwa sisi wananchi wote wa nchi hii.

Watawala wetu nawaomba Sana muwe waangalifu Sana mnapolitafutia ufumbuzi suala hili "very sensitive and explosive" la wamachinga, ama sivyo halitatuacha salama, kwani tutatetekea wote, wamachinga na wasio wamachinga.

Ndiyo maana kwenye kichwa cha habari ya "story" yangu nimetamka kuwa watawala wetu kuwavunjia vibanda vyao wamachinga bila kwanza kuwatafutia maeneo mengine, ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu!
 
Ni Jambo Jema kurejea katika mstari, Cha msingi Ni serikali kupambana mazingira bora ya uwekezaji. Ili ajira nyingi uzalishaji zipatikane, pia mikopo maalumu kwa vijana Toka halmashauri ilenge miradi ya uzalishaji yenye tija uzalishaji na ajira mbali ya mikopo midogo kuongeza mtawanyo bidhaa.
 
Toa suluhisho lako

Umelalamika paragraph zote

Sasa toa suluhisho

Wewe Ungekuwa Rais ungefanya kitu gani?

Tumechoka kusoma habari za Wasomi ambazo hazina suluhisho
Suluhisho ni kwa serikali hii kutengeneza ajira nyingi na kuwaajiri wamachinga hao na siyo kuwavunjia vibanda vyao, bila kuwapangia maeneo Mbadala wa kufanya shughuli zao, kwa kuwa wamachinga hao wanafanya shughuli zao kwa ajili tu ya mkono uende tumboni
 
Ni Jambo Jema kurejea katika mstari, Cha msingi Ni serikali kupambana mazingira bora ya uwekezaji. Ili ajira nyingi uzalishaji zipatikane, pia mikopo maalumu kwa vijana Toka halmashauri ilenge miradi ya uzalishaji yenye tija uzalishaji na ajira mbali ya mikopo midogo kuongeza mtawanyo bidhaa.
Umeongea vyema mno👏👏

Siyo mawazo hayo ya watawala wetu wa kuwavunjia vibanda vyao wamachinga hao, bila kwanza kwatafutia maeneo Mbadala ya kufanyia shughuli zao
 
Nilichokiona viongozi wetu wanafanya haya kwa visasi na sikingine

Yaani hawataki kukosolewa pia hawataki kushauriwa
Ni kweli kabisa👏👏

Kwa kuwa badala ya kuongeza nafasi za ajira kwa vijana, wao ndiyo wanazipunguza na hao vijana wanapoamua kujiajiri, ndipo wanapopambana na hao maaskari wasio na huduma, kwa kuwavunjia vibanda vyao, ambao wengine wamevipata kwa mikopo ya benki, ambayo inatakiwa irejeshwe
 
Hatuwezi kufumbia macho watu waharibu mazingira na kukwepa kulipa kodi kwa kivuli cha Machinga, Serikali haijakurupuka, na nikukumbushe tu hii ni serikali ya awamu ya Sita,

Unaposema wapewe maeneo je watalipa Kodi???

Tukutane tarehe 4 kwenye Usafi wa Jiji la DSM, DAR Mpya, DAR inayong'ara.
 
Umeongea vyema mno👏👏

Siyo mawazo hayo ya watawala wetu wa kuwavunjia vibanda vyao wamachinga hao, bila kwanza kwatafutia maeneo Mbadala ya kufanyia shughuli zao
Maeneo mbadala kama yapi? Machinga anataka akae road reserve maana wapita njia ndio hasa wateja wake. Ukimpeleka kimbiji huko atamuuzia nani mashambani?

Ndio maana wanakomalia mjini wauze zao bidhaa
 
Hatuwezi kufumbia macho watu waharibu mazingira na kukwepa kulipa kodi kwa kivuli cha Machinga, Serikali haijakurupuka, na nikukumbushe tu hii ni serikali ya awamu ya Sita,

Unaposema wapewe maeneo je watalipa Kodi???

Tukutane tarehe 4 kwenye Usafi wa Jiji la DSM, DAR Mpya, DAR inayong'ara.
Uzuri wa wabongo ni kuwa anapopata nafasi ya kula huwa anasahau kabisa kuwa kuna wenzie ambao kula ni mtihani kwao wanapambana kwa kila hali yani ili wasife njaa!
 
Toa suluhisho lako

Umelalamika paragraph zote

Sasa toa suluhisho

Wewe Ungekuwa Rais ungefanya kitu gani?

Tumechoka kusoma habari za Wasomi ambazo hazina suluhisho
Suluhisho tuache ubinafsi, wamachinga ni raia wa nchii hii pia nao wanastahili kuishi vizuri kama ambavyo watawala wanaishi. Huduma nzuri za kijamii ni stahili yao hivyo serikali iangalie namna ya kuwawezesha waachane na umachinga wafanye yale yenye tija zaidi!

Serikali haiajiri watu kwa wakati inategemea hao watu waishije?
 
Wamepewa maeneo mbadala. Usiturudishe nyuma wewe. Aidha lazima utambue kwamba hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuwaajiri wasomi wote wanaohitimu vyuo vikuu. Hapa serikali ya mama naipongeza sana.

Back
Top Bottom